Makubaliano ya kinyuklia : Mataifa ya EU yameionya Iran dhidi ya ukiukaji wa makubaliano hayo

Chanzo cha picha, EPA
Uingereza ,Ufaransa na Ujerumani zimeionya Iran dhidi ya kukiuka mkataba wa kinyuklia wa 2015 , BBC Imefichua.
Mjini New York siku ya Alhamisi, mataifa hayo matatu ya EU yalioweka saini mkataba huo yamesema kwamba watazua malalamishi iwapo mkataba huo utakiukwa zaidi.
Iran ilianza kukiuka mkataba huo baada ya Marekani kujiondoa na kuiwekea vikwazo Iran.
Shirika la Umoja wa mataifa la uangalizi wa Silaha za kinyuklia limesema kwamba Iran inajiwekea madini ya kutengezea nyuklia kupitia teknolojia ya kuchoma.
Tishio hilo lilitolewa katika mkutano na mawaziri wa Iran kandokando katika mkutano mkuu wa Umoja wa mataifa kulingana na mwandishi wa BBC James Landale.
Katika mpango huo wa kuzua ugomvi , huenda makubaliano yote ya kinyuklia yakaanguka na Umoja wa mataifa huenda ikaiwekea vikwazo Iran , ambavyo vitaidhinishwa na wanachama wote kulingana na mwandishi huyo.
Hatua hiyo huenda ikaathiri vibaya uchumi wa Iran , anaongezea.
Je mkataba wa kinyuklia wa Iran ni nini?
Mkataba huyo uliafikiwa 2015 na mataifa matatu ya EU pamoja na marekani, Urusi na China.
Ijapokuwa makubaliano hayo yaliiruhusu kujipatia idadi ndogo ya madini ya Uranium, kwa utafiti, yalipiga marufuku kujiwekea madini hayo kutengeza kawi na pia silaha za kinyuklia.

Chanzo cha picha, Reuters
Iran imekana madai kwamba inataka kutengeza silaha za kinyuklia na kusema kwamba mpango wake wa kinyuklia ni wa amani.
Makubaliano hayo yalionekana kama makubaliano ya kihistoria lakini mwaka 2018, rais Donald Trump wa Marekani alijiondo akisema kwamba mkataba huo ulikuwa na dosari na kuiwekea vikwazo Iran.
Mnamo mwezi Mei , Marekani iliimarisha vikwazo vyake dhidi ya Iran na kusema kwamba itajaribu kulazimisha mataifa yote kutonunua mafuta ya iran na kuiwekea presha Iran kuingia katika mazungumzo mapya ya kinyukl
Baada ya vikwazo dhidi yake kuimarishwa , Iran ilianza kukiuka baadhi ya makubaliano hayo ili kuzishinikiza nchi wanachama waliosalia kuisaidia.
Lakini shirika hilo la kinyuklia lilithibitisha kwamba mnamo tarehe mosi Julai kwamba Iran ilikiuka makubaliano hayo kwa kuongeza kiwango cha kilo 300 za kiwango cha madini ya Uranium ilichotakiwa kujipatia.
Siku sita baadaye , Iran ilianza kutengeneza madini hayo ya Uranium kwa kiwango cha juu zaidi ambacho ilikubaliwa kujiwekea katika mkataba huo licha ya kwamba hakijafikia kiwango kinachohitajika kutengeneza silaha za kinyukliaia.














