Wanawake wawili wadai mwandishi E. Jean Carroll aliwaeleza kuwa Trump alimbaka

Bi Carroll, mwenye umri wa miaka 75, ni mwanamke wa 16 kumshutumu Bwana Trump kwa tabia isiyofaa ya kingono

Chanzo cha picha, REUTERS AND GETTY

Maelezo ya picha, Bi Carroll, mwenye umri wa miaka 75, ni mwanamke wa 16 kumshutumu Bwana Trump kwa tabia isiyofaa ya kingono

Wanawake wawili wamesema wazi kuwa mwandishi wa E. Jean Carroll aliwatobolea siri baada ya Donald Trump kudaiwa kumbaka katika miaka ya 1990

Carol Martin na Lisa Birnbach wakati mwingine hawakubaliani juu ya ikiwa Bi Carroll angepaswa kuwaita polisi, imeeleza taarifa ya gazeti la New York Times.

Rais Trump anakana tuhuma hizo, akisema Bi Carroll "ni muongo kabisa" na "sio taipu yake ".

Bi Carroll, mwenye umri wa miaka 75, ni mwanamke wa 16 kumshutumu Bwana Trump kwa tabia isiyofaa ya kingono.

Bi Martin na Bi Birnbach walisema nini?

Bi Martin, ambaye alikuwa mtangazaji wa TV kati ya mwaka 1975-95,na Bi Birnbach, mwandishi , waliongea hadharani kwa mara ya kwanza kuhusu madai ya unyanyasaji wa kingono katika kipindi cha podcast cha gazeti la New York Times.

Bi Carroll, mwandishi wa ukurasa wa Elle, alisema kuwa katika kipindi hicho cha said in podcast alimuita Bi Birnbach mara moja baada ya madai ya kubakwa, akimwambia kuwa Bwana Trump alimlazimisha kufanya ngono.

Bi Birnbach alijibu kwa kusema kuwa alidhani kuwa ulikuwa ni ubakaji, akamtaka Bi Carroll awapigie simu polisi.

"Hebu twende polisi . Nitakupeleka polisi " Alisema Bi Birnbach , lakini akaongeza kuwa rafiki yake alikataa.

Bi Carroll alielezea kile kilichotokea baina yake na Trump kama "mapigano", si "uhalifu ".

Jessica Leeds, pia alidai kuwa alimtomasa walipokutana kwenye ndege katika miaka ya 1980

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Jessica Leeds, pia alidai kuwa alimtomasa walipokutana kwenye ndege katika miaka ya 1980

Pia alikiambia kipindi cha podcast cha New York Tomes kuwa anahisi kuwa alichangia kushawishi mienendo yta Bwana Trump. Alipoulizwa ikiwa anahisi kuwajibika na kile kilichotokea, alisema: "Kwa asilimia miamoja ."Bi Carroll alisema kuwa siku mbili au tatu baadae alimwambia pia Bi Martin kuhusu unyanyasaji huo.

Bi Martin alimshauri asiwaite polisi, akisema kuwa Trump ni mtu mwanaume maarufu mwenye uwezo mkubwa na mawakili wengi.

"Nilisema: Usimwambie yeyote. Nisingependa kumwambia mtu yeyote kuhusu hili," Bi Martin alinukuliwa akisema katika podcast.

Unyanyasaji unaodaiwa ulifanyika wapi?

E. Jean Carroll anasema ulitokea katika duka la Bergdorf Goodman katika eneo la Manhattan mjini New York mwishoni mwa mwaka 1995 au mwanzoni mwa mwaka 1996, wakati wawili hao walipokutana katika duka hilo kununua bidhaa.

Inadaiwa kuwa Trump ambaye wakati huo alikuwa mmiliki wa nyumba za kuishi anadaiwa kumuomba ushauri wake alipokuwa akinunua nguo ya ndani ya mwanamke mwingine na akamtania akimuomba kumuonyesha inavyovaliwa.

Lakini walipofika katika chumba cha kupimia nguo, alisema Trump alimsukuma kwneye ukutana kumbaka.

Ni Carroll, ambaye ushauri wa " E. Jean" umeonekana katika jarida la Elle tangu 1993, anasema aliweza kumsukuma baada ya "kutumia nguvu".

Bi Carroll alitoa madai hayo kwa mara ya kwanza katika jarida la New York Ijumaa iliyopita .Alisema kuwa ataangalia uwezekano wa kushinikiza mashtaka dhidi ya rais Trump.

Trump alijibu vipi shutuma dhidi yake?

Akizungumza Jumatatu, Bwana Trump alipuuzilia mbali madai hayo ambayo yanakaribia kuonekana katika kitabu kijacho cha Carroll , kiitwacho -What Do We Need Men For? A Modest Proposal.

Alisema kuwa hata hamfahamu kabisa Bi Carroll,pamoja na kwamba walionekana kwenye picha pamoja katika jarida la New York sambamba na madai ya shutuma zake.

"Ni mtu tu - Ni jambo baya sana kwamba watu wanaweza kutoa kauli kama hizo ," alisema.

Ilikuwa ni mara ya tatu kukana madai hayo tangu Bi Carroll ayaeleze wazi kwa umma huku awali Bwana Trump alimshutumu kwa "kujaribu kuuza kitabu chake " na "kubuni taarifa".

Mnamo mwaka 2016, Bwana Trump alitoa kauli kama hizo juu ya mwanamke mwingine aliyemshutumu kwa , Jessica Leeds, ambaye alidai kuwa alimtomasa walipokutana kwenye ndege katika miaka ya 1980.