Marekani: Mwanamke mjamzito ashitakiwa kifo cha mwanawe aliyeuawa kwa kupigwa risasi akiwa tumboni

Mugshot of Marshae Jones

Chanzo cha picha, Reuters

Maelezo ya picha, Mwanamke mjamzito ashitakiwa kifo cha mwanawe aliyeuawa kwa kupigwa risasi akiwa tumboni
Muda wa kusoma: Dakika 2

Mwanamke wa miaka 27 kutoka jimbo la Alabama, nchini Marekani ameshitakiwa kwa kuua bila kukusudia baada ya kupoteza ujauzito katika kisa cha ufyetulianaji risasi.

Marshae Jones alikamatwa siku ya Jumatano kwa kuhusika katika mzozo uliosababisha apigwe risasi ya tumbo, vyombo vya habari vinaripoti.

Mashataka dhidi ya Ebony Jemison aliyempiga risasi yalifutwa na mahakama kwa mdai kuwa alifanya hivyo kujilinda.

Makundi ya kutetea haki yanasema kuwa hatua hiyo inaonesha kuwa sheria mpya za jimbo hilo zinazodhibiti uavyaji mimba zitaathiri kesi zingine.

Bi Jones alipigana na Ebony Jemison mwenye umri wa miaka 23, tarehe 4mwezi Desemba mwaka jana, akiwa na ujauzito wa miezi mitano, kwa mujibu wa AL.com.

Ruka X ujumbe
Ruhusu maudhui? (Mitandao ya kijamii)

Mkala hii imebeba madhui yaliyotoka kwenye mitandao ya kijamii. Tunaomba ruhusa yako kabla kitu chochote hakija pakiwa, sababu wanaweza wakawa wanatumia Cookies na tekinolojia nyingine. Unaweza ukasoma sera sera ya kutumia cookies katika mitandao ya kijamii kabla ya kukubali. Kutazama maudhui haya chagua accept and continue

Onyo: Imetoka kwingine na inaweza kuwa na matangazo

Mwisho wa X ujumbe

Presentational white space

Kwa mujibui wa polisi, mabishano yalizuka kuhusu baba ya mtoto ambaye hajazaliwa, hali iliyomfanya Bi Jemison kumpiga risasi Bi Jones na kumfanya ampoteze ujauzito wake.

Polisi wanasema kwa kukuwa inadaiwa Bi Jones ndiye aliyeanzisha ugomvi uliohatarisha maisha mtoto wake ambaye hajazaliwa hakuwa na budi kufunguliwa mashtaka hayo.

Polisi pia wa walidai kuwa Bi Jemison alilazimika kujilinda dhidi ya Bi Jones.

Mkuu wa polisi wa jimbo hilo Lt Danny Reid wakati huo(Disemba) alisema: "Mhasiriwa pekee wa kweli katika kisa hicho alikuwa mtoto ambaye hajazaliwa. Ni mama yaake mtoto ambaye alianzisha ugomvi ambao ulisababisha kifo cha mtoto wake ambaye hajazaliwa."

Lt Reid aliongeza kuwa mtoto huyo "Lihusishwa katika ugomvi huo wakati alikuwa anategemea ulinzi kutoka kwa mama yake".

Mahakama ya Jefferson County Courthouse, Alabama

Chanzo cha picha, Google Maps

Maelezo ya picha, Bi Jones ameshitakiwa katika mahakama ya Jefferson County, Alabama

Siku ya Jumatano, Bi Jones alikamatwa na kushitakiwa kwa kuua bila kukusudia na kuwekwa mahabusu katika jela ya Jefferson County na hatimae kuachiliwa kwa dhamana ya dola 50,000 sawa na (£40,000)

Bi Jemison amesema kuwa hatua hiyo si ya haki.

"Nadhani hakustahili kushitakiwa kwa kosa la kuua bila kukusudia kwasababu hakumuua mwenyewe mtoto," aliiambia gazeti la Buzzfeed.

"Lakini alngelishitakiwa na kosa la kuhatarisha maisha ya mtoto au kusababisha vurugu."

Makundi ya kutetea haki yalaani hatua hiyo

Wanaharakati wa kutetea haki za wanawake na ambao wanaungamkono wanawake kujiamulia kama wanataka kulea mimba au kutoa wamelaani hatua ya jimbno hilo kumfungulia mashtaka Bi Jones - hali iliyoibua gumzo kuhusu sheria mpya ya jimbo hilo inayoharamisha uavyaji mimba pamoja na hatua zingine za kishera ambazo huenda zikaathiri kesi zisizohusiana na utoaji mimba.

Haijabainiki ni vipi sheria inayoharamisha utoaji mimba ilivyotumika katika kesi inayomkabili Bi Jones.

Polisi wa Pleasant Grove na ofisi ya mahakama ya wilaya ya Jefferson County haijatoa tamko lolote kwa BBC licha ya kuombwa kujibu madai hayo.

Maelezo ya video, Suala la utoaji mimba laelezewa kwa dakika tatu

Shirika la Yellowhammer linayofadhili makundi yanayotetea haki ya wanawake kujiamulia kama wanataka kuzaa au la, linasisitiza kuwa Bi Jones anahitaji kuwakilishwa kisheria.

Amanda Reyes, afisa mkuu mtendaji wa shiirika hilo,amesema katika taarifa yake kuwa: "Leo, Marshae Jones anashitakiwa kwa kuua bila kukusudia kwa kuwa mjamzito na kupigwa risasi akijibizana na mtu aliyekuwa na bunduka.

"Kesho itakuwa, mwanamke mwingine mweusi, pengine kwa kunywa pombe akiwa mjamzito. Na baada ya hapo, mwingine atashambuliwa kwa kutoenda kliniki kama inavyotakiwa."