Wafungwa wamenyimwa matibabu ya HIV falme za kiarabu

Wafungwa kutoka mataifa ya nje, waliopo katika moja ya magereza ya falme za kiarabu wamekua wakinyimwa matibabu ya virusi vya HIV kwa mujibu wa shirika la kutetea haki za Binadamu la Human Rights Watch.

Mfungwa wa zamani wa gereza la Dubai amesema kuwa alikua akicheleweshewa, kukatishwa ama kunyimwa kabisa matibabu yake.

Sheria za kimataifa juu ya wafungwa zinasema kuwa wana haki ya kupewa matibabu na huduma za kiafya.

BBC imejaribu kuwasiliana na ubalozi wa falme za kiarabu London lakini hawajasema lolote.

Unaweza pia kusoma;

''Falme za kiarabu inatakiwa kutoa matibabu, ikiwemo madawa kwa wafungwa wote waliopo kwenye gereza zao'' amesema Michael Page mkurugenzi msaidizi wa Human Rights watch mashariki ya kati.

wafungwa wa kigeni wenye virusi vya HIV waliopo Al Awir walikua wakipatiwa matibabu yao ndani ya miezi mitatu hadi sita, lakini hawapatiwi matibabu ya muda mrefu na yenye uhakika.

Wafungwa wenye virusi vya HIV wamewekwa katika eneo tofauti na wafungwa wengine, na ripoti zinasema huo ni ubaguzi na unyanyasaji wa hali ya juu.

Chanzo kimoja kimewaambia Human rights Watch kuwa mgonjwa mmoja alipisha miezi minne bila matibabu yake stahili, na akapatiwa majibu ya vipimo kuwa hali inazidi kuwa mbaya.

Kama mwanachama wa umoja wa mataifa Falme za kiarabu wanatakiwa kupambana na maambuziki ya visuri vya Ukimwi hadi kufikia 2030.

Umoja wa mataifa katika viwango vyake inaeleza kuwa wafungwa lazima wapewe matibabu na usaidizi wa kiafya mara wakihitaji.

Mapema mwaka huu, wataalamu wa haki za binaadam wamekemea hali mbaya ya wakimbizi huko Falme za kiarabu.

wanasema kuwa Ahmed Mansoor aliyekamatwa kwa kusema uongo kwenye mitandao ya kijamii, hakua na kitanda cha kulala wala maji, na pia alipatiwa mateso.