Ubalozi wa Marekani Tanzania watahadharisha Dar es Salaam kushambuliwa

HABARI ZA HIVI PUNDE

Ubalozi wa Marekani nchini Tanzania umetoa tahadhari kuwa kuna fununu za mipango ya mashambulizi jijini Dar es Salaam.

Kwa mujibu wa tahadhari hiyo iliyochapishwa kwenye kurasa rasmi za mitandao ya kijamii ya Ubalozi huo, eneo la Masaki ndilo linalolengwa.

Eneo hilo lililopo kwenye rasi ya Msasani ni moja ya maeneo ya makazi ya kigahari zaidi jijini humo.

Tahadhari hiyo inabainisha kuwa, maeneo yanayolengwa ni mahoteli na migahawa ambayo hutembelewa na watalii ikiwemo eneo maarufu la maduka ya Slipway.

"Ubalozi hauna ushahidi wa moja kwa moja wa tishio hilo ama taarifa za muda gani mashambulizi yatatokea, hata hivyo unawaonya wananchi kuchukua tahadhari."

Tutaendelea kukujuza zaidi kadri tutakavyokwa tunapokea taarifa juu ya tahadhari hiyo.