Ni kwanini Iran imeamua kuwaachilia huru wahudumu 7 meli ya mafuta ya Uingereza?

Chanzo cha picha, Reuters
Iran inasema sitawaachilia huru kwa sababu za kibinadamu wahudumu 23 wa meli ya mafuta inayomilikiwa na Uswiss , yenye bendera ya Uingereza siliyotekwa katika eneo la Strait of Hormuz mwezi Julai.
Mabaharia - watano wa Kihindi , MLatvian mmoja na Mrusi mmoja tayari wameondoka katika meli hiyo inayofahamika kama Stena Impero. amesema msemaji wa wizara ya mambo ya nje kwenye televisheni ya taifa.
Iran ilishutumu chombo hicho cha majini kwa "ukiukaji wa sheria za kimataifa za mipaka ya majini".
Kutekwa kwa meli hiyo kulitokea wiki mbili baada ya meli ya mafuta ya Iran kukamatwa ilipokuwa njiani kuelekea Gibraltar kwa usaidizi wa kikosi cha wanamaji wa Uingereza -The Royal Marines.
Ndege hiyo, ambayo kwa sasa inaitwa Adrian Darya 1, ilishukiwa kukiuka vikwazo vya Muungano wa Ulaya dhidi ya Syria , lakini iliachiliwa na mamlaka za Gibraltar tarehe 15 Agosti.
Meli ya Stena Impero ilikuwa ikipita katika eneo la maji la kimataifa lililopo Strait of Hormuz, ambayo ni njia nyembamba ya maji inayounganisha Ghuba na bahari ya India mnamo tarehe 19 Julai iliposhikiliwa na kikosi cha Iran (Islamic Revolution Guard Corps).
Picha za video zilionyesha Vikosi vikiivamia kutoka kwenye helikopta.
Uingereza inasema kuwa kikosi chake cha majini Royal Navykilitumwa katika eneo la Ghuba kujaribu kutoa msaada kwa meli na kikawaonya Wairan kwa njia ya radio kwamba hatua zao zilikuwa kinyume cha sheria , lakini hakikuweza kufikia eneo la tukio mapema.
Stena Impero ilipelekwa kweneye bandari ya Iran ya Bandar Abbas, ambapo iliiendela kutia nanga.
Waongozani wa Sweden -kampuni ya Stena Bulk, alisema mwezi uliopita kuwa imeweza kuzingatia mawasiliano machache sana na wahudumu wa meli na wameendelea kuwa na afya nzuri "ikilinganishwa na hali waliyonayo ". Lakini imeelezea hofu yake juu ya hali zao.
Siku ya Jumatano, msemaji wa wizara ya mambo ya nje wa Iran Abbas Mousavi aliimbia televisheni ya taifa hilo kuwa nahodha wa meli hiyo amewachagua watu saba miongoni mwa wafanyakazi wa meli hiyo watakaoachuliwa.
"Wameondoka katika meli hiyo na taratibu za mwisho zinaendelea ili kuwarudisha katika nchi zao ,"alisema na kuongeza kuwa uamuzi umechukuliwa kwa kuzingatia "sera za kibinadamu ". za Iran.

Bwana Mousavi amesisitiza kuwa mamlaka za Iranhazina tatizo na ''wahudumu wa meli na nahodha " na suala lilikuwa ni "ukiukaji wa sheria uliotekelezwa na chombo ".
Hata hivyo hakusema kuhusu kile kitakachotokea kwa Wahindi 13, Warusi wawili na Mfilipino mmoja - wahudumu waliosalia wa meli hiyo.
Stena Bulkimesema kuwa haina taarifa au ushahidi wowote unaooonyesha kuwa Stena Impero ilikiuka masharti au sheria zozote za safari za majini na kwamba iko nyuma ya wafanyakazi wake kwa kuwa walifuata masharti na mienendo ya kitaaluma.
Uingereza imesema kuwa Iran haikuwa na haki ya kufunga njia ya chombona ikaishutumu kwa "kufanya kitendo cha uharamia ".














