Kwa Picha: Mvuto wa Botswana

Huu ni mkusanyiko wa picha za maeneo ya kuvutia pamoja na wanyama pori nchini Botswana. Picha hizi zilipigwa na watu mbalimbali na zinaashiria mvuto ambao huwafanya watalii kutembelea taifa hilo la kusini mwa Afrika kwa wingi.

Chobe

Chanzo cha picha, Anna Sobotka

Maelezo ya picha, Anna Sobotka, ambaye ni mara yake ya kwanza kufika Afrika, anasema: "Sikutarajia kupendezwa na umaridadi na mandhari ya taifa hili kama nilivyofanya." Alipiga picha hii ya ndovu wakioga Mbuga ya Taifa ya Wanyama ya Chobe
Twiga

Chanzo cha picha, Anne May

Maelezo ya picha, Hii ni picha nyingine kutoka Mbuga ya Taifa ya Wanyama ya Chobe, wakati huu kutoka kwa Anne May ambayo inawanesha twiga wakinywa maji mto Chobe
Roller

Chanzo cha picha, Philip Willmott

Maelezo ya picha, Ndege hawa aina ya Roller wanaonyesha rangi za kupendeza ambao mtalii hukumbana nazo anapotembea porini Botswana. "Ndege hawa hupendeza wakiwa kwenye miti, lakini zaidi wakippaa na kupita mbele yako," anaandika Philip Willmott
Mbuyu

Chanzo cha picha, Patricia Mueller

Maelezo ya picha, Kuna mibuyu ya kuvutia pia. Mibuyu inayokua Botswana baadhi ilimea karne nyingi zilizopita.
2015 Kalahari

Chanzo cha picha, Tumisang Entaile

Maelezo ya picha, Mshiriki wa mashindano ya mbio za magari jangwani katika Jangwa la Kalahari mwaka 2015, mashindano yanayofanyika kila mwaka.
Jua likitua Okavango Delta.

Chanzo cha picha, Jana Pavlic

Maelezo ya picha, Jua likitua Okavango Delta.
Makgadikgadi

Chanzo cha picha, Diane Kim

Maelezo ya picha, Mnyama ajulikanaye kama meercat aonekana jua likitua eneo la Makgadikgadi Pans, moja ya maeneo tambarare yenye chumvi nyingi zaidi.
Okavango Delta

Chanzo cha picha, Tristan Fouere

Maelezo ya picha, Hapa ni maeneo ya kaskazini ya Okavango Delta eneo lifahamikalo kama NG23 karibu na Seronga.
Chobe

Chanzo cha picha, Kim Pickett

Maelezo ya picha, Wanyama wanapatikana kwa wingi. Chui huyu alipigwa picha na Kim Pickett Mbuga ya Taifa ya Wanyama ya Chobe. Botswana ina wanyama wakubwa wengi zaidi wa jamii ya paka kusini mwa Afrika.