Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Maiti ya kale iliyopo makumbusho ya Misri, mtu huyu alikufaje?
Timu ya wataalamu imeonekana kupata ufumbuzi wa kile ambacho kimekuwa kikichanganya umma kwa miongo mingi.
Swali ambalo wengi wanajiuliza, maiti ya kale ya Misri katika makumbusho ya Ulster ilifika hapo vipi?
Kulingana na utafiti uliofanywa kwa njia ya kisasa zaidi, iligundulika kuwa 'Takabuti' mtu huyo aliuawa kwa kudungwa kisu mgongoni.
Na siyo hilo tu, lakini wataalamu hao pia wanaamini kwamba huenda hata maiti hiyo asili yake siyo Misri, kulingana na uchunguzi wa vinasaba, jeni zake zinafanana zaidi na Ulaya ikilinganishwa na Misri ya sasa.
Uchunguzi uliofanywa kwa teknolojia ya kisasa na hata kisayansi umetoa ufumbuzi wa kifo chaTakabuti ambayo ilipelekwa Belfast in 1835.
Matokeo ya uchunguzi huo yanatolewa kwa Umma katika karne ya 185 yangu alipokufa.
Profesa Rosalie David, mtaalamu wa vitu vya kale vya Misri kutoka chuo kikuu cha Manchester, amesema utafiti umetoa ufafanuzi wa kina wa Takabuti na historia ya wakati alipokuwa hai.
"Ugunduzi ambao haukutarajiwa na wa msingi katika historia ya Ulaya umekuwa ufumbuzi wa aina yake katika historia ya Misri," amesema.
"Utafiti huu ambao ulihusisha teknolojia ya kisasa ya sayansi katika maiti za kale za Misri unaonesha vile taarifa mpya inaweza kupatika miaka elfu kadhaa baada ya kifo.
"Timu yetu - inayojumuisha taasisi na wataalam - ilikuwa katika nafasi ya kipekee ya kushirikishana utaalamu wao na teknolojia kwa utafiti mpana wa namna hii."
Profesa Eileen Murphy, mtaalam wa mabaki ya binadamu kutoka chuo kikuu cha Queen huko Belfast, ameelezea matokeo ya utafiti huo kama kitu cha "kustaajabisha
"Awali mara kwa mara Takabuti alisemekana kwamba anaonekana mwenye amani akiwa kwenye jenezani lakini baada ya utafiti huu tumebaini kuwa muda wake wa mwisho alipitia madhila makubwa kwasababu aliuawa."
Mwaka 2009, makala ya BBC Ireland Kaskazini, ilionyesha vile ambavyo Takabuti angelionekana.
Pia utafiti huo uligundua vitu kingine cha ajabu mwilini mwake. Vitu hivyo vinasemekana kwamba vilitumika kuziba jeraha la kisu alilopata huku moyo wake ukipatikana na kwamba upo katika sehemu stahiki.
Tunachofahamu kumhusuTakabuti
- Aliishi Thebesi wakati wa utawala wa 25 karibia miaka 2,600 iliyopita.
- Baba yake, Nepare, alikuwa kasisi katika hekalu la Amun, Karnak na mama yakeTasenirit, alikuwa kijakazi
- Inaaminika kwamba Takabuti alikuwa ameolewa kwa sababu alikuwa kimada wa Thebesi
- Aliaga dunia akiwa katika umri wa miaka ya 20 na kuzikwa karibu na hekalu la Hatshepsut
- Alikuwa na urefu wa futi 5
- Takabuti aliga dunia baada kudungwa kisu mgongoni
- Mama yake Takabuti alikuwa mwenye asili ya Ulaya au Mzungu. Hata hivyo, kwa utafiti wa hivi karibuni, hakuna uhakika kwambaTakabuti alikuwa ni raia wa kigeni nchini Misri
- Bado moyo wake upo: japo utafiti wa awali haukufanikiwa kubaini hili.
- Alikuwa na meno zaidi (33 badala ya 32) jambo ambalo hutokea kwa asilimia 0.02% ya watu
- Alikuwa na mifupa zaidi jambo ambalo hutokea kwa asilimia 2 tu ya watu duniani
Dkt Greer Ramsey, mtunzaji wa akiolojia katika Makumbusho ya Taifa ya Ireland Kaskazini, amesema kwamba kuendelea kwa teknolojia ya kisayansi kulikuwa kiungo muhimu kwa utafiti huo.
"Katika miaka ya hivi karibuni, maiti ya Takabuti pamoja na nywele zake ulikuwa umefanyiwa uchunguzi wa miale, pamoja na kifaa cha kupima umri wa vitu vya kale.
"Majaribio ya hivi karibuni yanajumuisha vinasaba na utafiti zaidi unaotumia miale ambao umewesha kupatikana kwa taarifa mpya na za kina zaidi."
Aliongeza: "Thibitisho la kwamba moyo wa Takabuti bado upo ni jambo ambalo haliwezi kuchukuliwa kwa uzito mdogo kwasababu katika Misri ya kale, kiungo hiki cha mwili kilikuwa kinatolewa punde tu baada ya mtu kufa na kupimwa kubaini ikiwa mtu huyo ameishi maisha ya furaha au la.
"Iwapo moyo ungepatikana ukiwa na uzito mkubwa, ungeliwa na zimwi 'Ammit' na kuaminika kwamba maisha yako ya baada ya kufa yangeishia hapo."
Takabuti alipatikana mji wa kale wa Misri eneo la Thebesi na Thomas Greg wa Marekani na mwili huo ukupelekwa Belfast 1834.
Tangu maiti ya Takabuti ilipowekwa katika makumbusho ya Ulster - anayeaminika kufa akiwa katika umri wa miaka ya 20, amekuwa kivutio kikuu cha utalii.
Utafiti huo wa hivi karibuni ulifadhiliwa na marafiki wa makumbusho ya Ulster.