Ziara ya Papa Afrika: Je, Afrika ndio inayotoa matumani ya kanisa katoliki?

A nun reacts at Namugongo Martyrs' Shrine during an open air mass held by Pope Francis on November 28, 2015

Chanzo cha picha, Getty Images

Papa Francis anaanza ziara yake ya mataifa matatu ya Afrika hii leo.

Hii ni ziara yake ya nne barani Afrika toka achukue hatamu za uongozi wa Kanisa Katoliki Duniani mwaka 2013, ukilinganisha na mtangulizi wake Papa Benedict XVI, ambaye alizuru Afrika mara mbili tu katika uongozi wake wa miaka nane.

Umuhimu wa Afrika kwa Kanisa Katoliki unaweza kuelezwa kwa maneno machache - ukuaji wa wafuasi.

Utafiti unaonyesha kuwa Afrika ina ongezeko kubwa la idadi ya wafuasi wa kanisa Katoliki duniani, huku magharibi mwa Ulaya ambako kuna wakati kuliwahi kutambuliwa kama moyo wa ukristo lakini sasa hivi eneo hilo limekuwa sehemu ambayo haijihusishi na ukristo.

Na wengi ambao wanajitambulisha kama wakristu magharibi mwa Ulaya huwa hawaendi kanisani mara kwa mara .

Na kufanya ukristo kuonekana kuwa unakuwa zaidi barani Afrika.

Utafiti huo uliofanywa na 'Pew Research Center ' umeatabiri kuwa ifikapo mwaka 2060 , wakristo wanne kati ya kumi watakuwa wametoka Afrika kusini mwa jangwa la sahara .

School children wait for Pope Francis' arrival at Lubaga Cathedral in Kampala on November 28, 2015.

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Waumini wa kanisa Katoliki waongezeka Afrika

Utafiti huo ambao umechapishwa na kituo cha utafiti nchini Marekani umeonyesha kuwa kuwa katika kipindi cha kati ya mwaka 1980 na 2012 idadi ya wakatoliki imeongezeka kwa asilimia 57 kwa bilioni 1.2 huku ukuaji barani ulaya ni aslimia 6 ukilinganisha na Afrika ni asilimia 283.

"Nadhani kanisa katoliki hatma yake kwa siku za mbeleni ni Afrika", alisema mtafiti Nicolette Manglos-Weber ambaye ni Profesa msaidizi wa dini na jamii katika chuo kikuu cha Boston.

Imejenga shule na hospitali

Kanisa katoliki linakuwa kwa kasi barani Afrika kwa sababu ongezeko la waumini pia linaongezeka kwa kasi tofauti na mabara mengine.

Hata hivyo kuna sababu nyingine ambazo zinafanya kanisa katoliki likue kwa kasi na miongoni mwa sababu hizo ni huduma za kijamii ambazo zinatolewa na kanisa hilo kwa kiwango kikubwa.

"Kanisa katoliki linatoa huduma ya hospiali, shule na huduma nyingine kwa jamii. Vitu ambavyo serikali za Afrika zimekuwa zikikabiliana na changamoto kuzitoa kwa wingi...Jukumu la kanisa kutoa huduma hizo imelifanya kuwa tofauti na makanisa mengine ya kiprotestanti au jumuiya za kiislamu," Ms Manglos-Weber adds.

Papa Francis a meweza kuongeza wawakilishi wa Afrika katika nafasi za juu za kanisa hilo.

Ingawa makadinari wengi bado wametoka Ulaya na kusini mwa Amerika, Papa amechagua makadinari 10 kutoka Afrika tofauti na sita ambao walichaguliwa na mtangulizi wake.

Papa Francis anazielezea kuwa nchi za Afrika, Asia na Amerika ya kusini kuwa ni eneo la kipato kidogo na cha kati.

Papa huyo amejipatia sifa kuwa ni kiongozi wa askini wanyonge na ametoa kipaumbele kwa mabadiliko ya tabia nchi na kutokuwa na usawa Afrika.

Papa tayari amewahi kutembelea nchi tano za Afrika-,Kenya, Uganda, Afrika ya kati, Misri na Morocco na katika ziara yae atatembelea Msumbiji na nchi za visiwani za Madagascar na Mauritius.

Mtangulizi wake alitembelea nchi tatu tu za Afrika.

"Baba huyu mtakatifu alitaka hoteli za bei na kukataa hoteli ya kifahari ambayo alichagulia akiwa Vatcan na kuulizia hoteli ya bei rahisi kwa wasaidizi wake, kiongozi wa kanisa nchini Msumbiji alinukuliwa akiviambia vyombo vya habari.

A poster welcoming Pope Francis to Kenya is pictured in the Kangemi slum on November 24, 2015 in Nairobi, Kenya.

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Papa alitembelea Kenya mwaka 2015

Katika ziara yake nchini Kenya mwaka 2015 alitembelea Kenya na kutembelea kwenye nyumba duni za Kangemi zilizopo Nairobi na kuzungumzia kuhusu ukoloni mambo leo.

Aliwahutubia umati wa watu kuwa analaani haki ambayo watu wanakosa na kuwafanya waangaike na kufananisha na jeraha au maisha duni.

Presentational grey line

Katika ziara hiyo ya siku sita, Papa alieneza ujumbe wake wa Amani, maridhiano, mashauriano na kuchochea juhudi za kuzima migawanyiko.

Akiwa nchini Kenya, Papa Francis alisema: "Vijana ndio rasilimali yenye thamani zaidi kwa taifa. Kuwalinda, kuwekeza katika vijana, na kuwasaidia, ndiyo njia bora zaidi ya kuhakikisha siku njema za usoni zenye kufuata busara na maadili ya kiroho ya wazee wetu, maadili ambayo ndiyo nguzo ya jamii."

Papa alitumia Kiswahili kuhitimisha hotuba yake, akisema: "Mungu abariki Kenya!"

Alikuwa ameandika maneno yayo hayo kwenye akaunti yake ya mtandao wa kijamii wa Twitter alipokuwa safarini, saa moja hivi kabla ya kuwasili Kenya.

Kando na Papa Francis, Mapapa wawili wengine wamewahi kuzuru mataifa ya Afrika.

Wa kwanza alikuwa Papa Paul VI aliyezuru Uganda mwaka 1969.

Baadaye Mtakatifu John Paul II alizuru mataifa 42 ya Afrika akitembelea Kenya mwaka 1980, mwaka 1985 na mwaka 1995; Uganda mwaka 1993; na Jamhuri ya Afrika ya Kati 1975.

Papa Francis

Pope Francis looks on at the end of the Wednesday general audience in Saint Peter"s square at the Vatican November 22, 2017.

Chanzo cha picha, Reuters

  • Alizaliwa Jorge Mario Bergoglio tarehe 17 Desemba 1936
  • Elimu yake aliipata Argentina, Chile na Ujerumani
  • Aliapishwa kuwa kadinari mwaka 1998
Presentational grey line