Kwanini tembo na almasi huenda wakaamua uchaguzi mkuu wa Botswana

Chanzo cha picha, Getty Images
Botswana inapiga kura katika uchaguzi mkuu hii leo na kama BBC ilivyogundua katika mjadala iliouandaa hivi karibuni huko Gaborone, almasi na tembo a u ndovu wana jukumu kubwa katika kubaini mshindi.
Chama tawala nchini Botswana Democratic Party (BDP) kimeshinda kila uchaguzi nchini Botswana tangu uhuru mnamo 1966, lakini mwaka huu kuna uwezekano hilo likabadilika.
Vyama vitatu ya upinzani vimeungana chini ya Umbrella for Democratic Change (UDC).
Wana manifesto walioinadi kwa makini inayoahidi nafasi laki moja za ajira. Katika nchi ambayo zaidi ya 20% ya idadi ya watu hawana ajira, na ambako kuna wasiwasi unaoongezeka kuhusu "wapatao kipato", hilo ni pendekezo la kuvutia.

Chanzo cha picha, Getty Images
Makamu rais wa muungano huo wa UDC Dumelang Saleshando ameiambia BBC katika mjadala huo kwamba "ni kuhusu uchumi uliowatenga raia wake".
"Unapoangaliwa sekta ya ujenzi, ni sekta iliokithiri Wachina. Unapotazama sekta ya biashara, Wahindi wamekithiri… hakuna sekta ya kiwanda hata moja nchini iliokithiri raia wa Botswana isipokuwa sekta ya biashara ndogo."

Taifa lililojengwa kwa Almasi
Mara nyingi Botswana hutajwa kuwa hadithi ya ufanisi Afrika uhuru wake ulipatikana pasi kushuhudiwa umwagikaji damu kama ulivyoshuhudiwa katika maatifa jirani zake, haijawahi kushuhudia vita vya kiraia na mara nyingi uchaguzi mkuu haukumbwi na ghasia.
Sehemu ya utajiri wa Botswana unatokana na almasi. Licha ya kwamba Urusi ina almasi nyingi zaidi kwa jumla, machimbo manne ya madini katika taifa hilo la kusini mwa Afrika lina idadi kubwa ya vito vya thamani duniani na Botswana ina hisa zake katika sekta hiyo ya 50-50 na De Beers, inayojieleza kuwa "kampuni inayoongoza duniani ya almasi".
Mkataba huo ulichangia $3.5bn katika mapato ya serikali mwaka jana, na biashara hiyo inawakilisha 40% ya uchumi wa nchi.
Fedhahizo zimejenga barabara, shule na hata hospitali lakini baada ya miaka zaidi ya 50 watu wengi wameanza kufikira pengine wanastahili kupata zaidi kutokana na bahati hiyo nzuri.
Mwaka huu, uvumi kuhusu ufisadi umechangia kuongezeka shaka kuhusu uhusiano huo.
Ushirikiano na De Beers unatarajiwa kuidhinishwa upya mwakani na limekuwa suala kubwa katika uchaguzi huu.
Uwezekano wa kupatikana makubaliano bora ndilo lilikuwa suali la kwanza katika mjadala wa BBC.
Waziri wa uchukuzi na mawasiliano Dorcas Makgato ametetea mtazamo wa serikali katika majadiliano hayo.
"Almasi kwetu ndio mustakabali wetu. Sisi ndio wazalishaji wakubwa wa almasi duniani kwahivyo itakuwa ni kama kujitia kitanzi kwetu sisi kutoiheshimu na kuipenda kama inavyostahili."
Lakini majadiliano yanasalia kuwa siri, wakati serikali haikuweza kuonyesha mkono wake, amesema.

Chanzo cha picha, Getty Images
Lakini bwana Saleshando analikataa hilo.
"95% ya watu hawajawahi kuiona almasi kwa macho yao. Ukweli ni kuwa ajira zilizo na mapato mazuri hutoka mataifa ya nje kupitia almasi za Botswana. Sisi tunasalia kuwa wachimbaji - tunayachimba mashimo tu."
Licha ya au kwasababu ya utajiri wake wa almasi, Botswana ina kiwango cha juu cha ukosefu wa malipo ya sawa duniani , kwa mujibu wa Benki ya Dunia, na raia wake wamenza kuuliza kwanini iwe hivyo.

Uchaguzi mkuu kwa mtazamo jumla:
- BDP - kilishinda uchaguzi wote tangu uhuru kikiongozwa na Mokgweetsi Masisi
- UDC - muungano uliundwa mnamo 2012, ukiongozwa na Duma Boko
- BPF - kiliundwa na rais wa zamani Ian Khama, kinaongozwa na Biggie Butale
- wapiga kura wanachagua wabunge 57, na wawakilishi 490 wa serikali za mitaa
- Rais anachaguliwa na bunge la taifa kwa muhula wa miaka mitano
- Kiongozi wa chama kilichojinyakulia viti vingi bungeni kawaida ndiye anayeibuka rais

Tatizo kuu - Tembo
Botswana huenda ndio nchi pekee duniani ambapo tembo au ndovu ndio suala kuu katika kila uchaguzi.
Kukiwa na idadi ndogo ya watu na kundi kubwa la wanyama hao barani Afrika, mizozo kat iya binaadamu na tembo ni wasiwasi wa kila siku.
Chini ya uongozi wa rais aliyekuwepo Ian Khama, Botswana ilikuwa ndiyo kiolezo cha uhifadhi.

Chanzo cha picha, Getty Images
Serikali yake ilisifiwa kwa kuidhinisha hatua zilizofanya kazi za kuinga uwindaji haramu, kwa kupiga marufuku uwindaji na kwa kuigeuza nchi hiyo kuwa hifadhi kubwa ya tembo barani Afrika.
Baadhi ya tembo huenda wamehamia nchini humo kutokana na hali nzuri. Lakini hilo limekuwa na gharama yake.
Ikiwa na kundi la takriban tembo 140,000, kitaifa wanyama hao wamekuwa wengi kushinda mazingira.
Watu wanakanyagwa hadi kufariki, vyakula vinaharibiwa mashamabni kwa siku na serikali inaendelea kukaidi wanapoambiwa la kufanya na mataifa ya nje yalio na nia njema.

Chanzo cha picha, Getty Images
Rais Mokgweetsi Masisi anaoenakana hana wasiwasi sana na inachofikiria jumuiya ya kimataifa kuliko anachokifikiria kiongozi aliyemtangulia.
Alipendekeza Uingereza inaweza kujaribu kuishi na tembo wa taifa hilo iwapo wanawapenda sana.
Akimkiuka kiongozi aliyemtamgulia ambaye bado ana ushawishi, kiongozo huyo mpya ameondosha marufuku dhidi ya uwindaji wa tembo. Hili limesababisha mzozo lakini ulionekana uamuzi wenye umaarufu wakati BBC ilipowauliza watu maoni yao mitaani Gaborone.
"Kuna mzozo kati ya tembo na binaadamu na wanawaua watu. Kwahivyo nafkiri kuwaua tembo ni fikra nzuri," asema Albert Lebala.
Keorapetse Mpolokang alikubaliana na hilo: "Wanaharibu mimea, hususan wakati wakulima."
Huku mwanamke mmoja akisisitiza msimamo wa rais: "Iwapo mataifa mengine yanataka kuwasilisha maoni kuhusu hatua yetu kuondosha marufuku ya uwindaji, wanapswa kuja nchini na kutazama madhara yalitokana na tembo kwa watu wetu."

Suala hilo kuhusu tembo ndilo mojawapo ya sababu za kuzuka mgawanyiko kati ya Rais Masisi na bwana Khama.
Yeye ni mtoto wa muasisi wa taifa hilo na kiongozi muhimu wa kitamaduni nchini kwahivyo kujitenga kwake kutoka chama ambacho aliahi kukiongoza na kukiidhinisha chama cha Botswana Patriotic Front (BPF) ni jambo kubwa.

Tshekedi Khama, kakake alizusha mshtuko alipojitoa kutoka baraza la mawaziri la Masisi na kujiunga na kakake kupambana na BDP.
Sio sehemu ya upinzani mkuu UDC lakini wameashiria huenda wakishirikiana nao na kuwasaidia kushinda.
Wadadisi wanasema kuna nafasi kubwa ya kuwepo mabadiliko serikali kuliko ilivyokuwa katika siku za nyuma.
Lakini BDP imefanikiwa pakubwa kupata ushindi katika uchaguzi na hakijawahi kushindwa.

Chanzo cha picha, Getty Images
Watu wanatazama mashariki nchini Zimbabwe na wanajua wamenusurika ghasia zilizoshuhudiwa katika matiafa mengi jirani.
Kunaonekana kuwepo mvutano katika akili za watu kati ya kukiamini BDP, na fursa ya kukwepo mkwamo na hasara iliodhihirika katika uhudumu wa muda mrefu madarakani.
" BDP ni chama kizuri lakini kimemakinika sana. hakuna kinachofanyika," anasema Manny, mfanyabiashara ndogo.
Licha ya kwamba alionya pia: "Tunahitaji mabadiliko - licha ya kwamba ninahofia kutakuwa na mathari iwapo tutaliidhinisha."
Muungano wa UDC unategemea kufanikiwa kuwashawishi watu kwamba ili kuweza kukuwa, demokrasi yao inahitaji kuwa na chama kipya madarakani. Lakini na inaeleweka, wakati hakuna chama kingine kilichowahi kuwepo madarakani, kuna wasi wasi kwamba mageuzi yoyote huenda yakaenda mrama.
















