Kim Jong Un asimamia jaribio la makombora mawili Korea kaskazini

Korea Kaskazini imesrusha makombora mawili ya masafa mafupi baharini kulingana na jeshi la Korea Kusini.

Jaribio hilo ni la saba kutekelezwa tangu Korea Kaskazini ilipomaliza mpango wake wa miezi 17 wa kusitisha majaribio yoyote ya silaha zake.

Jaribio hilo lilisimamiwa na rais wa taifa hilo Kim Jong Un kulingana na chombo cha habari cha taifa hilo KCNA. Chombo hicho kilisema kwamba lilikuwa jaribio la kombora kubwa ambalo ilisema liliundwa hivi karibuni.

Kim Jong un alilitaja kombora hilo kuwa silaha nzuri huku akilishukuru kundi la watalaam waliounda makombra hayo, KCNA ilisema.

Maafisa wa kijeshi wanasema kwamba makombora hayo yalirushwa saa kumi na mbili na dakika arobaini na tano na saa moja na dakika mbili muda wa Korea Kaskazini kutoka mji wa mashariki wa Sondok kusini mwa mkoa wa Hamgyong.

Wanasema kwamba makombora hayo yaliruka umbali wa kilomita 380 na urefu wa kilomita 97 kabla ya kuanguka katika bahari ya Japan, pia ikijulikana kama bahari ya mashariki.

''Jeshi letu linachunguza hali ilivyo iwapo majaribio zaidi yatafanyika huku tukujiandaa'' , alisema mkuu wa jeshi wa Korea Kusini.

Waziri wa ulinzi wa Japan , Takeshi Iwaya alihibitisha kombora hilo halikuanguka katika maji ya Japan lakini akataja kuwa ni ukiukaji wa wazi wa maazimio ya Umoja wa Mataifa.

Pyongyang tayari imeonyesha kukasirishwa na mazoezi ya kijeshi ya pamoja ya Marekani na Korea kusini ambayo yamekuwa yakiendelea.

Korea Kaskazini imeyataja kuwa maandalizi ya vita na kusema kwamba yanakiuka makubaliano walioafikia na rais wa Marekani Donald Trump na rais wa Korea Kusini Moon Jae-in.

Marekani na Korea kusini zimekataa kufutilia mbali mazoezi hayo na kwamba wameyafanya kuwa ya kiwango cha juu.

Katika taarifa ya rais siku ya Jumamosi Korea kusini ilitoa wito kwa Korea Kaskazini kutoongeza wasi wasi wa kijeshi uliopo huku akisisitiza mpango wao wa mazungumzo na Marekani kwamba utaendelea.

Mazungumzo ya kutounda silaha za kinyuklia yamekwama tangu mkutano wa ana kwa ana kati ya Trump na kiongozi wa Korea Kaskazini Kim mJong Un kugonga mwamba mnamo mwezi Februari.

Mwezi Juni viongozi hao wawili walikutana katika eneo la mpakani kati ya mataifa hayo ya Korea na kukubaliana kuendelea na mazungumzo.

Akizungumza baada ya majaribio hayo mawili , rais Donald Trump alisisitiza kwamba ana uhusiano mzuri sana na bwana Kim ambaye anasema kuwa amekuwa mkweli kwake.

Ni nini kinachoendelea sasa?

Korea kaskazini hivi karibuni ilipaza sauti ya hasira yake dhidi ya mazoezi yaliyopangwa kufanyika baina ya Marekani na Korea Kusini, tukio la mwaka ambalo washirika wamekataa kuachana nalo ,lakini limeleta athari kubwa.

Korea kaskazini inayaona mazoezi hayo ya kijeshi lama maandalizi ya vita na iliyaita "uvuriugaji wa roho " wa kauli ya pamoja aliyoisaini Bwana Trump na Kim katika kikao chao cha kwanza cha ana kwa ana cha mwaka jana cha Singapore.

Pyongyang ilikuwa imeonya kwamba mazoezi hayo yanaweza kuathiri kufufuliwa kwa mazungumzo ya kuanchana na nyuklia.

Jumatatu waziri wa mambo ya kigeni wa Marekani Mike Pompeo alisema kwamba anatumaini mazungumzo haya yanaweza kuanza "haraka sana '', lakini hakuna mkutano uliopangwa.

Vipi kuhusu uhusiano wa Marekani na Korea kaskazini ?

Mwaka jana , Bwana Kim alisema Korea Kaskazini ingesitisha majaribio ya nuklia, na ingeacha kufyatua tena makombora ya masafa marefu yanayoweza kuvuka mipaka ya mabara.

Shughuli za nyuklia zinaelekea kuendelea, hata hivyo , na picha za setilaiti za kituo kikuu cha nyuklia cha Korea Kaskazini mwezi uliopita zilionyesha kuwa taifa hilo huenda linatengeneza mionzi ya inayochochea makombora.

Serikali ya Pyongyangpia inaendelea kuonyesha uwezo wake wa kutengeneza silaha mpya licha ya kuwekewa vikwazo vikali vya kiuchumi.

Ilifyatua kombora la masafa mafupi la aina hiyo mapema mwezi Mei ,likiwa ni kombora la kwanza la aina yake tangu iliporusha kombora la ballistic mnamo mwaka 2017.

Korea Kaskazini pia ilionyesha manuwari yake ya kijeshi wiki iliyopita, ambayo maafisa wa Korea Kusini wamesema ina uwezo wa kubeba makombora hadi matatu ya masafa ya ballistic.