Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Wananchi wenye hasira kali wamburuza Meya nyuma ya gari nchini Mexico kwa kutotimiza ahadi za uchaguzi
Watu 11 wamekamatwa na kutiwa mbaroni kwa kosa la kumkamata meya wa kijiji chao kisha kumfunga katika gari na kumburuza mitaa mbalimbali.
Polisi waliingia kati tukio hilo kwa na kumuondoa meya Jorge Luis Escandón Hernández ambae alipatwa na majeraha kidogo.
Hili ni shambulio la pili kutoka kwa wakulima hao ambao wanadai hawajatimiziwa ahadi alizotoa meya Hernández, ikiwemo ujenzi wa barabara.
Polisi zaidi wamepelekwa katika kijiji cha jimbo la Chiapas.
Meya pamoja na viongozi wa chini wa serikali mara nyingi hushambuliwa nchini mexico na makundi ya kihalifu wasipofanya matakwa wanayoyataka, lakini kupigwa kwa ahadi za uchaguzi ni jambo geni.
Meya Hernández amesema atafungua kesi ya kutekwa na kutaka kuuwawa.
Video zilizochukuliwa na wapita njia nje ya ofisi ya meya huyo zimeonesha kundi la wanaume wakimvuta nje ya jengo na kumfunga nyuma ya gari.
Picha zilizochukulia na CCTV kamera zinaonesha akiburuzwa huku akiwa amefungwa kamba katika mikono yake katika mitaa ya Santa Rita.
Iliwachukua kundi la polisi kadhaa kuweza kumuokoa katika kadhia hiyo, watu kadhaa walijeruhiwa baina ya polisi na watu hao.
Katika tukio la miezi kadhaa iliyopita watu wasiojulikana walivamia na kuharibu ofisi yake, lakini yeye hakuwepo.
Wakati wa uchaguzi wa kiti cha meya, Hernández alihusishwa pia na ghasia dhidi ya mpinzani wake lakini alichiwa kutoka na kukosekana kwa ushahidi.