Tetesi za soka Ulaya Jumapili 15.09.2019: Messi, Kroos, Pogba, De Gea, Eriksen, Mane

Mchezaji nyota wa zamani wa England, David Beckham ameongezea nguvu mipango yake ya kutaka kumsajili mshambuliaji wa Barcelona Lionel Messi.

Beckham anamiliki klabu ya soka nchini Marekani ijulikanayo kama Inter Miami, ambayo imeshatuma wawakilishi wake kuzungumza na baba wa Messi. (Sun on Sunday)

Inter Miami pia wanataka kumsajili winga wa Real Madrid na timu ya taifa ya Wales, Gareth Bale, 30.(Maxifoot - in French)

Manchester United wanapanga kumsajili kiungo Mjerumani wa klabu ya Real Madrid Toni Kroos, 29, mwezi Januari katika mkataba wa kubadilishana wachezaji.

United wanaweza wakamtoa Paul Pogba na kukubali kiasi cha pesa kama sehemu ya makubaliano hayo. (Bild - in German)

Kipa wa Uhispania David de Gea, 28, ametia saini mkataba mpya wa miaka minne na Man United wa thamani ya pauni 250,000 kwa wiki, na malipo yanaweza kupanda mpaka pauni 350,000 kwa wiki kulingana na kiwango cha mchezo. (Sunday Mirror)

Mshambuliaji wa England Callum Hudson-Odoi, 18, anatarajiwa kuingia makubaliano mapya na klabu yake ya Chelsea mara baada ya kupona majeraha yake. (Sun on Sunday)

Liverpool wameanza mazungumzo ya kuongeza mkataba na mshambuliaji wake raia wa Senegali Sadio Mane. (SoccerLink, via Sport Witness)

Kiungo wa Denmark Christian Eriksen, 27, anasubiria uwezekano wa kuihama klabu ya Tottenham na kuelekea Real Madrid, mwezi Januari. (Marca - in Spanish)

AC Milan na Inter Milan wote wana mipango ya kumsajili kiungo Mserbia Nemanja Matic, 31, kutoka Manchester United mwezi Januari. (Corriere Dello Sport - in Italian)

Manchester United wametuma wachunguzi wake kumuangalia mshambuliaji wa Fenerbahce ya Uturuki Vedat Muriqi, 25, wakati akiichezea timu yake ya taifa ya Kosovo dhidi ya England wiki iliyopita. (Sunday Express)

Kocha wa Newcastle Steve Bruce amepewa ridhaa na uongozi wa klabu ya kusajili wachezaji wapya mwezi January, hususani mawinga. (Chronicle)

Mshambuliaji wa Juventus na Croatia Mario Mandzukic, 33, ambaye alikuwa akihusishwa na kutaka kuhamia Man United hivi karibuni, anakaribia kukamilisha usajili wa kuelekea Marekani katika klabu ya LAFC. (Calciomercato)

Beki raia wa England Tyrone Mings, 26,amesema alishangazwa sana pale Aston Villa walipoamua kumsajili kwa pauni milioni 20 kutoka klabu ya Bournemouth. (Express and Star)

TETESI ZA JUMAMOSI

Barcelona huenda ikamsajili mshambuliaji wa PSG na Ufaransa mwenye umri wa miaka 20 Kylian Mbappe baada ya kukosa kumsajili mchezaji mwenza raia wa Brazil Neymar, 27. (Mundo Deportivo - in Spanish)

West Ham iliipiku Bayern Munich ili kuweza kumsaini mshambuliaji wa Ufaransa mwenye umri wa miaka 25 Sebastien Haller kutoka Eintracht Frankfurt msimu huu katika usajili utakaovunja rekodi wa £45m. (Mail)

Watford ilimfuta kazi mkufunzi wake kwa kuwa hakuweza kuimarisha safu ya ulinzi na alikuwa hataki kuwachezesha baadhi ya wachezaji wapya waliosajiliwa.. (Sky Sports)

Nafasi ya kipa wa Manchester United David de Gea inaweza kupewa kipa mlinda lango mwengine ili kujaza pengo hilo huku mazungumzo kuhsu kandarasi ya mchezaji huyo yakiendelea. (Marca - in Spanish)

De Gea, 28, ameripotiwa kutia saini kandarasi ya miaka mitano katika uwanja wa Old Trafford. (Record)

Beki wa Ubelgiji Jan Vertonghen, 32, anataka kutia kandarasi mpya na klabu ya Tottenham huku mkataba wake ukitarajiwa kukamilika mwisho wa msimu huu. (Football Insider)

Spurs pia wamempatia kiungo wa kati Christian Eriksen kandarasi mpya ya £230,000 kwa wiki ili kujaribu kumzuia huku klabu za Man United na ile ya Real Madrid zikimnyatia.. (Mail)

Southampton ina hamu ya kumsaini kinda wa Ubelgiji mwenye umri wa miaka 18 Yari Verschaeren kutoka Anderlecht. (Calciomercato - in Italian)

Beki wa Cardiff na Ivory Coast Sol Bamba, 34, ni miongonii mwa wachezaji wanaotarajiwa kumrithi Neil Warnock atakapojiuzulu kama mkufunzi mwaka ujao. (South Wales Evening Post)

Manchester City na Manchester United zinamnyatia kiungo wakati wa Benfica kinda Florentino Luis, 20. (Mirror)

Mkufunzi wa Newcastle Steve Bruce anasema kwamba alijaribu kumsaini beki wa Liverpool na Uholanzi Virgil van Dijk, 28, akiwa mkufunzi wa Hull. (Guardian)

Jose Mourinho anasema kuwa mkufunzi wa Chelsea Frank Lampard ana kila uwezo wa kuwa mmojawapo wa wakufunzi bora katika klabu hiyo ya Stamford Bridge. (Sky Sports)

Mshambuliaji wa Tottenham na Ireland wa timu ya wachezaji wasiozidi umri wa miaka 21 Troy Parrott, 17, analengwa na Juventus Juventus, Real Madrid Bayern Munich. (Calciomercato - in Italian)