Mbunge adai alijilinda dhidi ya ubaguzi kwa kumpiga mwanamme A. Kusini

Mbunge Bi van Damme ametishia kupeleka mashtaka kwa polisi

Chanzo cha picha, AFP

Maelezo ya picha, Mbunge Bi van Damme ametishia kupeleka mashtaka kwa polisi
Muda wa kusoma: Dakika 2

Mbunge mweusi wa Afrika Kusini amejitetea kuwa alimpiga ngumi mbunge mwanamume baada ya kudaiwa kumtusi matusi ya ubaguzi wa rangi.

Phumzile van Damme kutoka chama cha upinzani cha Democratic Alliance amesema kuwa alijipata katika mzozo na mwanamke mzungu katika mji wa V&A Waterfront uliopo Cape wakati mwanamme mzungu alipotishia kuleta ghasia na kutumia lugha chafu alipokuwa akimuongelesha akimtaja kama "wewe mweusi".

Mji wa V&A Waterfront, ambao ni kitovu kikuu cha utalii, umeomba radhi kwa tukio hilo.

Bi van Damme hakufurahia namna alivyotendewa na afisa wa usalama alipo ripoti kwake tukio.

" Tunasikitishwa na tukio hili, ambalo hatukulishighulikia kwa malengo muhimu ,kwa heshima na huruma ," ulieleza mji wa kitalii wa V&A Waterfront kwenye ukurasa wake waTwitter.

Bi van Damme amesema kuwa alikuwa amesimama kwenye mstari katika duka la bidhaa mbalimbali alipolazimika kuzoza na mwanamke ambaye anadaiwa kumwambia kuwa " atamsukuma kando".

"Halafu nilipokwenda nje, alikuwa amesimama pale na familia yake katika hali ya kunitisha. Na ndipo nilipomsogelea na kumwambia, 'kwanini unaniangalia hivyo kwa kunitisha?' Halafu akasema, 'ni kwasababu wewe ni mweusi', Alisema van Damme katika video aliyoiweka kwenye ukurasa wake wa Twitter.

Alisema kuwa manamme, ambaye alikuwa na mwanamke, "alikuwa natishi kuzua ghasia, kwa hiyo katika hali ya kujilinda nilimpiga ngumi kwenye kichwa chake".

Bi van Damme amesema kuwa anakubali kutoa msamaha kwa V&A Waterfront na jukumu lao la kutovumilia tabia na mienendo isiyokubalika inayofanywa na wafanyakazi wake.

Amesema, hata hivyo ametishia kupeleka mashtaka kwa polisi.

Ruka X ujumbe
Ruhusu maudhui? (Mitandao ya kijamii)

Mkala hii imebeba madhui yaliyotoka kwenye mitandao ya kijamii. Tunaomba ruhusa yako kabla kitu chochote hakija pakiwa, sababu wanaweza wakawa wanatumia Cookies na tekinolojia nyingine. Unaweza ukasoma sera sera ya kutumia cookies katika mitandao ya kijamii kabla ya kukubali. Kutazama maudhui haya chagua accept and continue

Onyo: Imetoka kwingine na inaweza kuwa na matangazo

Mwisho wa X ujumbe

Visa vya ubaguzi wa rangi vimekuwa vikiendelea kugonga vichwa vya habari nchini Afrika Kusini.

Matamshi na mashambulio ya mwili ni miongoni mwa matukio ambayo yamekuwa yakiripotiwa licha ya kipindi cha ubaguzi wa rangi kuripotiwa kumalizika baada ya aliyekuwa rais wa nchi hiyo Hayati Nelson Mandela kuchukua mamlaka 1994.

Mwandishi wa habari wa Afrika Kusini Samora Mangesi alituma picha zake za majeraha aliyoyapata katika kile alichodai ni shambulio Mwaka jana

Chanzo cha picha, Samora Mangesi/Tweete

Maelezo ya picha, Mwandishi wa habari wa Afrika Kusini Samora Mangesi alituma picha zake za majeraha aliyoyapata katika kile alichodai ni shambulio Mwaka jana

Moja ya matukio hayo ni kupigwa kwa mtangazaji wa Televisheni na redio nchini Afrika Kusini mweusi ambaye alisema kuwa alikuwa muathiriwa wa shambulio lililochochewa na ubaguzi wa rangi baada ya kusimamisha gari lake kwa ajili ya kulisaidia kundi la wazungu ambao gari lao lilikuwa limepinduka.

Samora Mangesi alituma picha zake za majeraha aliyoyapata katika kile alichodai ni shambulio Mwaka jana.

Yeye na marafiki zake wawili wa kike waliitwa "nyani", alisema. Walipoulizwa ni kwanini wanatukanwa, walipigwa hadi wakapoteza fahamu. Alisema.

Taarifa juu ya shambulio hilo zilizua hasira miongoni mwa watumiaji wa mitandao ya kijamii.