Bajeti 2019: Kwanini wabunge wanawake walisusia kwa muda hotuba ya bajeti Kenya

Bunge la Kenya

Chanzo cha picha, Nation Media Twitter

Muda wa kusoma: Dakika 2

Wabunge wanawake nchini Kenya wamesusia kikao cha kusomwa kwa bajeti kulalamikia hatua ya mwenzao kudaiwa kushambuliwa katika majengo ya Bunge na mbunge wa kiume.

Wabunge hao walitaka mbunge wa Wajir Mashariki Rashid Amin kukamatwa kwa kumpiga mbunge mwakilishi wa wanawake wa jimbo la Wajir Fatuma Gedi.

Tukio hilo lilijiri wakati bunge liliporejelea kikao cha mchana cha usomaji wa bajeti.

Wabunge hao walisikika wakiimba nyimbo za kumtaka mbunge Rashid na kiongozi wa wengi bungeni kujiuzulu Aden Duale.

Wanawake hao walimlaumu Duale kwa kushindwa kuwatetea viongozi wanawake bungeni.

Ruka X ujumbe, 1
Ruhusu maudhui? (Mitandao ya kijamii)

Mkala hii imebeba madhui yaliyotoka kwenye mitandao ya kijamii. Tunaomba ruhusa yako kabla kitu chochote hakija pakiwa, sababu wanaweza wakawa wanatumia Cookies na tekinolojia nyingine. Unaweza ukasoma sera sera ya kutumia cookies katika mitandao ya kijamii kabla ya kukubali. Kutazama maudhui haya chagua accept and continue

Onyo: Imetoka kwingine na inaweza kuwa na matangazo

Mwisho wa X ujumbe, 1

Spika wa Bunge la Kenya, Justin Muturi, alilazimika kuwaita maafisa wa ulinzi wa Bunge kuwatoa nje wabunge waliokuwa wakizua vurugu mda mfupi kabla ya kusomwa kwa makadio ya Bajeti ya mwaka 2019/2020.

"Walinzi wa bunge watoeni wabunge wote wanaopiga mayowe katika ukumbi wa bunge," alisema Bw. Muturi .

Lakini viongozi hao waliokuwa na hasira waliendelea kupiga mayowe wakisama "Hatutanyanyaswa na wanaume, tumechoka'' hadi pale agizo la Spika lilipotekelezwa.

Inaripotiwa kuwa Bw. Rashid alimshambulia Bi Fatuma katika eneo la kuegesha magari baada ya wao kutofautiana vikali kabla ya kumzaba makofi mbele ya walinzi wao .

Vyombo vya habari nchini Kenya vinaripoti kuwa Rashid alitaka kujua kwa nini Bi Gedi - ambaye ni mwanachama wa kamati ya bajeti - hakuitengea mgao wa fedha eneo bunge la Wajir Mashariki wakati kamati ya bejeti ilipozuru eneo hilo hivi karibuni.

Ruka X ujumbe, 2
Ruhusu maudhui? (Mitandao ya kijamii)

Mkala hii imebeba madhui yaliyotoka kwenye mitandao ya kijamii. Tunaomba ruhusa yako kabla kitu chochote hakija pakiwa, sababu wanaweza wakawa wanatumia Cookies na tekinolojia nyingine. Unaweza ukasoma sera sera ya kutumia cookies katika mitandao ya kijamii kabla ya kukubali. Kutazama maudhui haya chagua accept and continue

Onyo: Imetoka kwingine na inaweza kuwa na matangazo

Mwisho wa X ujumbe, 2

Mwakilishi wa wanawake wa Homabay Magharibi mwa Kenya Gladys Wanga amethibitisha kushuhudia tukio hilo kwani alikuwa akiandamana na Bi Gedi.

Katika picha iliyosambazwa, Gedi anaonekana akitokwa na machozi kadhalika kuonekana kuwa na matone ya damu mdomoni.

Kisa hicho kimezua mjadala mkali katika mitandao ya kijamii nchini Kenya huku wengi wamuelekezea Bw. Rashid ghadhabu zao.

Kwa kutumia hushtag #JusticeForFatumaGedi katika mtandao wa kijamii wa Twitter Wakenya wamekua wakishinikiza mbunge Fatuma Gedi.

Ruka X ujumbe, 3
Ruhusu maudhui? (Mitandao ya kijamii)

Mkala hii imebeba madhui yaliyotoka kwenye mitandao ya kijamii. Tunaomba ruhusa yako kabla kitu chochote hakija pakiwa, sababu wanaweza wakawa wanatumia Cookies na tekinolojia nyingine. Unaweza ukasoma sera sera ya kutumia cookies katika mitandao ya kijamii kabla ya kukubali. Kutazama maudhui haya chagua accept and continue

Onyo: Imetoka kwingine na inaweza kuwa na matangazo

Mwisho wa X ujumbe, 3

Tayari mbuge Fatuma Gedi amewasilisha rasmi ripoti kwa polisi kuhusiana na kisa hicho.

Ruka X ujumbe, 4
Ruhusu maudhui? (Mitandao ya kijamii)

Mkala hii imebeba madhui yaliyotoka kwenye mitandao ya kijamii. Tunaomba ruhusa yako kabla kitu chochote hakija pakiwa, sababu wanaweza wakawa wanatumia Cookies na tekinolojia nyingine. Unaweza ukasoma sera sera ya kutumia cookies katika mitandao ya kijamii kabla ya kukubali. Kutazama maudhui haya chagua accept and continue

Onyo: Imetoka kwingine na inaweza kuwa na matangazo

Mwisho wa X ujumbe, 4

Mbunge, Rashid Khasim anazuiliwa katika kituo cha polisi.

Purukushani hilo ambalo lilichukua karibu nusu saa lilitulia baadae na wabunge hao wakarejea bungeni.