Urusi kuingia Afrika: Je itaimarisha nguvu ya bara hili?

President Putin and Basir

Chanzo cha picha, Getty Images

Urusi inapokea mkutano mkubwa na viongozi wa Afrika juma hili, ishara ya kukua ikiwa nchi yenye umuhimu katika ukanda wa Afrika.

Muungano wa usovieti ulikuwa na nafasi kubwa barani Afrika lakini uliyumba kiuchumi na kisiasa baada ya kipindi cha vita baridi.

Raisi Vladimir Putin amesema kuimarishwa kwa mahusiano na nchi za Afrika ni moja kati ya masuala ya sera za mambo ya nje zinazopewa kipaumbele na nchi yake.

Je uwepo wa Urusi barani Afrika hivi sasa una umuhimu gani?

Valdmir Putin
Maelezo ya picha, Rais wa Urusi Vladmir Putin

Hatutoi mitazamo yetu, kwa kuheshimu kanuni kwamba ''matatizo ya Afrika yatatatuliwa na Waafrika wenyewe'' kwa namna ambavyo Waafrika watapendekeza.

Hata hivyo hivi karibuni Gazeti la Washington Post lilizungumzia kuhusu Urusi "kutafuta mikataba kwa nguvu na mahusiano ya kiusalama" wakati ushawishi wa Marekani katika bara la Afrika ukiendelea kupungua.

Unaweza pia kusoma:

Katika mahojiano na shirika la habari la Urusi, kabla ya mkutano wa juma hili, Rais Putin alisema: ''Uhusiano wa Urusi na Afrika unaimarika,'' na kuzungumzia masuala ya kusaidia kama:-Msaada wa kisiasa na kidiplomasia-Masuala ya usalama-Msaada wa kiuchumi-Ushauri kuhusu kudhibiti maradhi-Misaada ya kibinaadamu-Elimu na mafunzo ya ufundi.

Second World War victory march re-enactment

Chanzo cha picha, Getty Images

Urusi imekuwa ikiimarisha mahusiano na baadhi ya nchi za Afrika, viongozi 12 wa nchi za kiafrika wamewahi kutembelea Moscow tangu mwaka 2015 na kati yao sita kwa mwaka 2018 pekee.Na mipango yake hii imefanya nchi za magharibi kudai kuwa zimekuwa zikichezewa na Moscow.Mwaka jana, mshauri wa zamani wa masuala ya usalama nchini Marekani, John Bolton alitangaza mpango mpya wa Marekani kwa ajili ya Afrika, ikiwemo kudhibiti China na Urusi.

Unaweza pia kusoma:

Mahusiano ya kijeshiUrusi imekuwa mshirika mzuri kwa Afrika na imekuwa ikipeleka silaha katika eneo hilo.Lakini Afrika hakuna soko kubwa la silaha- kama ilivyo kwa bara la Asia.Kati ya mwaka 2014-2018, bara la Afrika ukiacha Misri, lilinunua kiasi cha 17% ya silaha za Urusi zilizosafirishwa nje, kwa mujibu wa taasisi ya utafiti kuhusu masuala ya amani (SIPRI).

Russia's main arms market is Asia. . *Africa excluding Egypt.

Kwa kiasi kikubwa zilikwenda Algeria, nyingine chini ya 3% ya silaha zote zilizosafirishwa zilinunuliwa na mataifa mengine. Hivyo kwa ujumla, silaha zinazosafirishwa kwa nchi za kusini mwa jangwa la sahara ni kidogo.Hatahivyo, uhusiano wa kiulinzi umekuwa ukikua, na tangu mwaka 2014, kumekuwa na makubaliano ya ushirikiano wa kijeshi yaliyotiwa saini na nchi 19 za kiafrika.Mwaka 2017-18 , Urusi ilikuwa na mikataba ya kuuza silaha kwa Angola, Nigeria, Sudan, Mali, Burkina Faso na Guinea ya Ikweta.Silaha kama vile jeti za kivita, helkopta za kijeshi na za kusafiria, makombora ya kupambana na vifaru na injini kwa ajili ya ndege za kivita.

Russian contractors

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Wanajeshi wa kibinafsi Warusi wakilinda usalama katika Jamuhuri ya Afrika ya Kati

Matumizi ya wanajeshi wa kukodiMahusiano ya kijeshi na usalama ya Urusi hayahusu usafirishaji silaha pekee, ila wakati mwingine ni katika kutumia makundi binafsi ya wanajeshi wa kukodi.Kwa mfano, Urusi imekuwa ikisaidia Jamuhuri ya Afrika ya kazi (CAR), ikisaidia vikosi vya Umoja wa Mataifa vinavyounga mkono serikali dhidi ya makundi ya waasi.

Lakini vikosi binafsi za Urusi vimekuwa vikifanya kazi huko, vikitoa huduma ya kiusalama kwa serikali na kusaidia kulinda mali za kiuchumi.Shughuli za wanajeshi wa kukodi wa Urusi pia wamekuwa wakiripotiwa kuwepo katika nchi jirani ya Sudan na Libya pia katika nchi nyingine ikihusisha kampuni ya binafsi ya kijeshi Wagner inayodaiwa kuwa na ushirika na serikali ya Urusi.Maofisa wa Urusi ,wamekuwa wakikana ripoti hizo na imekuwa vigumu kuthibitisha uhusiano wao na Serikali ya Urusi, na kwa kiasi gani wamekuwa wakitoa usaidizi.

Mgodi wa Almasi

Chanzo cha picha, Petra Diamonds

Maelezo ya picha, Mgodi wa Almasi

Mali asiliUrusi ina motisha ya wazi ya kiuchumi kwa kutokana na uhusiano wake na bara la Afrika, kwani ina uhaba wa madini kama manganese, bauxite na chromium, ambazo zote ni muhimu kwa soko lake.Pia ina uzoefu katika sekta ya nishati, ambayo inaweza kutoa kwa nchi zenye utajiri wa rasilimali.