Makada waandamizi Makamba, Kinana ‘waitikia wito’ licha ya uvumi wa kuikacha CCM

Makada waandamizi waripoti CCM

Chanzo cha picha, CHAMA CHA MAPINDUZI

Maelezo ya picha, Makada waandamizi waripoti CCM
Muda wa kusoma: Dakika 2

Makatibu Wakuu wawili wastaafu wa chama tawala nchini Tanzania Chama Cha Mapinduzi (CCM) Abdulrahman Kinana na Yusuf Makamba leo Jumatatu wamejitokeza mbele ya kamati ya maadili ya CCM.

Viongozi hao walitakiwa kuhojiwa wiki iliyopita jijini Dodoma lakini hawakutokea na kuzua gumzo kubwa mtandaoni.

Hii leo, CCM kupitia ukurasa wake wa Twitter imethibitisha viongozi hao kufika mbele ya kamati katika ofisi za CCM jijini Dar es Salaam.

"Makatibu Wakuu Wastaafu Ndg. Yusuf Makamba na Ndg. Abdulrahman Kinana leo Februari 10, 2020 wamefika Ofisi Ndogo ya Makao Makuu ya CCM Lumumba Jijini Dar es Salaam kuitikia wito wa Kamati

ndogo ya Usalama na Maadili inayoongozwa na Makamu Mwenyekiti Bara Ndg. Philip Mangula," CCM ilithibitisha kupitia Twitter.

Viongozi hao wawili pamoja na Waziri wa zamani wa Mambo ya Nje wa Tanzania Bernard Membe wanatuhumiwa kwa makosa ya maadili na uongozi wa chama hicho.

Membe aliitikia wito na kuhojiwa Dodoma wiki iliyopita.

Kinana, Makamba waripoti CCM

Chanzo cha picha, CHAMA CHA MAPINDUZI

Maelezo ya picha, Kinana, Makamba waripoti CCM

Kutokuonekana kwa Kinana na Makamba kukazua gumzo kali nchini Tanzania huku baadhi mitandaoni wakidai kuwa vigogo hao wawili wamekikacha chama hicho.

Hata hivyo, ukurasa wa Twitter wa CCM haukueleza kinagaubaga mazungumzo baina ya viongozi hao na kamati ya maadili inayoongozwa na Philip Mangula.

Je, Kinana na Makamba wanatuhumiwa kwa makosa gani?

Makada hao, "wanakabiliwa na tuhuma za ukiukaji wa maadili kwa mujibu wa Katiba ya Chama na Kanuni ya Maadili na Uongozi."

sauti zao, wakiwa wakifanya nawasiliano kwa njia ya simu zilivujishwa kwenye mitandao nchini Tanzania wakizungumzia masuala mbalimbali kukihusu chama na mwenyekiti wake.

Sehemu ya mazungumzo yaliyovuja ya Mzee Yusuf Makamba na Kinana ni pamoja na kuandaa taarifa ya malalamiko dhidi ya 'mawanaharakati' Cyprian Musiba ambaye wanamtuhumu kwa 'kuwadhalilisha' bila

kuchukuliwa hatua yoyote na kuhoji analindwa na nani.

Ruka X ujumbe
Ruhusu maudhui? (Mitandao ya kijamii)

Mkala hii imebeba madhui yaliyotoka kwenye mitandao ya kijamii. Tunaomba ruhusa yako kabla kitu chochote hakija pakiwa, sababu wanaweza wakawa wanatumia Cookies na tekinolojia nyingine. Unaweza ukasoma sera sera ya kutumia cookies katika mitandao ya kijamii kabla ya kukubali. Kutazama maudhui haya chagua accept and continue

Onyo: Imetoka kwingine na inaweza kuwa na matangazo

Mwisho wa X ujumbe