Makubaliano ya kinyuklia ya INF: Marekani imelifanyia majaribio kombora lake la masafa ya kadri

Pentagon ilitoa picha ya jaribio hilo la silaha lililofanyika katika kisiwa cha San Nicolas Island tarehe 18 Agosti 2019

Chanzo cha picha, AFP

Maelezo ya picha, Pentagon ilitoa picha ya jaribio hilo la silaha

Marekani imefanyia jaribio kombora lake la masafa ya kadri wiki kadhaa baada ya kujiondoa katika makubaliano muhimu na Urusi yaliopiga marufuku silaha zenye uwezo kama huo za kinyuklia.

Pentagon imesema kwamba ilifanikiwa kurusha kombora hilo katika pwani ya California siku ya Jumapili.

Marekani ilijiondoa katika makubaliano hayo mnamo tarehe 2 Agosti baada ya kuishutumu Urusi kwa kulikiuka azimio hilo madai ambayo Moscow imekana.

Wachanganuzi wanohofia kwamba kuanguka kwa makubaliano hayo kutazua ushindani wa utengenezaji wa silaha mpya.

Makubaliano hayo yalioafikiwa katika kipindi cha vita baridi yalipiga marufuku silaha zenye uwezo wa kurushwa kati ya kilomita 500 hadi 5,500.

Pentagon imesema kwamba kombora hilo lililofyatuliwa kutoka kisiwa kinachodhibitiwa na wanamaji wa Marekani cha San Nicolas katika pwani ya Los Angeles, lilikuwa halina kichwa cha kinyuklia.

Silaha hiyo iliofanyiwa majaribio iliafikia lengo lake la zaidi ya kilomita 500, kulingana na idara ya ulinzi nchini Marekani.

Data iliokusanywa na mafunzo kutoka katika jaribio hilo itaelezea idara ya ulinzi kuhusu uundaji wa silaha za masafa ya kadri katika siku za usoni kuhusu uwezo wake.

Je ni nini kitakachofanyika na makubaliano hayo?

Urusi imeshutumiwa kwa kukiuka masharti ya mkataba huo katika siku za nyuma, lakini mapema mwaka huu, Marekani na Nato ilisema kwamba kulikuwa na ushahidi kwamba Moscow ilikuwa na mpango wa kurusha kombora jipya aina ya 9M729 linalojulilkana na Nato kama SSC-8.

Urusi imekana shutuma hizo na rais Putin alisema kwamba Marekani ilifanya makosa makubwa kujiondoa katika makubaliano hayo.

Mnamo mwezi Februari rais Trump aliweka siku ya mwisho ya Agosti 2 kwa Marekani kujiondoa katika makubaliano hayo iwapo Urusi itaendelea kukiuka masharti yake.

Rais wa Urusi Vladimir Putin alipiga marufuku makubaliano ya taifa lake katika mkataba huo muda mfupi baadaye.

Marekani ilijiondoa katika makubaliano hayo baada ya kutishia kufanya hivyo mnamo tarehe 2 Agosti na waziri wa maswala ya kigeni Mike Pompeo alisema: Urusi ndio ya kulaumiwa kwa kuanguka kwa mkataba huo.

Kombora jipya la Urusi la 9M729 linaitia tumbo joto Marekani na washirika wake

Chanzo cha picha, Reuters

Maelezo ya picha, Kombora jipya la Urusi la 9M729 linaitia tumbo joto Marekani na washirika wake

Kuanguka kwa makubaliano hayo ya kihistoria kumesababisha wasiwasi kwamba huenda kukazuka mashindano ya uundaji wa silaha kati ya Marekani, Urusi na China.

Katibu mkuu wa Umoja wa mataifa Antonio Guterres alisema kwamba 'kipindi cha mapumziko' cha vita vya kinyuklia kimekiukwa.

''Hatua hiyo huenda ikachochea zaidi na sio kupunguza , tishio linaloweza kusabababishwa na makombora ya masafa marefu'' , alisema akizitaka pande zote kutafuta makubaliano ya pamoja kuhusu silaha za kimataifa.

Katibu mkuu wa Nato Jens Stoltenberg alisaema kwamba muungano wa mataifa yaliopo katika bahari ya Atlantic utajibu kuhusu hatari inayosababishwa na kombora la Urusi la 9M729 kwa usalama uliopo.

Lakini aliongezea, Nato haitaki ushindani wa silaha - alithibitisha kuwa hakuna mipango ya muungano huo kuunda silaha zake za kinyuklia Ulaya.

Mwezi uliopita aliambia BBC kwamba makombora hayo ya Urusi yana uwezo wa kubeba kichwa cha kinyuklia, yana kasi na vigumu kuyabaini na yanaweza kufika katika miji ya Ulaya kwa dakika chache.

Je makubaliano hayo ya silaha yanasemaje?

Kiongozi wa Soviet Mikhail Gorbachev na rais wa Marekani Ronald Reagan walitia saini makubaliano hayo ya 1987

Chanzo cha picha, AFP

Maelezo ya picha, Kiongozi wa Soviet Mikhail Gorbachev na rais wa Marekani Ronald Reagan walitia saini makubaliano hayo ya 1987
  • Baada ya kutiwa saini na Marekani pamoja na Urusi 1987, mkataba huo wa kudhibiti silaha ulipiga marufuku silaha zote za kinyuklia na zile ambazo sio za kinyuklia na silaha fupi na zile za kadri isipokuwa silaha zinazorushwa kutoka baharini.
  • Marekani ilikuwa na wasiwasi na hatua ya Urusi kulifanyia majaribio kombora lake la SS-20 mwaka 1979 na ilijibu kwa kupeleka makombora barani Ulaya hatua iliosababisha maandamano ulimwenguni.
  • Kufikia mwaka 1991, takriban makombora 2,700 yalikuwa yameharibiwa.
  • Mataifa hayo mawili yaliruhusiwa kukaguana