Afcon 2019: Je Kenya na Tanzania zitawashangaza wapinzani wao Senegal na Algeria?

Chanzo cha picha, TFF/Twitter
Hatimaye siku imefika, mechi za kufungua dimba za Kundi C lenye mataifa makubwa mawili ya Afrika Mashariki, Tanzania na Kenya zinachezwa leo.
Mwaka huu Afrika Mashariki ina timu nne, pamoja na Uganda ambayo imepata ushindi wake wa kwanza kwenye michuano ya Afcon kwa kuilaza DRC 2-0.
Burundi wao wanashiriki kwa mara ya kwanza na wamepoteza mchezo wa kwanza dhidi ya miamba Nigeria kwa goli moja bila majibu.
Tukirudi kwenye kundi C wapinzani wa Kenya na Tanzania ni Senegal na Algeria, ambao wawili hao wakipigiwa upatu kusonga mbele.
Timu ya Algeria ilishinda taji hilo 1990 wakati walipokuwa wenyeji wa michuano hiyo ambapo wakati huo ni timu nane pekee zilizoshiriki huku Senegal ikikaribia kushinda taji hilo 2002 baada ya kulazwa kwa njia ya mikwaju ya penalti na Cameroon katika fainali.
Timu zote zinajigamba kumiliki nyota wa Ligi ya Uingereza na ligi nyengine mbali mbali za barani Ulaya wakiwemo Sadio Mane wa Liverpool na Riyad Mahrez kutoka mabingwa wa ligi Man City ya Uingereza ambaye ni kiungo muhimu wa Algeria.
Kenya kwa mara ya kwanza tangu 2004 na Tanzania kwa mara ya kwanza tangu 1980 zimerudi katika michuano hiyo lakini wachambuzi hawazipi nafasi kusonga mbele zaidi ya raundi ya kwanza.
Hii leo, Tanzania itaanza kupambana na Senegal huku Kenya ikiminyana na Algeria.
Je, Afrika Mashariki itachekelea tena na leo kama ilivyokuwa jana kwa Uganda dhidi ya DRC?
Yote yanawezekana, mwaka 2002 kwenye michuano ya Kombe la Dunia, Senegal ikionekana kama timu changa, iliwafunga wakoloni wao wa zamani Ufaransa ambao walikuwa ni mabingwa watetezi.
Senegal ilienda mpaka hatua ya robo fainali ambapo waling'olewa kwa goli la dhahabu na Uturuki.
Kitengo cha habari cha shirika la habari la AFP kiliziangazia timu hizo nne katika kundi ambalo huenda Senegal na Algeria zikapigania nafasi ya kwanza na ya pili huku Kenya na Tanzania zikimaliza wa tatu na nne.
ALGERIA-Mbweha wa jangwani
Algeria haina mafanikio ya haja katika kombe hilo , ikitinga fainali mara mbili katika majaribio 17 na kufanikiwa kushinda mara moja wakati walipopata nafasi ya kuandaa michuano hiyo.
Baada ya kikosi cha timu hiyo kutangazwa, kocha Djamel Belmadi alimuondoa mchezaji Haris Belkebla kwa kuonyesha makalio yake wakati wa mechi ya moja kwa moja iliokuwa ikionyeshwa katika mitandao ya kijamii.
Mkala hii imebeba madhui yaliyotoka kwenye mitandao ya kijamii. Tunaomba ruhusa yako kabla kitu chochote hakija pakiwa, sababu wanaweza wakawa wanatumia Cookies na tekinolojia nyingine. Unaweza ukasoma sera sera ya kutumia cookies katika mitandao ya kijamii kabla ya kukubali. Kutazama maudhui haya chagua accept and continue
Mwisho wa X ujumbe, 1
Nafasi yake imechukuliwa na Andy Delort, mmoja ya wachezaji wake waliozaliwa Ufaransa akiwa na mizizi ya Algeria ambaye aliamua kuwachezea Mbweha hao wa Jangwani.
Ni karibia muongo mmoja tangu Algeria iliposikika, ikifika nusu fainali ya michunao ya mwaka 2010 na hali ya hewa ya eneo la Afrika kaskazini huenda ikakisadia kikosi chake kufika mbali.
KENYA-Harambee Stars
Kiungo mkabaji wa Tottenham Victor Wanyama ameondoa presha iliokuwa inakikabili kikosi cha Harambee Stars kwa kusema kuwa ''hawana kiwango cha lengo lao Misri'.
Iwapo anazungumza ukweli ama kujaribu kuwaweka wapinzani wake katika hali ya switafahamu ni kitu ambacho kinahitaji mjadala, lakini Kenya ina rekodi mbaya huku wakitolewa katika raundi ya kwanza mara zote tano walizoshiriki katika kinyang'anyiro hicho.
''Ni lazima tutie bidii katika kila mechi na kuhakikisha kuwa tunapata pointi'', alisema Wanyama, lakini kusema ni rahisi zaidi ya kutenda.
Mkala hii imebeba madhui yaliyotoka kwenye mitandao ya kijamii. Tunaomba ruhusa yako kabla kitu chochote hakija pakiwa, sababu wanaweza wakawa wanatumia Cookies na tekinolojia nyingine. Unaweza ukasoma sera sera ya kutumia cookies katika mitandao ya kijamii kabla ya kukubali. Kutazama maudhui haya chagua accept and continue
Mwisho wa X ujumbe, 2
Huku wengi wakitarajia kwamba Harambee Stars huenda ikalazwa na Algeria pamoja na Senegal, mechi kati yake na majirani zake Tanzania ndio itakayokuwa na ushindani mkubwa huku timu zote mbili zikijaribu kutia guu katika raundi ya 16 bora.
SENEGAL-Simba wa Teranga
Wachanganuzi wengi wa soka waliipigia upatu Senegal kusonga mbele hadi fainali 2017, lakini walipoteza katika mikwaju ya penalti kwa waliotawazwa washindi Cameroon huku Mane akilia baada ya mkwaju wake kutoka nje.
Kikosi cha Simba hao wa Teranga, kinachoongozwa na Mane na nyota wa Napoli Kalidou Koulibaly, kinaonekana kuwa na uwezo mkubwa baada ya kushiriki katika kombe la dunia nchini Urusi.
Mkala hii imebeba madhui yaliyotoka kwenye mitandao ya kijamii. Tunaomba ruhusa yako kabla kitu chochote hakija pakiwa, sababu wanaweza wakawa wanatumia Cookies na tekinolojia nyingine. Unaweza ukasoma sera sera ya kutumia cookies katika mitandao ya kijamii kabla ya kukubali. Kutazama maudhui haya chagua accept and continue
Mwisho wa X ujumbe, 3
Wakati kocha wake na aliyekuwa mchezaji wa zamani Aliou Cisse alipopatiwa kandarasi mpya aliambiwa kushinda kombe la Afcon 2019 la sivyo atakiona cha mtema kuni.
Cisse ana kikosi chenye uwezo wa kutawala bara Africa lakini hakuna hakikisho kwamba wataibuka washindi wa kombe hilo huku Misri, Morocco na Nigeria zikiwa na matumaini kama hayo.
TANZANIA-Taifa Stars
Ilijihakikishia kushiriki katika michuano hiyo ya Misri baada ya kuilaza Uganda ambayo tayari ilikuwa imefuzu kwa magoli matatu na kushindwa kwa Lesotho kupata ushindi Cape Verde.
Mkufunzi Emmanuel Amunike ana uelewa wa kombe la Africa baada ya kuiwakilisha Nigeria katika kikosi ambacho kiliishinda Zambia katika fainali za 1994 zilizoandliwa Tunisia.
Yeye haiogopi Senegal wala Algeria, akisema: Timu zinazotajwa kuwa ndogo zinaelekea Misri ili kubadilisha mawazo ya wengi.
Mkala hii imebeba madhui yaliyotoka kwenye mitandao ya kijamii. Tunaomba ruhusa yako kabla kitu chochote hakija pakiwa, sababu wanaweza wakawa wanatumia Cookies na tekinolojia nyingine. Unaweza ukasoma sera sera ya kutumia cookies katika mitandao ya kijamii kabla ya kukubali. Kutazama maudhui haya chagua accept and continue
Mwisho wa X ujumbe, 4
Lakini bila Mane au Mahrez , Taifa Stars wanatarajiwa kujibidiisha na iwapo watafuzu miongoni mwa timu 16 bora basi watakuwa wamefaulu pakubwa.
Timu hiyo inatumai kwamba itailaza Kenya ili kushinda nafasi ya tatu bora.