Inked Sisterhood: Kipi huchangia kuchipuka kwa makundi ya waendesha pikipiki wanawake watupu?

Chanzo cha picha, Katie Cashman

Kundi la akina dada watupu waendesha pikipiki, wanaojiita the Inked Sisterhood, mara nyingi huwashangaza watu katika jamii nchini Kenya.


Chanzo cha picha, Katie Cashman

Kundi hilo hivi karibuni lilikamilisha safari ya 270km kutoka mji mkuu Nairobi, kuelekea kusini katika mji wa Loitokitok. Viatu vyao vya ngozi nyeusi, makoti na helmeti kichwanindio huwakinga katika barabara hatari yenye udongo mwekundu.
Baadhi ya wakaazi katika mji huo, ulio mpakani na Tanzania, walishangazwa, lakini wanawake hawa wamezoea watu kushangazwa nao.


Chanzo cha picha, Katie Cashman

Patience Mehta (juu), ni mkulima na msimamizi aliianzisha kundi la the Inked Sisterhood miaka miwili iliyopita kama njia ya kuwaunganisha na kuwapa nguvu wanawake wanaoendesha pikipiki. Lilitokana na shule ya mafunzo ya uendeshaji pikipiki Inked Bikers training school mjini Nairobi, ambako wanawake wengi walijifunza kuendesha na hivi sasa lina wafuasi 46.
Kundi hilo ni moja kati ya matano ya waendesha pikipiki wanawake watupu yaliochipuka katika miaka ya hivi karibuni yakiwemo pia Throttle Queens, Piki Dada and Heels of Steel.


Chanzo cha picha, Katie Cashman

Amepewa jina la utani "Empress Peanut" kutokana na umbo lake dogo na uongozi unaovutia, Bi Mehta alipata mshawasha wa kujifunza uendeshaji pikpiki baad aya kutazama filamu ya Nikita, ambayo nyota wake aliendesha pikipiki akiwa amevalia mavazi ya ngozi nyeusi.
Anaendesha pikipiki ya aina ya Hero Karizma ZMR 223cc - alioipa jina Babezy - anasema jina la kund lao lina maana ya ndani: "The ink ndio tunayoitumia kueleza hadithi yetu - na sio kuwa tuna michoro ya tatoo."


Chanzo cha picha, Katie Cashman

Pikipiki hutumika sana kwa usafiri mjini Nairobi. Boda boda zimejaa mjini lakini baadhiya watu hawavutiwi na tabia za baadhi ya maderevas na kuhofia usalama wao, wengine wakiwanyanyasa wanawake wakipita.
Licha ya kwamba ni kawaida kumuona mwanamke akiendesha pikipiki - wengi sasa wanaona manufaa ya kuvaa mavazi ya ngozi nyeusi na kupenya katikati ya msongamano wa mgarai mjini.


Chanzo cha picha, Katie Cashman

"Kwa muda mrefu majukumu ya wanaume yamekuwa wazi kutokana na kuchukuliwa kuwa hatari na wenye nguvu," anasema Bettina Bogonko.
Mhadhiri wa masomo ya matibabu anayemiliki pikipiki aina ya Lifan 250cc cruiser - aliyoipa jina Dragon - anasema: "Kilichoniepeleka barabarani kikamilifu na kwa kujiamini ni wakati babangu aliponipa baraka zake na kuniambia kuwa ninampa fahari kubwa."


Chanzo cha picha, Katie Cashman

Kabla ya kuanza kuendesha pikipiki mfanyakazi wa jamii Amanya Kuchio alikuwa akikaa saa tano au sita barabarani kila siku.
Baada ya kulifikiria, alimua kwamba yuko tayari kujitosa na anamiliki Hero Karizma ZMR 223cc - inayomsaidia kuokoa wakati barabarani na kupata muda zaidi na familia yake. "Inaniliwaza sana, ina gharama ndogo na napenda sana kupita kwa kasi barabarani na kuyapita magari yote. Zaidi ya hapo, umoja katika jamii ya waendesha pikipiki ni nzuri mno."


Chanzo cha picha, Katie Cashman

The Inked Sisterhood hukutana baada ya kila miezi michache na kuendesha pikipiki pamoja. Safari yao inayofuata ni ya 56km kuelekea mji mdogo wa Kimende, kaskazini mwa mji mkuu Nairobi.
wao hujumuika pamoja katika siku kuu kama siku ya kimataifa ya wanawake kuendesha pikipiki.


Chanzo cha picha, Katie Cashman

Wakili Doreen Murang'a anasema hana mambo makubwa maishani: "Lakini pikipiki yangu [ ZMR Hero Karizma] naipenda sana. Nimeipa jina na huwa nazungumza nayo inapokataa kuwaka."
Ni njia ya kukwepa mawazo: "Unapoiendesha ni lazima utulize akili barabarani, na sio kufikiria kazi iliosalia au machofu ya maisha. Ni wewe, barabara na upepo unaokupiga, na kama ni kama mimi ongezea muziki mwanana."


Chanzo cha picha, Katie Cashman

Wosia wake kwa wanawake wanaotaka kuendesha pikipiki : "Maisha yanaweza kumalizika muda wowote, kwahivyo uisitishwe kwa uoga . Ikiwa unataka kujifunza, kuna jamii inayokusubiri kujifunza na wewe, kukuwa na wewe na kuendesha na wewe pikipiki."


Chanzo cha picha, Katie Cashman

The Inked Sisterhood wanawaomba wanawake wajiunge nao ili nao wapate uhuru wao.
"Huitambui Nairobi unayoijua namna ilivyopangika kwa usafiri - kuanzia gharama, foleniu au msongamano wa magari au muda katika siku. Kuwana usafiri mwepesi kunakupa fursa ya kuutambua mji vizuri zaidi," anasema dada mmoja katika kundi hilo.
Picha: Katie Cashman, mpiga picha anayeishi Nairobi













