Kipsang bingwa wa Marathon apigwa marufuku

Chanzo cha picha, Huw Evans picture agency
Wilson Kipsang, aliyekuwa akishikilia rekodi ya dunia ya mbio za marathon na Bingwa wa London marathon amepigwa marufuku kwa kushindwa kuelezea pale alipo na pia kukiuka masharti ya vipimo kwa kuharibu ushahidi.
Shirikisho la riadha la Kenya limetangaza kumpiga marufuku mwanariadha huyo wa Kenya Ijumaa.
Kama sehemu ya kuhakikisha sheria ya kukabiliana na utumiaji wa dawa haramu inafuatwa, wanariadha washiriki wa michezo, lazima waeleze watakuwa wapi katika kipindi cha saa moja kila siku, siku saba za wiki, na miezi mitatu kabla, pamoja na pale watakapokuwa wakifanya mazoezi kila siku.
Kushindwa kueleza mara tatu pale utakapokuwa ndani ya kipindi cha miezi 12 mtu anapigwa marafuku.








