Jinsi dawa yenye bangi inavyoweza kutibu kifafa

Hand holding cannabis

Muungano wa Ulaya umeidhinisha kwa mara ya kwanza utumizi wa bidhaa za dawa ya bangi kwa lengo la kuwatibu wagonjwa walio na ugonjwa wa kifafa utotoni mwao.

Madaktari sasa wanaweza kumpatia mgonjwa tiba hiyo aina ya Cannabidiol inayotoka katika mmea wa bangi iwapo wanahisi kwamba wanaweza kumtibu mwathiriwa.

Imehalalishwa kutumika Uingereza pamoja na mataifa mengine ya Ulaya. Hata hivyo kuna wazazi wanaotaka dawa isio na mmea huo.

Unaweza pia kusoma:

Mwezi uliopita taasisi ya kitaifa ya afya nchini Uingereza ilifanya uamuzi wa awali wa kutopendekeza matumizi ya dawa hiyo kutokana na ukosefu wa ushahidi kuhusu madhara yake ya siku za baadaye.

Hatahivyo mwongozo rasmi unatarajiwa kutolewa baadaye mwaka huu .

Lakini Epidyolex ni nini?

Dawa hiyo haina madhara yoyote ya kiakili yanayotokana na bangi kwa jina tetrahydrocannabinol (THC).

Baadhi ya wazazi ambao wamezuru nchini Uholanzi ili kununua dawa hyo ya bangi , wanahisi kwamba tiba hiyo haitawasaidia watoto wengi kwa kuwa haina tetrahydrocannabinol THC ambayo wanadai kwamba imewasaidia watoto.

Epidyolex imeidhinishwa kama tiba mbadala kwa watoto wadogo walio na hadi umri wa miaka miwili ambao wana matatizo kifafa yanayoweza kusababisha mtu kupapatika kwa siku.

Dawa hiyo iliotengezwa na kampuni ya dawa ya GW Pharmaceuticals itatumika kwa mchanganyiko wa dawa nyengine ya kifafa kwa jina clobazm.

Je bidhaa nyengine za tiba ya bangi?

Kuna bidhaa tofauti za tiba ya bangi. Matumizi ya bidhaa ilio na THC yalihalalishwa nchini Uingereza mwezi Novemba 2018.

Tiba hizo zinaweza kutolewa na madaktari bingwa katika matukio kadhaa ambapo dawa nyengine zimefeli.

Hatahivyo kuna tiba nyengine zilizotengezwa kutokana na mmea wa bangi ambazo zimehalalishwa Uingereza.

Nabilone ni dawa , inayotumika kama capsule ambayo imetengezwa ili kuwa na utendakazi unaofanana na THC.

Madaktari huwapatia wagonjwa wanaopatiwa tiba ya kuuwa seli za saratani mwilini ili kusaidia kichefuchefu.

Sativex pia ni dawa inayotokana na bangi ilio na THC na hutumika nchini Uingereza kwa watu walio na ugonjwa wa mzio.

Je wataalam wanasemaje?

Ley Sander, mkurugenzi wa matibabu katika taasisi ya kifafa pamoja na magonjwa ya neva katika chuo kikuu cha London, alisema: Dawa hii mpya italeta matumaini kwa baadhi ya familia na uungwaji mkono wa Muungano wa Ulaya ni hatua kubwa.

Tiba ya bangi hatahivyo bado ni swala tata na kuwa ina vikwazo vingi mbeleleni.

Hatahivyo alisema kwamba ni muhimu kwa wote wale walio katika sekta ya dawa kuendelea kushirikiana na bodi ya ushauri wa tiba ili kuhakikisha kwamba dawa zina tiba na kwamba madhara yake katika siku zijazo yapo wazi.