Familia ya mwanamuziki Aaliyah yawakosoa mashabiki wanaolilemba sanamu lake

Chanzo cha picha, Getty Images
Familia ya Aaliyah imeomba kuwepo na "heshima" baada ya watu kuonekana wakiongezea kupaka lipstiki sanamu la mwanamuziki huyo wa pop lililopo katika eneo la Madame Tussauds mjini Las Vegas.
Sanamu hilo linalofananana na marehemu Aaliyah limekuwepo mahali hapo kwa siku tano tu-lakini baadhi wamekuwa wakipigwa picha wakiongezea urembo wao zaidi kwenye sanamu hilo.
Twitter rasmi ya Aaliyah' imeitaja tabia hiyo kama "isiyofaa na isiyokubalika".
Muimbaji huyo aliyetunukiwa tuzo mbalimbali za muziki alifariki katika ajali ya ndege mwaka 2001 akiwa na umri wa miaka 22.
Mkala hii imebeba madhui yaliyotoka kwenye mitandao ya kijamii. Tunaomba ruhusa yako kabla kitu chochote hakija pakiwa, sababu wanaweza wakawa wanatumia Cookies na tekinolojia nyingine. Unaweza ukasoma sera sera ya kutumia cookies katika mitandao ya kijamii kabla ya kukubali. Kutazama maudhui haya chagua accept and continue
Mwisho wa X ujumbe, 1
Sanamu hilo lililotengenezwa kwa nta limeonyeshwa kwa umma kwa ajili ya maadhimisho ya 18 tangu kifo chake.
Ukurasa wa Twitter wa mwanamuziki huyo pia ulituma ujumbe kutoka kwa Madame Tussauds Las Vegas ukisema wana wahudumu kwenye wavuti wao kila sikuambao "hupanga upya " namba na kuhakikisha "zinaonekaba bora zaidi".
Akaunti ya Aaliyah ilituma ujumbe huu uliosema: "Ni aibu kwamba baadhi ya watu hawana heshima".
Mkala hii imebeba madhui yaliyotoka kwenye mitandao ya kijamii. Tunaomba ruhusa yako kabla kitu chochote hakija pakiwa, sababu wanaweza wakawa wanatumia Cookies na tekinolojia nyingine. Unaweza ukasoma sera sera ya kutumia cookies katika mitandao ya kijamii kabla ya kukubali. Kutazama maudhui haya chagua accept and continue
Mwisho wa X ujumbe, 2
Aaliyah alikuwa nani ?
Aaliyah Haughton - ambaye alifahamika zaidi kwa jina lake la kwanza - alikuwa Muimbaji wa muziki wa R&B, mchezaji filamu na mwanamitindo wa Marekani.
Akizaliwa mwaka 1979 mjini New York na kukulia Detroit.

Chanzo cha picha, Getty Images
Albamu yake ya kwanza ya muziki iliyokuwa na wimbo Age Ain't Nothing But a Number ilirekodiwa akiwa na umri wa miakma 14 kwa usaidizi wa msahuri wake R Kelly.
Baadae aliteuliwa kwa tuzo mbali mbali za Grammys, na kushinda tuzo mkiwemo tuzo za MOBO na za Muziki wa Marekani.
'Try Again' ulikuwa ni moja ya nyimbo zake maarufu. Alitengeneza filamu yake akicheza kama 'Romeo Must Die' sambamba na sanamu ya 'Jet Li'.

Chanzo cha picha, Reuters
Aaliyah aliolewa na R Kelly alipokuwa na umri wa miaka 15 na Kelly akiwa na umri wa miaka 27, katika sherehe ya siri. Ni nadra sana kuelezea mahusiano yao.
Tarehe 25 Agosti 2001 Aaliyah alikuwa anarejea Marekani baada ya kuchukua video ya filamu ya muziki katika visiwa vya Abaco vilivyoko Bahamas wakati alipokufa katika ajali ya ndege.
Watu wengine wanane waliokuwemo ndani ya ndege hiyo pia walikufa.














