Jeshi la Sudan lasaini makubaliano ya kugawana uongozi na upinzani

jeshi la Sudan na viongozi wa Upinzani

Chanzo cha picha, AFP

Maelezo ya picha, Kiongozi wa maandamano (kushoto), mkuu wa jeshi (kulia) walisaini makubaliano hayo

Jeshi la Sudan limesaini makubaliano ya kugawana uongozi na upinzani.

Baraza tawala la kijeshi na viongozi wa upinzani nchini Sudan, wamesaini makubaliano ya kugawanya uongozi baada ya mazungumzo ya usiku kucha kumaliza mzozo nchini humo.

Kumefanyika sherehe zilizomalizika hivi punde katika hoteli ya Corinthia katika mji mkuu wa Khartoum.

Makubaliano hayo yanatazamia miaka mitatu ya uongozi wa pamoja utakaofuatwa kwa uchaguzi mkuu.

Baada ya kusainiwa kwa makubaliano hayo, viongozi wa pande zote wamezungumzia kizazi kipya katika taifa ambalo limeshuhudia ghasia na maujai ya mamia ya waandamanaji tangu kutimuliwa kwa kiongozi aliyekuwepo Omar El Bashir mnamo April.

Katika makabiliano na jeshi yaliogeuka kuwa ghasia zilizosababihsa vifo vya watu , waandamanaji walitaka jeshilikabidhi madaraka kwa utawala wa kiraia.

Utiaji saini wa makubaliano hayo, unaonekana kuthibitisha makubaliano yalioidhinishwa kimsingi mapema mwezi huu.

Yanaeleza kwamba jeshi litakuwa uongozini kwa miezi 21 ya kwanza, na baada ya hapo utawala wa kiraia utaidhinishwa katika miezi 18 itakayofuata, na kufuatwa kwa uchaguzi mkuu.

Makubaliano ya pili kuhusu masuala ya katiba yanatarajiwa kukamilishwa Ijumaa wiki hii.