6174: Kwanini takwimu hii imewatatiza wataalamu wa hesabu kwa zaidi ya miongo 7?

The number 6174, written down in multi-tone watercolours
Maelezo ya picha, Kitu gani kikubwa kuhusu nambari hii?

Itazame takwimu hii: 6174.

Kwa mtazamo wa kwanza, huenda sio kitu kikubwa - lakini imewatatiza wataalamu wa hesabu tangu mwaka 1949.

Kwanini? Haya ni mambo ya kustaajabisha na unayostahili kuyafahamu mwenyewe:

  • Chagua takwimu yenye nambari 4, nambari yoyote unayotaka, ilioyo na nambari tofauti angalau mbili (ikiwemo sifuri). Mfano 1234
  • Zipangilie kutoka kubwa kushuka chini: 4321
  • Sasa zipange kutoka ndogo kwenda kubwa: 1234
  • Punguza takimu ndogo kutoka kubwa: 4321 - 1234
  • Sasa rudia hatua ya 2, 3, na 4 kwa kutumia matokeo ya hesabu hiyo

Hebu tulifanye kwa pamoja

  • 4321 - 1234 = 3087
  • Zipangilie kutoka kubwa kushuka chini: 8730
  • Sasa zipange kutoka ndogo kwenda kubwa: 0378
  • Punguza takimu ndogo kutoka kubwa: 8730 - 0378 = 8352
  • Sasa turudie hatua tatu za mwisho kwa matokeo ya hesabu

Sasa tunatumia 8352

  • 8532 - 2358 = 6174

Rudia tena kwa kutumia 6174 -pangilia takwimu kutoka ndogo hadi kubwa na kubwa hadi ndogo na hesabu tofauti kati ya takwimu hizo mbili

  • 7641 - 1467 = 6174

Kama unavyoona, kutoka hapa hakuna haja ya kuendelea tena - utapata mfumo na takiwmu ya mwisho hiyo: 6174

Pengine unaweza kudhani hii ni sadfa. hebu tujaribu kwa kutumia takwimu nyingine tofauti. Mfano 2005?

  • 5200 - 0025 = 5175
  • 7551 - 1557 = 5994
  • 9954 - 4599 = 5355
  • 5553 - 3555 = 1998
  • 9981 - 1899 = 8082
  • 8820 - 0288 = 8532
  • 8532 - 2358 = 6174
  • 7641 - 1467 = 6174

Kama inavyoonekana, haijalishi ni takwimu gani utakayotumia, punde sio punde hesabu inaishia 6174, na kutoka hapo ni mfumo uo huo na matokeo yayo hayo.

Uvumbuzi wa Kaprekar

An abacus with red heart-shaped beads, over a bright blue background

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Kaprekar alipenda hesabu na alitumia muda mwingi akicheza na takwimu

Hongera sasa unaufahamu uvumbuzi wa maarufu 'Kaprekar's Constant'.

Mtaalamu wa hesabu kutoka India Dattatreya Ramchandra Kaprekar (1905-1986) alipenda sana kucheza na nambari na hivi ndivyo alivyovumbua uzito wa takwimu 6174.

Kaprekar aliwasilisha uvumbuzi huu duniani katika mkutano wa hesabati uliofanyika katika mji wa Madras nchini India mnamo 1949.

"Mlevi anataka kuendelewa kulewa pombe ili kusalia na raha aliyo nayo. Ndio hali nilio nayo katika suala la nambari," aliwahi kusema.

Kaprekar alisoma katika chuo kikuu cha Mumbai na alihudumu kama mwalimu maishani mwake katika kijiji cha Devlali, milimani kaskazini mwa Mumbai.

Licha ya kwamba uvumbuzi wake ulikejeliwa na kupuuzwa na wataalamu wa hesabu India - walioona kazi yake kuwa ni upuuzi na isio namaana - alikuwa mwandishi tajika hususan katika majarida maarufu ya sayansi.

Aliwahi pia kualikwa mara kwa mara kushiriki katika warsha au kuzungumzia katika hlafla shuleni na katika vyuo vikuu kuhusu mbinu au mfumo wake wa ajabu na mitazamo yake ya kuvutia kuhusu takwimu.

Maelezo ya video, Sibahle Zwane: Mtoto bingwa wa maswali ya hesabu kutoka Afrika Kusini

Anayecheka wa mwisho....

Taratibu, fikra za Kaprekar zikaanza kupata umaarfu nyumbani na nje ya nchi - kufikia miaka ya 1970, mwandishi mashuhuri wa Marekani anayependa hesabati Martin Gardner aliandika kitabu kumhusu katika jarida maarufu la sayansi Scientific America.

Hii leo Kaprekar na uvumbuzi wake anatambulika na kutumika na wataalamu wa hesabu duniani hususan kwa wale ambao kama yeye - hawawezi kujuzuia kucheza na takwimu.

Yutaka Nishiyama, mhadhiri katika chuo kikuu cha Osaka cha Uchumi anasema "Nambari 6174 ni nambari ya ajabu".

Katika makala iliyochapishwa kwenye jarida la mtandaoni +plus, Nishiyama anafafanua namna alivyotumia " kompyuta kuaini iwapo nambari zote nne zinafika 6174 katika hatua kadhaa ".

Matokeo yake? kila takwimu yenye nambari nne ambazo hazifanani hufika jumla ya 6174 chini ya mfumo wa Kaprekar kwa hatua zisizozidi 7.

"Usipofika 6174 baada ya kutumia mfumo wa Kaprekar mara saba, basi umefanya makosa katika hesabu yako na unabidi urudia tena!" Nishiyama anasema.

Kujiburudisha kwa hesabu

Little boy learning with abacus at preschool

Chanzo cha picha, Getty Images

Kaprekar's constant sio mchango pekee kwa hesabati, mtu aliyetumia hesabu kama kiburudisho.

Pengine umewahi pia kusikia kuhuhu nambari ya Kaprekar : nambari ambayo inaporegelewa kwa mraba uwakilishi wake unaweza kugawanywa kwa nambari mbili ambazo jumla yake ni sawa na takwimu ya awali.

Huenda mfano ukakusaidia kuelewa zaidi:

  • 297² = 88,209
  • 88 + 209 = 297

Mingine ya nambari ya Kaprekar ni: 9, 45, 55, 99, 703, 999, 2,223, 17,344, 538,461...Zijaribu mwenyewe alafu uone kitakachofanyika!

Sasa hata wewe ni mtaalamu wa hesabati, angalau kujiburudisha!