Mashambulizi Sri Lanka: India yamkamata mtu anayeshukiwa kutekeleza mashambulizi

Watu zaidi ya 250 walipoteza maisha katika mashambulizi siku ya Pasaka nchini Sri Lanka

Chanzo cha picha, Anadolu Agency/Getty Images

Maelezo ya picha, Watu zaidi ya 250 walipoteza maisha katika mashambulizi siku ya Pasaka nchini Sri Lanka
Muda wa kusoma: Dakika 2

Wapelelezi kutoka taasisi ya kupambana na ugaidi nchini India wamemkamata mtu mmoja anayeshukiwa kuwa na uhusiano na mtu aliyejitoa muhanga wakati wa matukio ya mashambulizi ya siku ya Pasaka nchini Sri Lanka.

Maafisa wa upelelezi wamesema Mohammad Azharuddin, 32, alikua rafiki na Zahran Hashim kwenye mtandao wa Facebook, mtu anayedaiwa kuwa mpangaji wa mashambulizi, kama ilivyodawaiwa na wanamgambo wa Islamic State (IS).

Kukamatwa huko kulikuja baada ya kuvamia mahabusu inayoshukiwa kuwa ya wanamgambo wa IS katika mji wa kusini mwa India, Coimbatore.

Mashambulizi ya mabomu talisababisha vifo vya zaidi ya watu 250 na kuwajeruhi 500 wengine .

Watu wengine watano wamekamatwa kwa ajili ya mahojiano, limeeleza shirika la upelelezi la India (NIA), ambao walivamia eneo hilo na kuwakamata.

Ilifungua kesi dhidi ya Bwana Azharuddin na wengine tarehe 30 mwezi Mei, kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa kwa waandishi wa habari.

Maafisa wa intelijensia na polisi wanaendelea na msako hasa katika mji wa Ukkadam, jirani na mji wa Coimbatore, ambapo maafisa wanasema washukiwa watatu, akiwemo Azharuddin, wanaishi.

Ruka X ujumbe
Ruhusu maudhui? (Mitandao ya kijamii)

Mkala hii imebeba madhui yaliyotoka kwenye mitandao ya kijamii. Tunaomba ruhusa yako kabla kitu chochote hakija pakiwa, sababu wanaweza wakawa wanatumia Cookies na tekinolojia nyingine. Unaweza ukasoma sera sera ya kutumia cookies katika mitandao ya kijamii kabla ya kukubali. Kutazama maudhui haya chagua accept and continue

Onyo: Imetoka kwingine na inaweza kuwa na matangazo

Mwisho wa X ujumbe

Mamlaka nchini humo zinawashutumu washukiwa sita kwa kupandikiza propaganda za IS na kujaribu kuwavuta ''vijana '' kutekeleza mashambulizi kusini mwa India, ikiwemo jimbo la Tamil Nadu, jimbo ambalo mji wa Coimbatore unapatikana.

Zahran Hashim
Maelezo ya picha, Zahran Hashim anadaiwa kuwa kiongozi wa waliotekeleza mashambulizi ya mabomu

Mamlaka nchini Sri Lanka zimekana ripoti kuwa zimeshindwa kufanyia kazi tahadhari zilizotolewa Marekani na idara ya intelijensia ya india kuhusu kuwepo kwa tishio la mashambulizi.

Taasisi ya NIA imekuwa na mfululizo wa msako kusini mwa India tangu mwezi Aprili .

Mwezi Aprili mtu mmoja alikamatwa katika jimbo la Kerala ambaye alikua anashutumiwa kupanga shambulio la kujitoa muhanga.

Watu kadhaa pia wanaoshukiwa kuwa na mahusiano na wanamgambo wa IS walishutumiwa kupanga mashambulizi mjini Delhi, shirika la habari la Uingereza, Reuters limeripoti.