Kwanini picha ya mwanasiasa huyu na Malala Yousafzai inashutumiwa?

Waziri wa elimu Quebec anashutumiwa kwa kuweka picha na mwanaharakati anayetetea elimu Malala Yousafzai.

Mshindi huyo wa tuzo ya Nobel ya amani anayevaa mtandio kichwani hangeweza kutoa mafunzo katika jimbo hilo la Canada.

Quebec hivi karibuni ilipitisha sheria yenye mzozo inayowazuia baadhi ya wafanyakazi wa serikali, wakiwemo walimu kutovaa mavazi yoyote ya kidini kazini.

Jean-François Roberge amesema alijadiliana na Bi Malala masuala ya elimu na maendeleo ya kimataifa.

Alipigwa risasi kichwani na wanamgambo wa Taliban mnamo 2012 kwa kusubutu kwenda shuleni na tangu hapo ametambuliwa kimataifa kwa kazi zake katika kampeni ya kushinikiza elimu kwa wasichana.

Mnamo Juni, Quebec ilipitisha sheria inayozuia wafanyakazi wa serikali walio katika nafasi za usimamizi kutovaa mavazi ya kidini kama vile vilemba au hijab wakiwa kazini.

Sheria hiyo (CAQ) inawalenga majaji, maafisa wa polisi, walimu na wafanyakazi wa umma.

Mswada huo ulizusha maandamano na mjadala mkubwa katika jimbo hilo.

wafuasi wanasema sheria hiyo ni hatua muhimu kuelekea kujumuishwa kutenganishwa kwa kanisa na serikali ya jimbo la Quebec.

Licha ya kwamba sheria hiyo haikutaja dini yoyote maalum, wakosoaji wanalalamika kwamba inabagua na wanasema inawalenga wanawake wa kiislamu katika jimbo hilo wanaovaa hijab au vitambaa vingine vya kichwani.

baadhi ywa wadadisi katika mitandao ya kijamii wamemtaja waziri huyo kuwa ni mnafiki kwa kupiga picha na Bi Yousafzai.

Roberge, aliyekutana na Yousafzai akiwa Ufaransa, alitetea sheria hiyo alipoulizwa kwenye Twitter na mwandishi Salim Nadim Valji namna ambavyo angejibu iwapo Bi Yousafzai atake kuwa mwalimu Quebec.

"Bila shaka ningemwambia kwamba ingekuwa heshima kubwa na kwamba hukuQuebec, kama ilivyo Ufaransa na katik amatifa mengine ya wazi yalio na waumini tofauti, walimu hawawezi kuvaa mavazi ya kidini wakati wakiwa kazini," alisema.