Programu ya Google inayofasiri na kutamka lugha ya ishara

Chanzo cha picha, Google AI
Google inasema imeunda programu inayoweza kufanikisha simu kufasiri na 'kusoma kwanguvu' lugha ya ishara.
Kampuni hiyo ya teknolojia haijaunda programu tumishi lakini imechapisha utaratibu ambao inatumai utawasaidia wavumbuzi kuunda programu zao tumishi
Kufikia sasa programu ya aina hii imefanikiwa kufanya kazi katika kompyuta tu.
Wanaharakati kutoka jamii ya watu wenye ulemavu wa kusikia wameikaribisha hatua hiyo, lakini wanasema teknolojia hiyo huenda ikapata changamoto kunakili kikamilifu baadhi ya mawasiliano.
Katika blogu ya AI , wahandisi watafiti wa Google Valentin Bazarevsky na Fan Zhang wamesema dhamira ya teknolojia hiyo iliyochapishwa bure ni kuhudumia 'kwa misingi ya kuelewa lugha ya ishara'.
Iliundwa kwa ushirikiano na kampuni ya MediaPipe.
"Tunafurahia kuona watu watakachokivumbua. kwa upande wetu, tutaendelea na utafiti wetu kuifanya teknolojia kuwa thabiti na iliyoimarika,kuongeza idadi ya ishara ambazo tunaweza kuzitambua," msemaji wa Google ameiambia BBC.
Google imetambua hii kama hatua ya kwanza. Wanaharakati wanasema programu inayotoa sauti kutoka ishara za mikono pekee utakosa kutambua hisia usoni mwa mtu au kasi ya kutoa ishara na hili linaweza kubadili maana ya kinachosemwa.

Chanzo cha picha, Google
Jesal Vishnuram, msimamizi anayehusika na teknolojia ya ulemavu wa kusikia anasema jitihada hiyo ni hatua ya kwanza nzuri kwa watu wanaosikia, lakini inahitaji kujumuishwa na uwezo mwingine.
"Kutoka mtazama wa mtu mwenye ulemavu wa kusikia, itakuwana manufaa zaidi kwa programu kuundwa itakayoweza kutoa ufasiri wa moja kwa moja wa maandishi au sauti kuigeuza pia kuwa lgha ya ishara kusaidia mawasiliano ya kila siku na kupunguza kutengwa kwa watu wenye ulemavu wa kusikia," amefafanua.
Vidole vilivyofichwa
Kufikia sasa, kwa kujaribu kufuatilia ishara za mikono kwenye video, mkunjo wa vidole na kupeta kwa mkono kumeficha sehemu nyingine za mkono. Hili lilizusha mchanganyiko wa programu za awali za aina hiyo.
Google inaweka grafu ya pointi 21 katika vidole, kiganjani na sehemu ya nyuma ya mkono, jambo linalofanya kuwa rahisi kuelewa ishara ya mkono, wakati mkono ukipinda au wakati vidole viwili vikishikana.
Makampuni mengine ya teknolojia Marekani yameunda teknolojia zilizojaribu kusoma kwa suati lugha ya ishara kwa kutumia kompyuta.
Mwaka jana, Microsoft ilishirikiana na taasisi ya kitaifa ya teknolojia kwa walemavu wa kusikia kutumia kompyuta katika madarasa zilizowasaidia wanafunzi wenye ulemavu huo kwa kutumia mfasiri mtangazaji.

Chanzo cha picha, Microsoft
Baadhi ya wanafunzi walilalamika katika blogu kukosa baadhi ya walichokuwa wakisema wahadhiri kwasababu walitatizika kwa kilichokuwa kikiandikwa ubaoni na kile kilichokuwa kikisemwa na mtu aliyetumia lugha ya ishara.
lakini baada ya kupata mawasiliano yote kwenye kompyuta, tatizo hilo lilitatulika.
Kwengineko duniani, wavumbuzi wameunda teknolojia katika maenoe walioko.
Kijana mmoja mwenye umri wa miaka 25 nchini Kenya ameunda glavu za mikono zinazofasiri lugha hiyo ya ishara kupitia programu tumishi ya Android inayofasiri kwa sauti.
Roy Allela alimuundia mpwa wake glavu hizo ambaye ana ulemavu wa kusikia , na uvumbuzi huo umeshinda tuzo hivi karibuni kutoka jamii ya wahandisi wa mitambo Marekani.
















