Coronavirus: Virusi vipya vyasababisha kifo chengine huku usambazaji kupitia binadamu ukithibitishwa

Idadi kuu ya visa vya ugonjwa huu nchini China imepatikana katika mji wa Wuhan

Chanzo cha picha, EPA

Maelezo ya picha, Idadi kuu ya visa vya ugonjwa huu nchini China imepatikana katika mji wa Wuhan

Mwathiriwa wa nne nchini China amefariki kutokana na virusi vipya ambavyo vimesambaa nchini humo , huku maafisa wakithibitisha kwamba vinaweza kusambazwa kupitia mtu mmoja hadi mwingine.

Mzee mwenye umri wa miaka 89 alikuwa mwathiriwa wa hivi majuzi wa virusi hivyo ambavyo husababisha aina moja ya homa ya mapafu.

Aliishi mjini Wuhan, mji unaodaiwa kuwa chanzo cha mlipuko huo.

Zaidi ya visa 200 kufikia sasa vimeripotiwa katika miji mikuu nchini China ikiwemo Beijing na Shanghai.

Shirika la afya duniani WHO linafikiria kutangaza janga la dharura la kiafya kama ilivyofanya wakati wa homa ya nguruwe na Ebola. Uamuzi huo utafanywa katika mkutano siku ya Jumatano.

Wahudumu 15 wa fya mjini Wuhan wameambukizwa virusi hivyo

Chanzo cha picha, Reuters

Maelezo ya picha, Wahudumu 15 wa fya mjini Wuhan wameambukizwa virusi hivyo

Tume ya kitaifa ya afya siku ya Jumatatu ilithibitisha kwa mara ya kwanza kwamba maambukizi hayo yanaweza kusambaa kupitia wanadamu.

Ilisema kwamba watu wawili mjini Guangdong waliambukizwa kwa njia hiyo. Katika taarifa nyengine,

Tume ya afya ya mjini Wuhan ilisema kwamba takriban wahudumu 15 wa afya waliambukizwa ugonjwa huo , huku mmoja wao akiwa katika hali mahututi.

Wafanyakazi hao wanadaiwa kuambukizwa na virusi hivyo baada ya kugusana na wagonjwa. Wote wametengwa huku wakipata matibabu.

Je ugonjwa huo umeenea maeneo gani?

Ugonjwa huo mara ya kwanza uligunduliwa mjini Wuhan, mji uliopo katikati ya China ulio na idadi ya watu milioni 11 , mwaka uliopita. Kuna takriban visa 218 vya virusi nchini China kulingana na WHO.

Kuna visa kadhaa ambavyo tayari vimebainika Ulaya: Viwili nchini Thailand kimoja Japan na chengine Korea Kusini. Wale walioambukzwa walikuwa wamewasili kutoka Wuhan hivi majuzi.

Presentational white space

Mamlaka katika mataifa mengi ikiwemo Australia, Singapore, Hong Kong, Taiwan na Japan zimeimarisha uchunguzi wa abiria wanaosafiri kwa ndege kutoka Wuhan.

Marekani pia imetangaza mikakati kama hiyo katika viwanja vya ndege vya San Francosco , Los Angeles na New York..

Nchini Australia mtu mmoja ambaye alikuwa amesafiri kuelekea Wuhan ametengwa na anafanyiwa vipimo.

China ndio taifa linalochangia watalii wengi zaidi nchini Australia , huku zaidi ya watu milioni moja wakilitembelea taifa hilo mwaka uliopita.

Je virusi hivyo vinasambaa kwa kasi gani?

Kuna hofu kwamba virusi hivyo vinaweza kusambaa rahisi - na katika maeneo mengine nchini huku mamlioni ya raia nchini China wakijiandaa kusafiri kuelekea nyumbani kwa siku kuu ya kusherehekea mwaka mpya nchini China wiki hii.

Mamilioni ya raia wa China wanasafiri kuelekwa makwao ili kusherehekea sikukuu ya mwaka mpya nchini.

Mamilioni ya raia wa China wanasafiri kuelekwea makwao ili kusherehekea sikukuu ya mwaka mpya nchini humo

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Mamilioni ya raia wa China wanasafiri kuelekwea makwao ili kusherehekea sikukuu ya mwaka mpya nchini humo

Hatua ya raia kusafiri kutoka eneo moja hadi jingine inamaanisha kwamba mamlaka hazitaweza kuchunguza kuenea zaidi kwa ugonjwa huo. Wataalam wanasema kwamba tayari kunaweza kuwa na visa vingi vya maambukizi kutoka kwa ugonjwa huo.

Ripoti ya kituo cha uchanganuzi wa magonjwa katika chuo kikuu cha Imperial mjini London kimesema kuwa kunaweza kuwa na zaidi ya maambukizi 1,700.

Hatahivyo , Gabriel Leung, mkuu wa idara ya matibabu katika chuo hicho cha Hongkong anasema kwamba maambukizi hayo yanaweza kufikia watu 1,300 kufikia sasa.

Mlipuko huo umesababisha virusi kwa jina Coronavirus ambavyo vimesababisha vifo vya watu 774 kati ya karibia watu 2000 nchini , wengi wakiwa barani Asia na ambapo China ilishutumiwa kwa kuficha.

Rais wa China Xi Jinping ametaka juhudi kuchukuliwa ili kuzuia mlipuko huo kulingana na vyombo vya habari, ikiwemo kusambaza habari na kuchukua hatua za haraka.

Je tunajua nini kuhusu virusi hivi?

Sampuli ya virusi vya ugonjwa vilivyochukuliwa kutoka kwa mgonjwa na kuchunguzwa katika maabara na maafisa wa serikali pamoja na wale wa shirika la afya duniani WHO zimethibitisha kwamba ugonjwa huo ni ule wa Coronavirus.

Virusi hivyo ni familia kubwa ya virusi sita na kirusi hicho kipya kitaongeza idadi hiyo kufikia saba ambapo ni maarufu kwa kusababisha maambukizi miongoni mwa binadamu.

Virusi hivyo vinaweza kusababisha homa, lakini pia vinaweza kusababisha ugonjwa mbaya wa Sars ambao uliwauwa watu 774 kati ya 8,098 walioambukizwa katika mlipuko ulioanza China 2002.

Uchanganuzi wa jeni za ugonjwa huo mpya unaonyesha kuhusishwa karibu na ugonjwa wa Sars zaidi ya ugonjwa wowote wa Coronovirus.

Mamlaka ya China imeripoti visa 139 vipya vya ugonjwa huo usiojulikana katika siku mbili, ikiwa ni mara ya kwanza kwa maambukizi hayo kuthibitishwa nchini humo nje ya mji wa Wuhan.