January Makamba: Waziri wa mazingira na Muungano Tanzania afutwa kazi na rais Magufuli

January Makamba

Chanzo cha picha, Makamba/Facebook

Muda wa kusoma: Dakika 2

January Makamba, aliyehudumu katika nafasi ya Waziri wa Mazingira na Muungano nchini Tanzania toka kuingia madarakani kwa Rais John Pombe Magufuli ametimuliwa kazi.

Taarifa ya Ikulu Tanzania haijaeleza sababu ya uteuzi wa Makamba kutenguliwa na nafasi yake sasa inachukuliwa na George Simbachawene.

Simbachawene anarejea kwenye baraza la mawaziri baada ya kujiuzulu uwaziri wa Nishati na Madini Septemba 2017 baada ya jina lake kutajwa kwenye kashfa ya kingia mkitaba ya madini iliyoitia hasara Tanzania.

Rais Magufuli pia amemteua Hussein Bashe, mbunge wa Nzega Mjini kushika nafasi ya Naibu Waziri wa Kilimo.

Kupitia mtandao wa Twitter, Makamba ameandika: "Ni kweli nimeyapokea mabadiliko yaliyofanywa kwa moyo mweupe kabisa kabisa. Nitasema zaidi siku zijazo." Huku akiambatanisha maneno hayo na picha yake na rais msaafu Ally Hassan Mwinyi wakiwa wanaangua kicheko.

Ruka X ujumbe, 1
Ruhusu maudhui? (Mitandao ya kijamii)

Mkala hii imebeba madhui yaliyotoka kwenye mitandao ya kijamii. Tunaomba ruhusa yako kabla kitu chochote hakija pakiwa, sababu wanaweza wakawa wanatumia Cookies na tekinolojia nyingine. Unaweza ukasoma sera sera ya kutumia cookies katika mitandao ya kijamii kabla ya kukubali. Kutazama maudhui haya chagua accept and continue

Onyo: Imetoka kwingine na inaweza kuwa na matangazo

Mwisho wa X ujumbe, 1

Pia Zitto Kabwe amkaribisha Makamba katika viti vya wabunge vya kawaida maarufu kiingereza 'back bench'

"Rafiki yangu @jmakamba karibu tena Backbench tuendelee na kazi. Ulikuwa Mbunge bora sana back bench 2010-2012 na ninaamini itakuwa hivyo tena 2019-2020. Umekuwa mmoja wa Mawaziri bora kabisa ambao umeonyesha tofauti ya KUTAWALA na KUONGOZA. Namna ulivyoongoza marufukuya mifuko ya Plastiki ilionyesha falsafa yako ya uongozi ni tofauti sana na falsafa ya Serikali yenu ya CCM. Tuna kesho nyingi tupambane kuijenga Tanzania inayojali watu wake na ya kidemokrasia."

Ruka Instagram ujumbe
Ruhusu maudhui? (Mitandao ya kijamii)

Mkala hii imebeba madhui yaliyotoka kwenye mitandao ya kijamii. Tunaomba ruhusa yako kabla kitu chochote hakija pakiwa, sababu wanaweza wakawa wanatumia Cookies na tekinolojia nyingine. Unaweza ukasoma sera sera ya kutumia cookies katika mitandao ya kijamii kabla ya kukubali. Kutazama maudhui haya chagua accept and continue

Onyo: Imetoka kwingine na inaweza kuwa na matangazo

Mwisho wa Instagram ujumbe

Bashe amshukuru Magufuli

Wakati huohuo Hussein Bashe amemshukuru Rais wa Tanzania, John Magufuli kwa kumteua kuwa naibu waziri wa kilimo huku akiahidi kwenda kutoa mawazo mapya ndani ya wizara hiyo inayochangia asilimia 28 ya pato la taifa (GDP).

Kulingana na gazeti la Mwanachi nchini Tanzania, Bashe ametoa kauli hiyo leo Jumapili alipokuwa akizungumza na chombo hicho cha habari kupita taarifa ya Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais Ikulu ya Tanzania ilipotoka na kuelezea uteuzi huo.

"Mimi niseme tu kwanza nimshukuru Rais kwa imani yake kwangu ambayo amenipa, kwa hiyo jukumu langu nimepewa

kwenda kumsaidia waziri (wa kilimo, Japhet Hasunga) kwenda kuhakikisha tunafikia malengo na matamanio ya Watanzania," amesema Bashe ambaye ni mbunge wa Nzega Mjini.

"Hii ndio sekta iliyoajili Watanzania wengi, inaendesha uchumi wa nchini inachangia 28 ya GDP na asilimia 70 ya ajira lakini ina changamoto nyingi, nina amini katika ushirikiano tutafanikiwa.

Ruka X ujumbe, 2
Ruhusu maudhui? (Mitandao ya kijamii)

Mkala hii imebeba madhui yaliyotoka kwenye mitandao ya kijamii. Tunaomba ruhusa yako kabla kitu chochote hakija pakiwa, sababu wanaweza wakawa wanatumia Cookies na tekinolojia nyingine. Unaweza ukasoma sera sera ya kutumia cookies katika mitandao ya kijamii kabla ya kukubali. Kutazama maudhui haya chagua accept and continue

Onyo: Imetoka kwingine na inaweza kuwa na matangazo

Mwisho wa X ujumbe, 2

"Katika taarifa hiyo ya uteuzi, Bashe anakwenda kuchukua nafasi iliyoachwa wazi na Innocent Bashungwa ambaye aliteuliwa kuwa waziri wa viwanda na biashara. Wakati huohuo Hussein Bashe amemshukuru Rais wa Tanzania, John Magufuli kwa kumteua kuwa naibu waziri wa kilimo huku akiahidi kwenda kutoa mawazo mapya ndani ya wizara hiyo inayochangia asilimia 28 ya pato la taifa (GDP).