Tuzo kwa Hodan Nalayeh: Somalia kumuenzi mwandishi aliyeuawa na al-Shabab

Hodan Nalayeh
Maelezo ya picha, Hodan Nalayeh alihamia Kismayo mwaka jana
Muda wa kusoma: Dakika 1

Serikali ya Somalia imetangaza kuwa itatoa tuzo ya kwa heshima ya mwanahabari Hodan Nalayeh aliyeuawa katika shambulio la kigaidi nchini humo wiki iliyopita.

Tuzo ya kila mwaka ya Hodan Nalayeh itapewa mtu ''aliyenawiri'' kwa kazi yake miongoni mwa wasomali wanaoishi nje ya nchi.

Nalayeh, ambaye aalikulia Canada, alirekea nchini Somalia mwaka jana kuangazia taarifa za ufanisi katika nchi aliozaliwa.

Alikua miongoni mwa watu 26 waliouawa na wanamgambo wa al-Shabab mjini Kismayo Ijumaa iliyopita.

Nalayeh, amabye alikua na ujauzito wa miezi tisa aliuawa pamoja na mume wake baada ya watu waliojihami kwa silaha kuvamia hoteli ambayo ilikuwa na wanasiasa wa jimbo moja nchini humo walikuwa wakijadiliana kuhusu masuala ya uchaguzi.

Nalayeh alisifiwa kwa kuangazia masuala mengingeni kuhusu Somalia kando na vita vya wenyewe kwa wenyewe, ugaidi na ukame.

Azma yake ya kuangazia taarifa ya sura mpya ya ufanisi wa Somalia uliwafanya vijana wa taifa hilo wanaoishi katika mataifa mengine duniani kusaidia katika mikakati ya kujenga upya taifa hilo.

Kifo chake kilipokelewa kwa majonzi makubwa.

Kwa heshima ya maisha yake ya "kutia moyo" Wizara ya mambo yanje ya Somalia "itamtambua mtu anayeishi nje ya Somalia atakayefanya jambo la kipekee litakalochangia ufanisi wa taifa hili", ilisema taarifa iliyochapishwa katika mtandao wa Twitter.

Ruka X ujumbe
Ruhusu maudhui? (Mitandao ya kijamii)

Mkala hii imebeba madhui yaliyotoka kwenye mitandao ya kijamii. Tunaomba ruhusa yako kabla kitu chochote hakija pakiwa, sababu wanaweza wakawa wanatumia Cookies na tekinolojia nyingine. Unaweza ukasoma sera sera ya kutumia cookies katika mitandao ya kijamii kabla ya kukubali. Kutazama maudhui haya chagua accept and continue

Onyo: Imetoka kwingine na inaweza kuwa na matangazo

Mwisho wa X ujumbe