Abubakar Shekau: Kiongozi wa Boko Haram 'atatizika kusoma' katika kanda mpya ya video Nigeria

Shekau anaonekana akipata tataizo la kusoma

Chanzo cha picha, Boko Haram

Muda wa kusoma: Dakika 2

Kiongozi wa kundi la Boko haram nchini Nigeria Abubakr Shekau , amejitokeza katika video mpya ikiwa ni ya kwanza baada ya kipindi cha mwaka mmoja.

Katika video hiyo, iliotolewa ili kuadhimisha kukamilika kwa mwezi mtukufu wa Ramadhan , kiongozi huyo alizungumza kwa lugha ya Kiarabu na kuonekana kutatizika kuona, kutokana na vile alivyokuwa akipata matatizo ya kusoma maandishi yake.

Katika ujumbe wake kiongozi huyo alipinga demokrasia na kutetea sera za kundi hilo za chuki dhidi ya elimu ya dunia na chochote kinachohusiana na utamaduni wa magharibi.

Hakuna lolote jipya isipokuwa wakati ambao kanda hiyo imetolewa ni muhimu na huenda inatuma ujumbe wa moja kwa moja kwa serikali ya Nigeria.

Lengo la kanda hiyo ya video

Rais Muhammadu Buhari aliapishwa kwa muhula wa pili wiki iliopita huku taifa hilo likiwa miaka 20 tangu kurudi kwa demokrasia- mfumo wa serikali ambao kundi la Boko haram limekuwa likijaribu kuupindua ili kuweka sheria ya kiislamu.

Ruka X ujumbe, 1
Ruhusu maudhui? (Mitandao ya kijamii)

Mkala hii imebeba madhui yaliyotoka kwenye mitandao ya kijamii. Tunaomba ruhusa yako kabla kitu chochote hakija pakiwa, sababu wanaweza wakawa wanatumia Cookies na tekinolojia nyingine. Unaweza ukasoma sera sera ya kutumia cookies katika mitandao ya kijamii kabla ya kukubali. Kutazama maudhui haya chagua accept and continue

Onyo: Imetoka kwingine na inaweza kuwa na matangazo

Mwisho wa X ujumbe, 1

Ruka X ujumbe, 2
Ruhusu maudhui? (Mitandao ya kijamii)

Mkala hii imebeba madhui yaliyotoka kwenye mitandao ya kijamii. Tunaomba ruhusa yako kabla kitu chochote hakija pakiwa, sababu wanaweza wakawa wanatumia Cookies na tekinolojia nyingine. Unaweza ukasoma sera sera ya kutumia cookies katika mitandao ya kijamii kabla ya kukubali. Kutazama maudhui haya chagua accept and continue

Onyo: Imetoka kwingine na inaweza kuwa na matangazo

Mwisho wa X ujumbe, 2

Inonekana kwamba bwana Shekau anajaribu kutoa ishara kwamba yeye na kundi lake bado wapo licha ya kwamba kundi la Boki haram linaloshirikiaa na wapiganaji wa islamic State IS ndilo linaloonekana kutekeleza mashambulio mengi kaskazini mashariki mwa Nigeria.

Shekau ambaye ameliongoza kundi la Boko haram kwa muongo mmoja , alianzisha ushirikiano na IS 2015, akiliita kundi hilo Islamic State mkoa wa Afrika magharibi (iswap).

Ujumbe huo unaonekana kulilenga jeshi ambalo hivi karibuni lilisema kuwa mashambulizi yake yalilishinda kundi la Boko Haram, ijapokuwa limekiri kwamba kundi la Iswap ni changamoto kubwa.

Kundi la Iswap latoa changomoto kwa Boko Haram

Lakini mwaka uliofuata, kundi hilo lilivunjika baada ya IS kumfuta kazi Shekau, kwa kutekeleza mashambulizi bila kujali raia wakiwemo Wislamu , wanawake na watoto.

Shekau na kundi lake la Boko Haram waliendelea kufanya mashambulizi yao tofauti na kundi la Iswap.

Uasi wa miaka 10 wa kundi la Boko Haram nchini Nigeria - na nchi nyingine kadhaa - umewaua zaidi ya watu 20,000 na kulazimisha mamilioni ya wengine kutoroka makaazi yao.