Mafuriko ya India: Chui alazimika kusisinzia kwenye kitanda cha mkazi wa India

Chanzo cha picha, WTI
Chui jike ambaye alitoroka mbuga ya wanyama ya India iliyokumbwa na mafuriko katika jimbo Assam alipatikana akiwa amejituliza kwenye kitanda cha mkazi mmoja ndani ya nyumba.
Inaaminiw akuwa alitoroka kutoka mbuga ya wanyama ya Kaziranga , ambako wanyama 92 wamekufa sihu za hivi karibuni kutokana na mafuriko makubwa.
Maafisa kutoka hifadhi ya wamnyamapori walilazimika kwenda kwenye nyumba hiyo, ili kuiondoa ndani ya chumba cha kulala.
Aliongozwa kuelekea kwenye eneo la msitu la mbuga.
Kwa mujibu wa shirika la hifadhi ya wanyamapori nchini India (WTI), kwa mara ya kwanza chui huyo jike alionekana kwenye barabara kuu iliyopo karibu Alhamisi asubuhi, yapata kilomita 200 kutoka mbuga ya wanyama ya taifa.
Huenda alisumbuliwa na barabara yenye magari mengi na hivyo kuamua kutafuta maficho ndani ya nyumba ambayo , ilikuwa karibu na barabara kuui, alisema

Chanzo cha picha, WTI
Mwenye nyumba kwa jina Rathin Barman, ambaye aliongoza shughuli ya kumuondosha chui huyo kwenye kitanda chake , amesema kuwa chui huyo aliingia nyumbani kwake ambayo iko karibu na duka majira ya saa moja ujunu asubuhi halafu akasinzia kwa siku nzima.
"Alikuwa amechoka sana na alikuwa na siku ya usingiizi mtamu ,"aliiambia BBC.
Mmiliki wa nyumba ,Motilal, ambaye anamiliki pia msururu wa maduka , pia alitoroka kwake na familia alipomuona chui akiingia ndani ya nyumba.
"Jambo zuri zaidi ni kwamba hakuna mtu hata mmoja aliyetibua usinginzi wake kwa hiyo alilala fofofo . Katika eneo hili watu huwaheshimu sana wanyama ," Alisema Bwana Barman.
"[Motilal] anasema atatunza shuka lililokuwa kwenye kitanda pamoja na mti wake ili viwe kumbukumbu ya kutembelewa na chui ."
Maafisa wa shirika la hifadhi ya wanyamapori nchini India WTI waliitwa halafu wakaanza maandalizi ya kumuondosha kwa usalama kwenye makazi hayo.
Mkala hii imebeba madhui yaliyotoka kwenye mitandao ya kijamii. Tunaomba ruhusa yako kabla kitu chochote hakija pakiwa, sababu wanaweza wakawa wanatumia Cookies na tekinolojia nyingine. Unaweza ukasoma sera sera ya kutumia cookies katika mitandao ya kijamii kabla ya kukubali. Kutazama maudhui haya chagua accept and continue
Mwisho wa X ujumbe

Walizuwia magari kwenye barabara kuu kwa muda wa saa nzima na kuwasha vijinga vya moto ili kumuamsha chui huyo aliyelala fofofo. Hatimae aliondoka kwneye nyumba hiyo saa kumi na moja unusu jioni , akavuka barabara taratibu na kuelekea usawa wa msitu.
Bwana Barman alisema kuwa haikuwa wazi ikiwa aliingia msituni au "alikwenda katika maeneo mengine ".
Mbuga hiyo ya wanyamapori Kaziranga National Par ambayo inatambuliwa na shirika la Umoja wa mataifa la Unesco- inawahifadhi chui 110 ,lakini hakuna hata mmoja aliyefariki kutokana na mafuriko yanayoikumba mbuga hiyo.
Wanyama waliouawa katika mbuga hiyo kutokana na mafuriko ni pamoja na swala , ngili saba, nguruwe pori sita na ndovu mmoja.
Mafuriko ya mvua za masika yameathiri kwa kiasi kikubwa majimbo ya mashariki mwa India ya Bihar na Assam, na tayari yamewauwa watu zaidi ya 100 na kuwasambaratisha wengine mamilioni.
Msimu wa mvua ya masika ambao huanzia mwezi Juni hadi septemba pia umesababisha maafa katika maeneo ya Nepal na Bangladesh.












