Serikali ya Botswana kupinga uamuzi wa mahakama kuu uliohalalisha mapenzi ya jinsia moja

Chanzo cha picha, AFP
Serikali ya Botswana itaka rufaa dhidi ya uamuzi wa mahakama kuu nchini uliohalalisha mapenzi ya jinsia moja, mkuu wa sheria amesema.
Mwezi uliopita mahakama hiyo ilipinga sheria za wakatiwa ukoloni zinazotaja kifungo cha hadi miaka saba gerezani kwa yooyte anayejihusisha katika mapenzi ya jinsia moja, ikieleza kwamba sheria hiyo inakwenda kinyume na katiba.
Uamzui huo ulipongezwa na wengi na kutajwa kuwa ni kupiga hatua katika kuimarisha haki za wapenzi wa jinsia moja Afrika.
Lakini mkuu wa sheria nchini humo Abraham Keetshabe amesema majaji katika mahakama hiyo wamefanya makosa.
"Nimesoma kwa kina uamuzi huo wa kurasa 132 na maoni yangu ni kwamba mahakam kuu ilifanya makosa katika kufikia uamuzi huu," Keetshabe amesema katika taarifa iliyotolewa jana Ijumaa.
Ameongeza kwamba ataipeleka kesi hiyo katika mahakama ra rufaa, lakini hakutoa ufafanuzi zaidi kwa misingi ya rufaa hiyo.

Chanzo cha picha, EPA
Uamuzi wa mahakama kuu mwezi uliopita ulifikiwa kwa pamoja na majaji watatu.
" Utu wa binadamu unapata madhara wakati makundi ya walio wachache yanabaki nyuma," Alisema Jaji Michael Leburu alipokuwa anasoma hukumu . " Jinsia ya mtu si mtindo wa fasheni. Ni utambulisho wa maana wa utu."
Kesi iliwasilishwa na mwanafunzi aliyelalamika kwamba jamii imebadilika na mapenzi ya jinsia moja yanakubalika katika maenoe mengi.
Hukumu hiyo ilipokelewa kwa shangwe kubwa na wanaharakati wanaoendesha kampeni za wapenzi wa jinsia moja kote barani Afrika, ambako mahusiano ya mapenzi hayo ni kinyume cha sheria za nchi nyingi.
Botswana inaonekana kama moja ya nchi za Afrika thabiti zilizokomaa kidemokrasia, lakini mahusiano ya kimapenzi ya watu w ajinsia moja yalikuwa ni kinyume cha sheria chini ya sheria ya nchi hiyo ya mwaka 1965.
Mkala hii imebeba madhui yaliyotoka kwenye mitandao ya kijamii. Tunaomba ruhusa yako kabla kitu chochote hakija pakiwa, sababu wanaweza wakawa wanatumia Cookies na tekinolojia nyingine. Unaweza ukasoma sera sera ya kutumia cookies katika mitandao ya kijamii kabla ya kukubali. Kutazama maudhui haya chagua accept and continue
Mwisho wa X ujumbe
Katika baadhi ya nchi za Afrika watu wanaoshiriki mapenzi ya jinsia moja hukabiliwa na kifungo cha maisha jela au hukumu ya kifo.
Angola, Msumbiji na Ushelisheli zote zimefutilia mbali sheria zinazopinga mapenzi ya jinsia moja katika miaka ya hivi karibuni.
Mnamo mwezi Mei, mahakama kuu nchini Kenya' iliamua kutobatilisha sheria inayopiga marufuku mapenzi ya jinsia moja.
Majaji wa Kenya walipinga hukumu iliyotolewa na majaji wa India, iliyo halalisha kisheria ngono ya watu wa jinsia moja walio na umri wa utu uzima, pamoja na msururu wa hukumu nyingine zilizotolewa kote katika nchi wanachama wa Jumuiya ya madola na kwingineko, na wakasema Kenya inapaswa kutunga sheria zake zitakazoendana na utamaduni wake.
Kenya ni nchi ya kwanza ya Afrika chini ya sheria kusikiliza mahakamani ombi la kutaka kufutiliwa mbali kifungu cha sheria inayopinga mapenzi ya jinsia moja.

Ngono baina ya watu wa jinsia moja ni kosa linaloadhibiwa kwa kifo katika maeneo ya Kaskazini mwa Nigeria , Sudan, Somalia na Mauritania.
Sheria za Tanzania zinaweza kumsababishia anayeshiriki mapenzi ya jinsia moja kufungwa kifungo cha maisha jela.
Angola,Msumbiji na Ushelisheli kwa pamoja ziliondoa sheria zinazokataza mapenzi ya jinsia moja katika miaka ya hivi karibuni.














