Iran yataka kuondolewa vikwazo kabla ya mazungumzo kuhusu mradi wa silaha za nyukilia

Chanzo cha picha, AFP/Getty
Iran imesema iko tayari kufanya majadiliano kuhusu mpango wa silaha za nyukilia na Marekani.
Msemaji wa Iran amesema suala la silaha ''linazungumzika bila masharti yeyote''.
Waziri wa mambo ya nje Mohammad Javad Zarif amesema mazungumzo kuhusu silaha yatafanyika ikiwa vikwazo vitaondolewa.
Marekani ilijiondoa kwenye mkataba wa nyukilia wa mwaka 2015 mwaka jana na kuiwekea vikwazo vikali dhidi ya Iran.
Katika kujibu hatua hiyo, Iran ilitangaza mwezi Julai kuwa imeongeza kiwango cha urutubishaji wa madini ya urani yaliyowekwa kwenye makubaliano hayo.Nchi hiyo imesisitiza kuwa haijaribu kutengeneza silaha za nyukilia.
Katika mahojiano ya televisheni siku ya Jumatatu, Bwana Zarif amesema kwenye televisheni ya NBC kuwa nafasi ya mazungumzo ipo wazi'' ikiwa Marekani itaondoa vikwazo.
Mkala hii imebeba madhui yaliyotoka kwenye mitandao ya kijamii. Tunaomba ruhusa yako kabla kitu chochote hakija pakiwa, sababu wanaweza wakawa wanatumia Cookies na tekinolojia nyingine. Unaweza ukasoma sera sera ya kutumia cookies katika mitandao ya kijamii kabla ya kukubali. Kutazama maudhui haya chagua accept and continue
Mwisho wa X ujumbe
Raisi wa Marekani Donald Trump amesema Marekani ''imepiga hatua'' na Iran na kuwa hawakuwa ''wakitafuta kuubadili utawala'', ingawa alisisitiza kuwa nchi haiwezi kutengeneza silaha za nyukilia na haiwezi kujaribu makombora ya masafa marefu.
Kwanini Iran imeongeza viwango vya urutubishaji?
Mapema mwezi Mei, Trump aliweka shinikizo zaidi kwa Iran kwa kuidhinisha upya marufuku kwa matiafa yanayonunua mafuta kutoka kwa Iran.
Hatua hiyo ilinuiwa kusitisha kipato kikuu kwa serikali ya Iran.
Rais wa Iran Hassan Rouhani alitangaza kuwa nchi yake inarudi nyuma katika ahadi zake katika makubaliano hayo.
Hii ikiwa ni pamoja na kutotiii sheria kuhusu akiba yake ya urutubishaji mdogo wa madini ya Uranium kiwango kilichowekwa kikwa ni - 300kg na tani 130 - na kusitisha uuzaji wa akiba ya ziada katika mataifa ya nje.
Rouhani pia aliyapatia mataifa hayo ya Ulaya siku 60 kulinda mauzo ya mafuta ya Iran. Iwapo yatashindwa kufanya hivyo , Iran itakiuka masharti ya urutubishaji Uranium na kusitisha uundwaji upya wa kinu cha Arak, ambacho mafuta yake yaliotumika yana plutonium yalio na uwezo wa kuunda mabomu.
Mkataba wa nyukilia bado unafanya kazi?
Trump alijiondoa kwenye mkataba mwezi Mei mwaka 2018.Amedai kuwa Iran haijachukua hatua zaidi kukomesha mradi wa nyukilia. Akitaka kuwepo kwa makubaliano mapya ambayo yatadhibiti mradi huo.
Iran imekataa kuzungumzia mabadiliko yeyote, na imetishia kuimarisha hatua hii ya kuvunja makubaliano ikiwa Ulaya haitasaidia kudhibiti madhara ya vikwazo vya Marekani.

Chanzo cha picha, EPA












