Mashambulizi ya visima vya mafuta vya Saudia: Je ni nani anayetumia ndege zisizo na rubani zinazobeba silaha Mashariki ya kati?

Ndege isio na rubani inayomilikiwa na Marekani katika Ghuba la Persia

Chanzo cha picha, Getty Images

Mashambulizi dhidi ya hifadhi za mafuta za taifa la Saudia yamezua uvumi kwamba ndege zisizo na rubani zilihusishwa.

Mamlaka za Marekani na Saudia zinasema kwamba hivyo ndivyo ilivyokuwa.

Shambulio la utumizi wa ndege zisio na rubani limeongezeka katika miaka ya hivi karibuni na hususana katika eneo la mashariki ya kati.

Hivyobasi ni nani anayemiliki na ni nani aliyetumia katika shambulizi?

Silaha mpya.

Matumizi ya kwanza ya kijeshi ya kutumia ndege isio na rubani ilio na silaha yalikuwa Oktoba 2001 usiku wa kwanza wa vita vya Afghanistan dhidi ya msafara wa Taliban.

China imekua ikiuza ndege hizo kwa wingi kote duniani

Chanzo cha picha, AFP

Maelezo ya picha, China imekua ikiuza ndege hizo kwa wingi kote duniani

Ndege zisizo na rubani zinazomiliki silaha zilikuwa zikitumika na mataifa yalioendelea kama vile Israel na Marekani.

Hatahaivyo China nayo iliingilia na kuanza kuuza silaha zake duniani .

China imepiga jeki usambazaji wa ndege za kijeshi zisizokuwa na rubani katika eneo la mashariki ya kati ikiuza silaha hizo kwa zaidi ya mataifa sita.

Soko la ndege hizo zinazotumiwa na raia pia liligundua teknolojia hiyo na kuibadilisha kuwa ndege zinazotumia silaha.

Huku Teknolojia hiyo ikiwa sio ngumu, ndege kama hizi zilizo na uwezo mkubwa zinaweza kutengezwa na taifa lolote - Iran ikiwa mfano.

Na Iran imechukua jukumu muhimu la kuimarisha teknolojia ya ndege hizo na kuzisambaza kwa washirika wake kama vile waasi wa Houthi waliopo Yemen.

Nani anayemiliki nini?

Eneo la mashariki ya kati ndilo lenye vita dhidi ya ugaidi. Limevutia mataifa yenye teknolojia ya hali ya juu kama vile Marekani Uingereza na Urusi.

Kuna uadui mkubwa .

Uadui mkubwa unaojulikana duniani ni ule kati ya Israel na mataifa ya Kiarabu upande mmoja na Iran, washirika wake kama Hezbollah na waasi wa Houthi katika upande mwengine.

Marekani

Marekani imetumia ndege zisizo na rubani zilizo na silaha katika eneo la mashariki ya kati , katika kampeni yake dhidi ya al- Qaeda na Islamic State.

Silaha kama vile ndege zisizo na rubiani za kuvizia zimetumika dhidi ya maeneo ya Syria , Iraq, Libya na Yemen.

Ndege isio na rubani kwa jina MQ-9 ni kubwa , nzito na yenye uwezo zaidi ya ile ya kuvizia ikiwa na uwezo wa kubeba silaha kubwa zinazoweza kusafiri mbali.

Kama mshirika mkuu wa Marekani kijeshi , Uingereza ilinunua ndege kadhaa zisizo na rubani kutoka Marekani na imezitumia zaidi katika maeneo ya taifa la Iraq na Syria.

Israel

Ikijulikana kwa muda mrefu kama taifa mwanzilishi wa teknolojia ya UAV , Israel ni miongoni mwa wauzaji wa ndege zizsizo na rubani zinazotumika na raia ikiwa imeuza zaidi ya asilimia 60 ya ndege hizo kote duniani kulingana na utafiti wa 2018.

Mbali na wateja wengine taifa hilo limeuzia Urusi na limefanikiwa kutungua ndege moja ilipokuwa ikitoka Syria kuingia Israel.

Israel inatumia ndege tofauti kukusanya habari na kutekeleza mashambulizi.

Ndege zake zilizo na silaha ni pamoja na Heron TP, The Hermes 450 na The Hermes 900.

Lakini Israel imekuwa na wasiwasi kuuza ndege hizo zinazoweza kubeba silaha.

Iran imejitengezea ndege yake kwa kutumia teknolojia yake

Chanzo cha picha, AFP

Maelezo ya picha, Iran imejitengezea ndege yake kwa kutumia teknolojia yake

Iran

Licha ya kuwekea marufuku ya kununua silaha , Iran imejenga uwezo wa kujitengezea ndege zisizo na rubani zinazoweza kubeba silaha.

Ndege kwa jina Shahed 129 ilizinduliwa 2012 na imetumika kuwakabili IS na maeneo kadhaa nchini Syria na Iraq.

The Mohajer 6 imekuwa ikitengezwa tangu 2018.

Lakini umuhimu mwengine wa utengezaji wa ndige hizo nchini Iran ni uwezo wake wa kutaka kueneza teknolojia yake kwa washirika wake katika eneo hilo

Marekani imeishutumu Iran kwa kuwasambazia waasiwa Houthi ndege hizo

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Marekani imeishutumu Iran kwa kuwasambazia waasiwa Houthi ndege hizo

Matumizi ya ndege hizo miongoni mwa makundi ya kivita

Waasi wa Houthi ni miongoni mwa watumizi wa ndege za UAV miongoni mwa makundi yasiokuwa na serikali.

Wanaendesha idadi kubwa ya mifumo ambayo kulingana na UN na wataalam inategemea sana teknolojia kutoka Iran.

Waasi wa Houthi wametumia Qasef-1 , ambayo jopo la Wataalam wa UN limesema kuwa inafanana na mifumo ya Iran.

Hizi ni ndege zisizo na rubani ambazo hulipuka zinapowasili katika eneo zilikotumwa.

Wapiganaji wa Lebanon wa dhehebu la Kishia Hezbollah wamekuwa wakitumia idadi ndogo ya kile kinachoonekana kuwa ndege za Iran zisizo na rubani.

Athari zake nini?

Ni wazi kwamba teknolojia ya ndege zisizo na rubani zinazobeba silaha imesambaa kote .

Licha ya Marekani kukataa kuuza ndege hizo kwa wasihirika wake hakujazuia ndege hizo kusamabaa kwa kuwa China imekuwa ikiziuza .

Utumizi wa UAV kushambulia maeneo umesaidia kufungua mbinu nyengine ya mashambulizi.

Ndege zenye rubani zimetumika kushambulia maeneo bila ya madhara makubwa kuonekana.

Ndege hizo zinaonekana kutengezwa kukabiliana na vita dhidi ya ugaidi.