Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Utafiti: Madaktari na wagonjwa watofautiana kuhusu dalili za kuvimbiwa
Madaktari na watu wanatofautiana kuhusu dalili ya kuvimbiwa hali ambayo huenda ikawaacha baadhi ya watu bila ushauri au matibabu wanayohitaji, watafiti wanasema.
Huku wataalamu wa matibabu wanapofikiria kuwa kutopata haja kubwa mara kwa mara ni moja ya dalili kuu ya kuvimbiwa, chini ya thuluthi ya watu wanapinga hilo, kwa mujibu wa utafiti.
Kundi hilo la wataalamu kutoka chuo cha King's College mjini London lilisema kuwa maana mpya ya neno kuvimbiwa inahitajika kutolewa, kulingana na hali binafsi ya wagonjwa.
"Hii inaashiria kuwa mwiko wa haja kubwa umekwisha," Shirika la Guts UK lilisema.
Kuvimbiwa ni hali ambayo inawapata watu wengi na inasadikiwa kuwa mtu mmoja kati ya watu saba wanaojipata katika hali hiyo huchukuliwa kuwa wenye afya.
Inamaanisha kuwa na tatizo la kupata choo au kwenda haja kubwa wakati kama kawaida - lakini jinsi inavyotibiwa hutofautiana pakubwa.
Watafiti wanasema orodha hii ifuatayo huenda ikasaidia kupata maaana mpya ya kuvumbiwa:
- Kujihisi maumivu ya tumbo, kuumwa na kufura tumbo- nguo kutokutosha kama kawaida
- Kuumwa na njua ya haja kubwa- wakati mwingine kutokwa na damu kutokana na hali ya kujikamua kwa nguvu ukijaribu kupata choo
- Kukosa kupata choo mara kwa mara au kupata choo kigumu - mara nyingi huwa kutoka mara tatu kwa siku hadi siku moja kwa wiki
- Kutoka chooni ukiwa na hisia kuwa hujamaliza haja
- Kufura tumbo na- kutoa hewa mara kwa mara
- Kutokwa na damu katika njia ya haja kubwa
Orodha hii inazingatia vigezo gani?
Watafiti waliwahoji watu wa kawaidi 2,557, watu 411 waliyovimbiwa na wataalamu wa magonjwa ya tumbo 365 na kuchapisha matokeo ya utafiti huo katika Jarida la Marekani la Gastroenterolojia.
Waligundua kuwa watu wengi wanafikiria dalili za kuvimbiwa hazijajumuishwa katika mwongozo wowote rasmi wa matibabu
Hii ni pamoja na:
- Kuchukua muda mrefu chooni lakini unashindwa kupata choo
- Kukosa utulivu
- Kuhitaji dawa za kutuliza hali ya kuvimbiwa
Japo idadi kubwa ya watu waliyosema wamevimbiwa walikuwa na dalili zilizoshabihiana na zile zilizotolewa katika mwongozo rasmi, mmoja kati ya kilawatu watatu hawakuwa na ufahamu kuhusu dalili zao binafsi wakati wamevimbiwa.
Madaktari na wagonjwa hawakubaliani kuhusu dalili za kuvimbiwa, Utafiti ulibaini.
Wataalamu wa matibabu wameweka msisitizo zaidi katika hali ya kuenda haja kubwa mara kwa mara kama dalili kuu lakini ni nusu ya watu waliyohojiwa waliyobaini kujipata na dalili hii.
Wataalamu wanasema nini?
Dr Eirini Dimidi, mmoja wa watafiti waliyohusika kutoka King's College London, amesema: "Utafiti wetu huenda ukaonesha kuwa watu wanatafuta msaada wa kupata ushauri kuhusu jinsi ya kubaini ikiwa wamevimbiwa na jinsi ya kushughulikia hali hiyo."
Alisema kuvimbiwa mara nyingi kuvimbiwa hutokana na ukosefu wa lishe iliyo na vyakula vya nyuzinyuzi lakini huenda kuna sababu nyingine ambayo huenda ikasababisha hali hiyo kama vile saratani ya njia ya kupitisha haja kubwa.
Dr Dimidi amesema"ni vyema kupata ushauri wa daktari ukijipata na dalili zinazosababisha kuvimbiwa".
Kuwasiliza wagonjwa wanakizungumzia suala la kuvimbiwa ni muhimu, alisema Julie Harrington, kutoka shirika la Guts UK.
"Wagonjwa ni wataalamu, kutokana kile wanachoshuhudia katika miili yao, wakiungana na wataalamu wa matibabu, utakuwa jambo jema."
Kuvimbiwa kunatofautiana na watu wanapata dalili tofauti, aliongeza.
"Ukosefu wa kwenda haja kubwa mara nyingi hakuhusishwi na tatizo la kuvimbiwa kwa sababu watu husubiri miezi kati ya 6-12 kabla ya kuelezea tatizo hilo kwa kuogopa ama kuona haya.
"Ni vyema kuuelewe mwili wako."
watu wanatakiwa kwenda haja kubwa mara ngapi?
Ni vigummu kiujibu swali hili - Lakini majibu hutofautiana kuto mtu mmoja hadi mwingine.
Katika utafiti huu, kwenda haja kubwa mara saba kwa wiki ilionekana kuwa jambo la kawaidi kwa watu ambao hawakuwa na tatizo la kuvimbiwa.
Lakini wataalamu wanasema hali ya kujisikia kwenda haja mara moja au tatu kwa wiki ni jambo la kawaida.
Kwa hivyo mtu anahitaji kujua ni jambo gani la kawaida kwake ili aweze kung'amua mabadiliko yoyote yakijitokeza.
Kuna njia za kutibu hali hiyo?
Watu wengi hufanikiwa kutambua tatizo lao wenyewe ambalo na kujaribu kulitatua kwa kuongeza chakula chenye nyuzinyuzi(fibre) na kunywa maji zaidi kwa mujibu wa ushauri wa NHS
Nyuzinyuzi hupatikana katika vyakula kama vile mkate , pasta, matunda, na nafaka.
Kufanya mazoezi zaidi na chakula mara kwa mara pia kunaweza kusaidia.
Unaweza kununua dawa zakukabiliana na kuvimbiwa ama ubadilishe lishe yako kama hufanyi mazoezi.
Pia ni vyema kutafuta msaada wa kimatibabu tatizo likiongezeka ama ukijipata na dalili zingine.