Kimbunga Doriani: Bahamas yapigwa na kimbunga kibaya zaidi

In this NOAA GOES-East satellite image, Hurricane Dorian leaves the Caribbean Sea and tracks towards the Florida coast taken at 14:20 UTC August 29, 2019 in the Atlantic Ocean.

Chanzo cha picha, Getty Images

Kimbunga chenye nguvu zaidi kimepiga visiwa vya Bahama nchini Marekani na kuvunja rekodi za vimbunga vyote vilivyowahi kupiga na kusababisha maafa makubwa .

Hii ni dhoruba ya pili katika rekodi ya bahari ya atlantiki ambayo imeweza kustahimili mawimbi mpaka kufikia 175mph (285kilometa kwa saa).

Kimbunga hicho kinaendelea kusonga taratibu magharibu na kinaweza kufika mashariki ya bahari ya Marekani, majimbo ya Marekani ya Florida, Georgia na South Carolina yote .

Dhoruba hii inavuma vya kasi ndogo ambayo inasafiri toka magharibi ambayo ni kilometa 9 kwa saa ambayo ni sawa na mph 6.

Satellite image shows Dorian as it approaches the Bahamas

Chanzo cha picha, AFP

Lipi jipya kutoka Bahamas?

Kituo maalum cha janga la kimbunga kimesema kuwa kimbunga hicho kilipiga majira ya saa kumi, dhoruba hiyo ilitokea pembezoni mwa mashariki mwa Bahama, na kutua katika kisiwa cha Abaco.

Grand Bahama ina jumla ya idadi ya watu ambayo ni takribani 50,000, wanaoishi umbali wa kilometa 100 mashariki magharibi mwa pwani ya Palm huko Florida.

'Ni dhoruba yakutishia maisha' ambayo ipo katika futi 23 ambayo ni sawa na mita 7 kama inavyokadiriwa katika baadhi ya maeneo.

Mpaka sasa hakuna kauli rasmi kutoka kwa maafisa wa visiwa vya Bahamas juu ya majanga hayo.

Ingawa kuna ripoti ambayo imetolewa kuwa maeneo yaliyoathirika Bahamas yanakumbwa na changamoto ya umeme na shida ya mtandao.

Hata hivyo, video na picha zilizotumwa katika mtandao wa Twitter na Bw. Latrae Rahming ambaye ni msaidizi wa waziri mkuu mstaafu Perry Christie, zinaonesha maafa makubwa katika visiwa vya Abaco, ambayo ni makazi ya takribani watu 17,000.

Magari yamejaa maji, paa zimeharibiwa na maji ya pwani ambayo yamefikia ukingo wa paa.

Graphic
Presentational white space

Mkurugenzi mtendaji wa wizara ya utalii na anga, amesema ; 'Inaumiza, kumekuwa na uharibifu mkubwa kwa mali na miundombinu. Bahati nzuri hakuna upotevu wa maisha ambao mpaka sasa umeripotiwa'.

Hata hivyo; Taarifa kutoka kwa mashuhuda zinasema kuwa kuna mtoto mmoja ambaye amedai mjukuu wake wa miaka 8 amezama katika visiwa hivyo vya Abaco.

Waziri mkuu Hubert Minnis ameamuru watu wote wanaoishi maeneo ya Grand Bahama na kisiwa cha Abaco kuhama makazi yao , na watalii wote waliombwa kuondoka maeneo hayo.

Ingawa kuna baadhi ya watu wameripotiwa kugoma kuhama makazi yao.

A flooded car park in Miami Beach on 30 August 2019

Chanzo cha picha, Getty Images

"Nnachoweza kusema ni kwamba natumai, hii si mara ya mwisho watasikia sauti yangu, Mungu awe nao"Bw. Minnis alisisitiza.

Waziri mkuu huyo mkuu aliongeza kusema kuwa inawezekana kuwa ni siku mbaya kuliko zote za maisha yake duniani." Tunapambana na kimbunga… ambacho hakijawahi kutokea katika historia ya Bahamas."

Presentational white space
People look at a road damaged due to Dorian in Riviere-Pilote, Martinique

Chanzo cha picha, Reuters

Vipi kuhusu Marekani?

Japo kuwa dhoruba hiyo kwa sasa inaelekea magharibi, imetabiriwa kubadili muelekeo wa kwenda kaskazini magharibi, huku ikielekea mashariki mwa bahari ya Marekani.

Raisi Donald Trump amehairisha safari yake ya kuelekea nchini Poland na kukutana na maafisa wa usimamizi wa majanga ya dharura.

Rais Trump amewaambia waandishi wa habari siku ya jumapili kuwa "hali ni mbaya" upande wa pwani ya mashariki ya Marekani kwa sababu bado baadhi ya maeneo yanaendelea kuathirika.

Presentational white space
A shell lies on a white sand beach in this glamour shot of the Bahamas
Getty Images
Commonwealth of the Bahamas

Capital: Nassau

  • Population391,000

  • Area13,939 sq km (5,382 sq miles)

  • Major languageEnglish

  • Major religionChristianity

  • Life expectancy72 years (men), 78 years (women)

  • CurrencyBahamian dollar

Source: UN, World Bank

Kimbunga kimekuwa kikubwa, na mawimbi yameongezeka mpaka kufikia maili 45 ambayo ni takribani kilometa 75 kutoka mwanzo wa kimbunga hicho.

Raisi Trump ametoa kauli iliyotoa hali ya dharura ya shinikizo kwa jimbo la Florida, na majimbo ya gavana Ron De Santis ambaye aliwaandaa askari 2000 wa kutetea dharura ya taifa , na wengine 2000 kuwa tayari.

Residents load sandbags to protect their homes in Deltona, Florida, as they prepare for Hurricane Dorian, on August 31, 2019.

Chanzo cha picha, AFP

Bw. DeSantis alitoa tahadhali kwa watu kutojumuika kutokana na mabadiliko ya kimbunga yanayotabiriwa kuendelea kutokea.

'Hiki kimbunga katika hatua hii kinaweza kuleta maafa makubwa zaidi' alisema.

Vivutio maarufu, kikiwemo 'Disney World mjini Orlando', vipo katika uangalizi mkubwa hivi sasa.

Nguzo za umeme katika mitaa ya Miami zimeamuriwa kuondolewa ili kuepuka maafa zaidi.

Watu wameanza kuhamishwa kwa lazima maeneo ya pwani ya South Carolina, watu 830,000 wameathirika ikifuatiwa na Georgia.

Storm damage in Marsh Harbour, the Abaco islands

Chanzo cha picha, Reuters

Maelezo ya picha, Picha katika mitandao ya kijamii ikionyesha kisiwa cha Abaco

Je, mabadiliko ya tabia nchi yanasababisha kutokea kwa kimbunga mara kwa mara

Wanasayansi hawawezi kusema kama mabadiliko ya tabia nchi yameongeza idadi ya matukio ya kimbunga.

Hata kama mwaka 2018 ulikuwa mwaka wa tatu ambao kuna dhoruba za wastani katika ukanda wa Atlantiki,.

Hata hivyo wengi huwa hawaamini kama mabadiliko ya tabia nchi ndio zinasababisha dhoruba mbalimbali.

Na hii ni kwa sababu kuu mbili:.

Sababu ya kwanza ni kuongeza kwa joto la bahari ambalo linaongeza kasi ya upepo ,dhoruba linapopiga na kusaongeza kiwango cha kimbunga.

Kuna suala la kuongezeka kwa kina cha bahari.

Kina hicho kinatarajia kuongezeka kutoka mguu mmoja mpaka minne ifikapo karne ijayo.

Karne chache zilizopita matukio ya aina hiyo yalikuwa yanakuja kwa kiwango kidogo.

Presentational grey line

Ni uharibifu wa kiasi unaletwa na kimbunga?

Kasi ya upepo ni 157mph, pepo hizi ni za nadra japo vimbunga vingine vine vilishawahi kufikia hatua hii miaka mitatu iyopita;

  • Michael ilitua jimboni Florida mwaka jana ambacho kilisababisha vifo 59 na uharibifu wa thamani dola bilioni 25. Kilikuwa ni kimbunga chenye nguvu kuliko vyote kutua Marekani ndani ya miaka 26 na kimbunga hiki cha nne kimesababisha ghasia kubwa zaidi nchini.
  • Maria, mnamo mwaka 2017, iliharibu kisiwa cha Dominica , ambapo pia kilisababisha vifo vya watu 31 kabla ya kueneza maafa mjini Puerto Rico.
  • Mnamo mwaka 2017 Irmano ilitua mara saba, huku mara nne ikiwa katika jamii ya tano, pembezoni mwa kaskazini mwa visiwa vya Caribbean, kabla ya kutua katika jimbo la Florida ikiwa kama jamii ya nne ya kimbunga hicho.
Presentational white space