Kobe Bryant: Uchunguzi wa chanzo cha ajali ya ndege unaendelea

Wachunguzi wa Marekani wanafanya uchunguzi kubaini chanzo cha helikopta iliyomuua mchezaji wa zamani wa mpira wa kikapu Kobe Bryant , kuanguka siku ya jumapili huko Califonia.

Watu wote tisa waliokuemo kwenye helkopta hiyo walifariki akiwemo binti wa mchezaji huyo Gianna..

Wachunguzi wanalenga kuangazia upande wa hali ya hewa na kuangalia itilafu za kiufundi kama zilikuepo.

Bryant alkuwa anafahamika kama mchezaji bora katika historia ya mpira wa kikapu.

Aliipatia ushindi wa NBA , timu yake ya Los Angeles Lakers mara tano pamoja na medali mbili za dhahabu katika mashindano ya Olimpiki.

Mchezaji huyo alistaafu kucheza mpira wa kikapu mwezi Aprili mwaka 2016.

Salamu za rambirambi zimekuwa zikimiminika kutoka kwa mashabiki wake, wachezaji wenzake wa mpira na watu maarufu katika maeneo mbalimbali duniani, huku wakimpongeza kwa kazi nzuri aliyoionyesha wakati anacheza mpira wa kikapu.

NBA imefuta mechi ya Lakers na Clippers ambayo ilipangwa kufanyika siku ya Jumanne.

Uchunguzi utaangazia nini?

Wachunguzi kutoka mamlaka ya anga na bodi ya taifa ya usalama wa usafirishaji wanakutana ili kuanza kufanya uchunguzi wa ajali hiyo kwa utofauti.

Watu wapatao 20 huko LA watafanya kazi na mamlaka ya anga kuchunguza helikopta hiyo iliyotengenezwa na kampuni gani na kuchunguza injini yake, imeripotiwa kutoka Washington.

Uchunguzi ulianza siku ya jumatatu kwenye masalia ambayo ya ndege hiyo ambayo yalikuwa yameharibika vibaya.

Shirika la kijasusi la FBI linasaidiana na wafanyakazi wa bodi ya usalama wa usafirishaji kuweka picha za tukio katika utaratibu sahihi.

Ndege hiyo inayofahamika kama Sikorsky S-76B illianguka pembezoni mwa mji wa Calabasas , magharibi mwa Los Angeles siku ya jumapili.

Hali ya hewa ya ukungu wakati ndege hiyo ilipoanza safari na polisi katika wa eneo hilo walisema kuwa inawezekana helikopta hiyo ilianguka kutokana na hali ya hewa kuwa mbaya .

Rubani alitaka usimamizi maalum ili ndege hiyo iweza kuruka chini ya kiwango cha hali ya hewa kilichopo, mjumbe wa bodi ya taifa ya usafirishaji salama Jennifer Homendy, ambaye alienda kwenye eneo ambalo ajali ilitokea kuchukua ushahidi.

Alieleza pia kuwa helikopta hiyo iliyozunguka kwa dakika 12 kabla ya kupewa kibali cha kuondoka.

Rubani alimuomba muongozaji msaada wa kuongozwa kwa helikopta hiyo ili kuzuia ajali lakini aliambiwa kuwa ndege ilikuwa ndogo sana kufuatiliwa na rada.

Dakika chache baadae ,rubani alisema kuwa anapanda mlima ili kukwepa mawingu , aliongeza.

Helikopta ilipanda mlima na kwenda tofauti na uelekeo, kwa mujibu wa taarifa za kwenye rada kabla mawasiliano hayajapotea, "usawa ambao ajali ilitokea".

Rubani aligundua kuwa kuna shida wakati alipoanza safari kwa kukosa muongozo, mkurugenzi wa usalama wa anga bwana Thomas Anthony,aliiambia BBC.

"Ndio maana kuna umuhimu wa kutumia vifaa vya ndege, ambavyo vinatoa muongozo.

Ingawa aliongeza pia kuwa sababu ambayo ilisababisha ndege hiyo kupata ajali, wachunguzi wanapaswa kuangalia mambo gani ambayo yanaweza kusababisha janga kutokea."

Hata hivyo aliongeza kusema kuwa ajali ya ndege hiyo haikusababishwa na jambo moja na wachunguzi wanapaswa kuangalia zaidi mambo gani ambayo yalisababisha ajali hiyo.

Helikopta hiyo yenye namba S-76 ni ndege ambayo imetengenezwa vizuri na inatumika maeneo mengi duniani, alisema na kuongeza kuwa ndege hiyo ina injini mbili hivyo hata injini moja ikishindwa kufanya kazi nyingine ina uwezo wa kuendelea kufanya kazi.

Bi. Homendy alisema pia helikopta hiyo haikuwa na kisanduku cha kunakili sauti yaani 'black box'.

Kwa nini Kobe Bryant alikuwa anasafiri na helikopta?

Bryant alikuwa anaenda kufundisha klabu aliyokuwa anachezea binti yake kwenye mashindano ya vijana.

Alikuwa anapenda kutumia helikopta ili kukwepa foleni ya mjini Los Angeles.

"Los Angeles ni maarufu kwa kuwa na foleni kubwa barabarani" alisema Profesar Michael Manville, kutoka taasisi ya usafirishaji.

Foleni hii inatokana na kutokuepo kwa gharama ya kulipia barabara na uchumi wa mji kukua hivyo kuwafanya wakazi wa eneo hilo kushindwa kuacha kuendesha magari yao na kufanya foleni kuwa kubwa.

Kwa mujibu wa utafiti wa mwaka 2018 , dereva wa Los Angeles lost huwa wanapoteza muda wa saa 128 katika foleni kwa mwaka.

Safari ya Bryant, ilianzia nyumbani kwake ambako ni karibu na fukwe za Newport kuelekea taasisi ya michezo ya Mamba iliyoko Thousand Oaks, ambako ingemchukua zaidi ya saa bila kukaa kwenye foleni - ingawa ingeweza kumchukua zaidi ya saa tatu kama hali ya hewa si nzuri.

Kina nani wengine walikuepo kwenye helikopta hiyo?

Mamlaka imepata miili mitatu tayari iliyokuwa katika ndege hiyo ingawa, hawajatajwa rasmi ni kina nani.

Wanafamilia na wafanyakazi wenzie wanasema kuwa kocha wa timu ya mpira wa magongo ya Orange, John Altobelli ni miongoni mwa abiria wa helikopta hiyo akiwa na mke wake Keri pamoja na binti yao Alyssa ambaye alikuwa anacheza timu moja na Gianna.

Christina Mauser, ni kocha wa mpira wa kikapu katika shule aliyokuwa anasoma Gianna alikuwa katika ndege hiyo, mume wake aliandika katika mtandao wa Facebook.

Vyombo vya habari vya Marekani vimeripoti salamu za rambirambi kwa familia ya Sarah Chester, na binti yake Payton, ambao wanadaiwa kuwa miongoni mwa watu ambao walikuwa ndani ya helikopta hiyo na Ara Zobayan ambaye alikuwa rubani.

Kwa nini Kobe Bryant alikuwa maarufu sana?

Ni bingwa wa mashindano ya NBA mara tano ,

Vilevile Bryant alicheza kwenye timu ya Los Angeles Lakers kwa miaka 20 kabla hajastaafu kucheza mwaka 2016.

Mafanikio yake yanajumuisha kuwa mchezaji bora wa NBA mwaka 2008 pamoja na kuwa bingwa mara mbili wa NBA kwa kufunga katika mashindano ya Olimpiki.

Alijulikana kwa kupata pointi 81 dhidi ya timu ya Toronto Raptors mwaka 2006, mchezo wa pili mkubwa katika historia ya NBA.

Bryant alishinda tuzo za Oscar kama mchezaji wa filamu fupi mwaka 2018 filamu hilo ilikuwa 'Dear Basketball', filamu ya dakika tano iliyoangazia barua moja ya michezo aliyoandika mwaka 2015.

Bryant na mke wake, Vanessa, walikuwa na watoto wengine wakike watatu ambao ni Natalia, Bianca na Capri.

Bryant alishutumiwa kwa kesi ya unyanyasaji wa kingono mwaka 2003, na binti mwenye umri wa miaka 19-aliyekuwa akifanya kazi katika mgahawa wa Coloradot. Alikanusha madai hayo, na kusema kuwa walikuwa na mahusiano ya kimapenzi ya kukubaliana.

Kesi hiyo ilifutwa baada ya mtu aliyemshtaki kukataa kutoa ushahidi mahakamani.

Ingawa baadae aliomba radhi kwa kitendo kile na kusema sababu ilikuwa msichana aliyekuwa naye hakuwa na mtazamo sawa na wake wakati walipokuwa kwenye mahusiano yao.