Shambulio la kambi ya kijeshi Niger: Takriban wanajeshi 73 wameuawa

Wanamgambo wamewaua takriban wanajeshi 73 katika shambulio dhidi ya kambi moja ya kijeshi magharibi mwa Niger, kulingana na jeshi.

Wanajeshi 12 pia walijeruhiwa katka shambulio hilo likiwa ndio baya zaidi kwa miaka kadhaa siku ya Jumanne.

Waziri wa Nigera Issoufou Katambe aliambia BBC kwamba idadi kuu ya magaidi 'imezuiliwa '. hakuna kundi lililosema lilihusika na mauaji hayo , lakini wapiganaji wanaohusishwa na Islamic State na wale wa Boko Haram wanatekeleza operesheni zao nchini humo.

Bwana Katambe aliambia BBC kwamba kulikuwa na mapambano makali katika eneo la Inates karibu na mpaka na Mali.

Amesema kuwa mamia ya wapiganaji walishambulia kambi hiyo.

Tunachokijua kuhusu shambulio

Shambulizi hilo lilifanyika yapata maili 30 kutoka eneo la Ouallam, ambapo wanajeshi wanne wa Marekani walifariki pamoja na wanajeshi wengine wanne wa Nigeria miaka miwili iliopita wakati doria yao iliposhambuliwa katika uvamizi.

Wapiganaji wa Kiislamu wamekuwa wakitekeleza mashambulizi katika eneo lote la jangwa la sahara , wakiwateka raia wa kigeni na kulenga michezo inayopendwa sana na raia wa kigeni .

Jeshi lililobuniwa kuweka usalama katika eneo hilo limeshindwa kuzuia ghasia hizo. Baadhi ya wachanganuzi wamesema kwamba uvamizi wa kambi za kijeshi unalenga sio tu kuiba silaha lakini kupanua ardhi inayomilikiwa na wanajihad hao.

Shambulio hilo lilijiri siku kadhaa kabla ya kufanyika kwa mkutano nchini Ufaransa kati ya rais Emmanule Macron na viongozi wa mataifa ya Afrika magharibi kuzungumzia usalama katika eneo hilo.

Serikali ya Nigeria mapema iliomba kuongezewa muda wa miezi mitatu ili kutangaza hali ya tahadhari , ambayo mara ya kwanza ilitangazwa miaka miwili iliopita.

Jeshi la Niger linang'ang'ania kudhibiti kuenea kwa makundi yaliojihami. Katika wiki za hivi karibuni kumekuwa na mashambulio yalioongozeka kutoka kwa washirika wa kundi la Islamic State katika eneo la taifa hilo lililopo karibu na Mali.

Wapiganaji wanaotekeleza operesheni zao katika eneo hilo na Niger ni wanachama wa kundi la Mataifa matano ya Sahel G5 - pamoja na Burkina Faso , Mali, Mauritania na Chad ambayo inalenga kukabiliana na mashambulizi hayo.

Ni eneo tete

Kulingana na Reuters wanajeshi watatu na wapiganaji 14 waliuawa siku ya Jumatatu katika shambulio dhidi ya kambi nyengine katika eneo la Agando magharibi mwa jimbo la Tahoua, kulingana na wizara ya Ulinzi.

Maelfu ya raia na wanajeshi wameuawa katika eneo hilo la Sahel ambapo mapigano hayo yalianza wakati wapiganaji walipoasi kaskazini mwa Mali 2012.

Mgogoro kwa sasa umeenea hadi katikati mwa Mali na taifa jirani la Burkina Faso na Niger.

Mashambulizi yanaendelea licha ya wanajeshi 4500 wa Ufaransa kupelekwa katika eneo hilo ikiwa ni miongoni mwa operesheni Barkhane ili kuwasaidia wanajeshi wa mataifa hayo.

Wanajeshi 13 wa Mali waliuawa mwezi uliopita wakati ndege mbili za kijeshi zilipogongana wakati wa operesheni dhidi ya wapiganaji wa taifa hilo waliopo kaskazini likiwa ndio pigo kubwa kuwahi kulikabili jeshi la Ufaransa katika miongo minne.

Jinsi makundi hayo yanavyofadhili operesheni zao

Utafiti uliofanywa na taasisi ya usalama katika kipindi cha miaka miwili iliopita unaonyesha uhusiano kati ya wapiganaji walio na itikadi kali pamoja na vitendo vya mauaji vinavyoendelea katika maeneo ya mipakani ya Liptako-Gourma.

Makundi hayo yanafaidika kutokana na watoa huduma na wadhibiti wa vitendo hivyo.

Ili kuendeleza vitendo hivyo watoa huduma hizo hutafuta fedha, chakula na uwezo wa kuendeleza operesheni hizo mbali na kuimarisha maeneo wanayotoka ikiwemo kupitia kusajili wapiganaji wapya.

Kundi hilo limeanzisha mikakati ya kuchangisha fedha , wizi wa mifugo mbali na uchimbaji wa madini. Wizi wa mifugo unafanyika kwa wingi katika eneo hilo hususan katika mpaka wa Mali na Niger na katika maeneo mengine ya katikati ya taifa la Mali.

Mifugo iliobwa huchukuliwa na kuuzwa katika masoko ya karibu ama kuuzwa wachinjaji. Katika maeneo mengine makundi ya wapiganaji wenye itikadi kali wameanzisha kuwatoza wakulima kodi ya mifugo yao ili kupata usalama.

kitendo hicho kimeenea sana katika mpaka katika ya Mali na Niger. Baadhi ya makundi pia yanaishi katika maeneo mashariki mwa Burkina Faso yenye dhahabu. lengo la ni kufanya biashara ya madini hayo.