Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Imamu aliyefariki akipambana na ubaguzi wa rangi Afrika Kusini
Jamaa na marafiki wa imamu aliyefariki miaka 50 iliyopita akipinga ubaguzi wa rangi nchni Afrika kusini bado wanasononeka kutokana na kifo chake anaandika mwandishi wa BBC Penny Dale.
Matukio mawili muhimu huko Cape Town nchini Afrika Kusini mnamo Septemba 29 mwaka 1969.
La kwanza lilikuwa ni msafara wa mazishi - takriban watu 40,000 walilibeba jeneza la Imam Abdullah Haron kwa kiasi ya kilomita 10 mpaka sehemu ya kuzikwa katika makaburi ya waislamu Mowbray.
Na usiku wake tetemeko la ardhi kubwa na ambalo ni nadra kutokea lilitikisa.
Kwa wengi waliohudhuria mazishi, matukio hayo mawili yalihusiana - wanasema kifo cha imamu huyo wa Afrika kusini mwenye miaka 45 kilikuwa ni cha uchungu na kilichowashutusha wengi.
Imam Haron alifariki gerezani mnamo Septemba 27, baada ya kuwekwa kizuizini peke yake kwa siku 123 na kuhojiwa kila siku kuhusu kuhusika kwake katika vita dhidi ya utawala wa ubaguzi wa rangi uliomalizika mnamo 1994 kufuatia kuchaguliwa kwa rais Nelson Mandela kama kiongozi wa kwanza mweusi nchini humo.
Imam Haron alikuwa kiongozi wa kwanza wa dini kufariki gerezani chini ya utawala huo wa ubaguzi wa rangi. Kifo chake kiliashiria kuwa hata viongozi wa dini hawakuwa salama dhidi ya utawala wa ukandamizaji wa mtu mweupe.
Msanii aliyepewa jina la Imam
Kifo chake kilisababisha hasira duniani na akawa muislamu wa kwanza kukumbukwa katika kanisa maarufu la St Paul's Cathedral mjini London.
Maafisa wa usalama wanasema alifariki baada ya kuanguka kutoka kwenye ngazi.
Walisema hawakuhusika na mbavu mbili zilizovunjika mwilini mwa Imamu huyo pamoja na majeraha mingine 27 mwilini mwake, licha ya kutambulika kwa mtindo wao wa kuwapiga na kuwatesa wafungwa.
familia ya imamu huyo inasema haiukubali 'uongo huo' na wanataka uchunguzi mpya katika kukumbuka miaka 50 tangu kifo chake.
Msanii Haroon Gunn-Salie anaiunga mkono kampeni hii - amepewa jina kwa heshima ya imamu huyo na ameunda kazi kadhaa za sanaa katika kumkumbuka maisha na kifo chake.
Kazi yake ya hivi karibuni Gunn-Salie, Crying for Justice, ni makaburi 118 matupu anayosema ni ya kila mtu aliyeuawa akiwa kizuizini wakati wa utawala huo wa ubaguzi wa rangi akiwemo Haron.
Walizuiwa pasi kushtakiwa - na polisi wanasema walianguka kutoka kwenye ngazi, walianguka wakiwa bafuni au walijirusha kutoka kwenye madirisha.
'Kilio kwa mahakama'
Hakuna aliyechukuliwa hatua kwa mauaji hayo na ni kidonda kilicho wazi kwa familia zao.
Yatakapomalizika makaburi hayo yalioundwa na Gunn-Salie yataunda neno: 'Justice?' yaani Haki.
"Kazi hiyo ya sanaa ni kilio kwa mahakama," anasema Gunn-Salie.
"Ni taarifa ya wazi inayouliza, kufukua yaliopita, kutoa ushahidi na kuzituliza familia za wahanga."
Kwa masikitiko, mjane wake mwenye umri wa miaka 93 Galiema Haron alifariki Jumapili, takriban miaka 50 kamili tangu mazishi ya mumewe pasi kupata utulivu wa roho.
Imam Haron alikuwa mojawapo ya maimamu vijana Afrika kusini - alikuwa na miaka 32 tu alipoteuliwa kuongoza waumini katika msikiti wa Stegmann Road mjini Cape Town.
Alianzisha mafunzo kwa watu wazima, makundi ya majadiliano ambapo mada zilichaguliwa na vijana na kuwahimiza wanawake kushiriki.
Aliwakaribisha pia watu wasiotoka jamii ya waislamu wakiwemo wa vyama vya wafanyakazi na wanasiasa wa liberali kuja kuzungumza kuhusu kinachoendelea nchini.
Alipinga sheria kandamizi
Alitenda alichosema, alizitembela jamii za watu weusi katika mitaa kama Langa, Gugulethu na Nyanga, ambako alifahamika kwa umaaufu kama mfundisi, au padri.
Kando na kuwa imamu, Haron alifanya kazi kama muuzaji katika duka la pipi Wilson Rowntree. kazi yake ilimruhusu kuingia kutoka sehemu moja hadi nyingine bila ya mataizo hata baada ya utawala kupinga watu kuzunguka na kuzitenga jamii kwa misingiya rangi na kuidhinisha sheria zilizoshinikiza hilo.
Mnamo 1966 na miwshoni mwa 1968, imam alikwenda Hijja Saudi Arabia. Alisafiri kwa siri pia kwenda Misri kukutana na wanasiasa wanaoishi uhamishoni na baraza la kiislamu duniani.
Alikwenda London pia ambapo binti yake mkubwa Shamela alikuwa anasoma. Kufika huko alikutana na Canon John Collins wa kanisa la St Paul's Cathedral, aliyekuwa anachangisha fedha za familia zisizojiweza za wanaharakati wa kisiasa waliouawa wanaozuiwa au waliolazimika kuishi uhamishoni.
Wawili hao walifanya urafiki wa dhati na Abdullah Haron alikubali kubeba kimagendo na kugawanya pesa hizo aliporudi Afrika kusini.
Lakini wakati aliporudi Afrika kusini mnamo 1969, imam huyo alijuwa kwamba yuko katika hatari. Mnamo Mei 28 mwaka 1969 alichukuliwa na polisi ya utawala wa ubaguzi wa rangi na miezi minne baadaye alifariki.
Taarifa ya ziada na Audrey Brown
Kufahamu zaidi kuhusu Imam na msanii huyo sikiliza makala haya kutoka BBC.