Coronavirus: Mataifa ya Afrika yaimarisha hatua ya kukabiliana na mlipuko

Mataifa ya Afrika mashariki yametangaza hatua ya tahadhari na mipango ya kukabiliana na virusi vya Corona vinavyosababisha maradhi ya kupumua huku idadi ya watu waliofariki kutokana na mlipuko wa virusi hivyo nchini China ikiongezeka na kufikia 26.

Afrika ni mshirika mkuu wa kibiashara wa China na maelfu ya raia wa nchi hiyo wanafanya kazi katika mataifa tofauti barani humo.

Kenya na Uganda zimeanza kuwafanyia uchunguzi abiria wanaowasili katika mataifa hayo kutoka maeneo mbali mbali duniani.

Mataifa ya Sudan Kusini na Rwanda yametoa ushauri kwa umma na wasafiri kuzingatia ushauri waliopewa.

Maafisa wa China wanasema visa vipya 830 vya maambukizi ya virusi hivyo vimethibitishwa.

Hayo yanajiri wakati ambapo miji iliyowekwa chini ya uangalizi wa hali ya juu ikifikia 10.

Wataalamu kutoka shirika la Afya Duniani wamesema ni mapema kutangaza mlipuko wa virusi vya corona kuwa janga la kimataifa.

Kufikia sasa karibu miji 10 katika mkoa wa kati nchini China ambayo ina watu milioni 60 imewekewa vikwazo vya usafiri ili kukabiliana na kusambaa kwa virusi hivyo.

Siku ya Alhamisi mgonjwa aliyekuwa na virusi vya corona alifariki karibu na mkoa wa Hebei - ikiwa ni kisa cha kwanza kuripotiwa katika mkoa huo.

Kifo kingine kimeripotiwa katika mkoa wa kaskazini mashariki mwa Heilongjiang ambao unapakana na Urusi.

Lakini athari iliyosababishwa na mlipuko wa virusi vya corona haujashuhudiwa katika mkoa wa Hubei pekee.

Mamlaka nchini China imefutilia mbali matamasha makuu ya umma katika maeneo mengine ya nchi ikiwa ni pamoja na:

  • Kufunga kwa ukumbi wa Beijing palace
  • Kufutilia mbali tamasha la sinagogi la kimataduni mjini Beijing
  • Kufutiliwa mabli kwa tamasha la kimataifa la Hong Kong
  • Kufutiliwa mbali kwa shindano la kandada la kila mwaka Hong Kong
  • Kufutiliwa mbali kwa tamasha la mwkampya wa China mjini Macau

Hali ya maambukizi kimataifa ikoje?

Mataifa ya Vietnam na Singapore siku ya Alhamisi yalithibitisha visa vya maambukizi na kuungana na Thailand, Japan, Taiwan, Korea Kusini na Marekani.

Nchi nyingi zimetangaza hatua ya kufanyia wasafiri uchunguzi raia wa China wanaowasili katika viwanja vyao vya ndege, ikiwa ni pamoja na viwanja vya kimataifa vya ndege mjini Dubai na Abu Dhabi.

Taiwan imewapiga marufuku raia wa China kutoka mkoa wa Wuhan huku wizara ya mambo ya nje ya Marekani ikiwaonya raia wa nchi hiyo wanaosafiri China kuwa waangalifu.