Vikwazo Iran: Madhara gani yanajitokeza kwenye soko la dawa

Mwanaume akiwa kwenye duka la dawa Iran

Chanzo cha picha, Getty Images

Iran imesema vikwazo dhidi yake vinazuia dawa za kuokoa maisha kuingia nchini humo, ingawa kumekuwa na msamaha wa bidhaa za dawa.

''Marekani imetoa msamaha kwa dawa na vifaa tiba kwa ajili ya raia wa Iran kwenye vikwazo vya Marekani,'' anasema Brian Hook, mwakilishi maalum wa Marekani nchini Iran.

Je ni kwa namna gani vikwazo vimeathiri upatikanaji wa dawa nchini Iran?

Aina gani ya dawa huingizwa nchini Iran?

Iran inatengeneza dawa zake nyingi lakini linapokuja suala la dawa zinazotengenezwa kwa teknolojia ya juu, Iran hutegemea zaidi dawa kutoka nje.

Inakadiriwa kuwa ingawa asilimia 4 ya dawa zake zinatoka nje kwa kuzingatia ujazo, dawa nyingi zenye ghara,a kubwa zinazoingizwa ni takribano theluthi ya thamani yake kwa ujumla.

Vikwazo vimesababisha ongezeko la gharama za bidhaa za dawa

Chanzo cha picha, AFP

Kuna data ndogo kuhusu dawa zinazoingia nchini Iran na gharama zinazolipiwa lakini ushahidi usio wa kisayansi unaweza kutoa picha ya namna hali ilivyo.

Idhaa ya uajemi ya BBC imesikia kutoka kwa wasikilizaji wake kuhusu kuogezeka kwa gharama za dawa.

Mwathirika wa ugonjwa wa tumbo ameeleza ugumu anaoupata kupata dawa muhimu za kutibu maradhi hayo.

''Ninalazimika kusafiri kwenye miji mingine na majiji kutazama maduka yao ya dawa kama yana dawa hizo,''alieleza.

''Baadhi ya maduka yana dawa hizo lakini gharama iko juu sana sina uwezo wa kununua.

Hospitali ya Tehran

Chanzo cha picha, Google

BBC pia ilizungumza na kampuni ya dawa inayoingiza dawa kutoka Iran, ambaye alisema katika kipindi cha miaka miwili iliyopita kulikuwa na uhaba wa dawa na gharama ilikuwa juu.

Dawa za usingizi, za kutibu saratani na sukari zilikuwa ngumu kupatikana, walieleza.

Katika kipindi cha mwaka mmoja uliopita, gharama za huduma za afya na dawa ziliongezeka kwa asilimia 19 kwa mujibu wa takwimu za Iran.

Lakini upungufu huu na ongezeko la gharama kunaweza kuwa na sababu nyingi, si tu matokeo ya vikwazo dhidi ya Iran.

Maelezo ya video, Vikwazo vya Marekani vinaiathiri vipi Iran?

Kwa namna gani vikwazo vinafanya kazi?

Vikwazo vya kimataifa viliondolewa mwaka 2016 baada ya makubaliano na Iran kuhusu mradi wa nyukilia, lakini mwezi Novemba mwaka 2018, Marekani iliweka vikwazo vikali dhidi ya viawanda vya Iran na taasisi za fedha.

Ilitishia kuiadhibu vikali na kuiondoa kwenye mifumo ya kifedha ya Marekani kwa makampuni ya nje yanayolenga kukwepa vikwazo hivi.

Daktari akichunguza macho ya mgonjwa

Chanzo cha picha, Getty Images

Hatahivyo, wasafirishaji wa bidhaa kama dawa na vifaa tiba na kampuni zinazofanya biashara hii hawapaswi kuadhibiwa na Marekani kwa kufanya biashara na Tehran.

''Tatizo ni kuwa unahitaji kutafuta benki itakayokuwa tayari kufungua milango ya kibiashara kushughulikia hilo,'' anasema Richard Nephew, na mtaalamu wa masuala ya vikwazo vya Marekani.

Pia, sio dawa zote au vifaa tiba zinazopatiwa msamaha.

''Biashara ya dawa na jinsi ya kushughulikia malipo na Iran imeendela kuwa ngumu, '' anasema Justine Walker, Mkurugenzi wa sera za vikwazo idara ya fedha ya Uingereza, inayowakilisha benki za Uingereza.

''Kisheria, dawa hazizuiliwi linapokuja suala la vikwazo. Hatahivyo, huzuiliwa

Dawa zinafika nchini Iran?

Dawa

Chanzo cha picha, Getty Images

Takwimu za Iran zilizobainika na BBC zinaonyesha kuwa dawa na vifaa tiba zilifika kiasi cha pauni milioni 145 sawa na dola milioni 176 mwezi septemba mwaka 2018, kisha zikaanza kuporomoka.

Mpaka mwezi Juni mwaka 2019 dawa zinazoingizwa zilishuka kwa asilimia 60 na kufikia dola milioni 67.

Kuporomoka huku haiwezekani sababu ikawa sababu ya vikwazo.

Pia kuna Data zinapatikana kutoka EU, mshirika muhimu wa kibiashara na Iran.

Tangu vikwazo vilipowekwa mwezi Novemba mwaka jana, mauzo kwenda Iran yalishuka kabla ya kupanda taratibu mwezi Mei.

Je ni hatari kufanya biashara na Iran?

''Kufuata kanuni mpya na kuingia gharama za ziada, kwa mfano kwa kubadilisha benki, hufanya biashara kati ya Iran na makampuni madogo ''kutisha'' anasema Esfandyar Batmanghelidj, mwanzilishi wa Bourse & Bazaar, ambayo inafuatilia uchumi wa Iran.

Ukosefu wa fedha za kigeni ndani ya Iran na ubadilikaji wa sarafu ya Irani pia hufanya uagizaji kuwa ghali zaidi.