Jinsi wanawake wa Kimarekani walivyojitengenezea utajiri?

Rihanna

Chanzo cha picha, Kevin Mazur

Maelezo ya picha, Muimbaji aliyegeuka kuwa mjasiliamaliyuko kwenye orodha kutokana na biashara yake ya urembo na nguo za ndani

Jarida la Forbeslimetoa orodha ya majina ya wanawake wa Kimarekani waliohtengeneza utajiri wao wenyewe.

Huku kukiwa kuna idadi ya watu maarufu waliohtajwa , pia kuna wengine kadhaa walioweza kujijengea himaya ya mafanikio yanayohtambulika ya kibiashara.

Tumeangalia baadhi ya utajiri zaidi ya mafanikio ya wanawakena sekta ambazo zimewasaidia kuupata utajiri wao.

Vipodozi hutengeneza pesa

Kylie Jenner

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Kylie Jenner ni mwanamke mdogo zaidi kwenye orodha

Ikiwa unataka kuwa tajiri huenda huenda ukafikiria kuanzisha kampuni ya vipodozi. sekta ya vipodozi na mafuta ya mwili imewainua wanawake 10 kati ya 80 kwenye orodha ya mamilione na mabilionea wote.

Huenda ukashangaa kusikia mjasiliamali wa vipodozi, kulingana na jarida la Forbes, si hata Kylie Jenner bali ni mzaliwa wa Romania Anastasia Soare.

Mfanyabiashara huyo mwanamke anamiliki nembo ya vipodozi ya Anastasia Beverly Hills cosmetics . Bi Soare alihamia Los Angeles mnamo mwaka 1989 na 2000 akaanzisha kampuni yake ya kutengeneza bidhaa za mapodoni ya nyusi au wanja.

Jarida la Forbes sasa linathamanisha nembo yake ya vipodozi kwa kiwango dola bilioni $1.2 juu kidogo ya kampuni ya Kylie Jenner , kampuni ya bidhaa za urembo ya KKW inayomilikiwa na Kim Kardashian West na Fenty Beauty ya Rihanna.

Huda Kattan

Chanzo cha picha, Huda Beauty

Maelezo ya picha, Huda Kattan alianzisha Huda Beautymwaka 2013 na yuko katika namna 36 katika orodha ya jarida la Forbes ya wanawake tajiri zaidi waliojitengenezea utajiri wenyewe nchini Marekani

Huda Kattan pia yuko katika orodha . Wazazi wake wakiwa ni raia wa Iraqi, Kattan alicha kazi yake ya masuala ya fedha na kuwa mwanavipodozi vya mwili. Alianzisha kampuni ya Huda Beauty.

Mamilionea wengine ambao wanaweza kushukuru vipodozi kwa kuwapatia utajiri ni pamoja na wanawake wawili akiwemo mmiliki wa L'Oreal. Toni Ko aliuza vipodozi kwa kutumia nembo yake ya NYX mwaka 2014 katika mkataba ambao ulimtengenezea dola milioni 500

Jamie Kern Lima, ni mtangazaji wa zamani wa televisheni ambaye pia liuza bidhaa zake za vipodozi kwa L'Oreal na akawa mwanamke wa kwanza kuwa mkuruhgenzi mkuu wa Kampuni b

Mwanaridha tajiri wa kike nchini Marekani

Serena Williams

Chanzo cha picha, TPN

Mchezaji nyota wa Tenisi Serena Williams ametajwa kama mwanamke pekee milionea katika sekta ya michezo aliyeweza kujitengenezea utaji wake mwenyewe . Loikielezea ni kwa nini Serena aliweza kuwa kwenye orodha ya Forbes lilisema: "Alikuwa amewekeza katika miradi 34 kwa kipindi cha miaka mitano kupitia kampuni yake ya Serena Ventures. uwekezaji wake ukiwa ni wa dola milioni 10

"Alianzisha kampuni kwa pesa yake mwenyewe iliyouza mavazi moja kw amoja kwa wateja mwaka 2018. Pia anamiliki shea katika kampuni za Miami Dolphins na UFC.

" Ana ushirika na makampuni zaidi ya kumi na taaluma yake ya tenisi ameweza kupata tuzo zenye thamani ya dola milioni 89m kiwango hicho kikiwa ni mara mbili ya mwanamichezo yoyte yule mwanamke wa riadha ."

Mauzo ya Fasheni

Si vipodozi tu na mafuta ya kutunza mwili vinavyowatajirisha wanawake wa Kimarekani wajasiliamali . baadhi wanaweza kushukuru uelewa wao wa mitindo ya mavazi kwa kuwaletea utajiri.

Huku huenda ukiwa ulishasikia majina ya wabunifu wa mitindo kama Vera Wang na Donna Karan, unaweza pia kuwajumuisha Doris Fisher na Jin Sook Chang?

Doris Fisher, mwenye umri wa miaka 87, muasisi mwenza wa maduka yanayouza nguo ya Gap mwaka 1969 na mumewe baada ya wawili hao kuhangaika kutafuta jinzi zinazowatosha , kampuni yao sasa ina thamani ya dola bilioni 2 za kimarekani .

Forever 21

Chanzo cha picha, SOPA Images

Jin Sook Chang ni mwanamke nyuma ya maduka ya nguo za fasheni ya Forever 21, yaliyoanza kama duka dogo la nguo mjini Los Angeles likiitwa Fashion 21.

Kwa sasa maduka hato yanawaajiri maelkfu ya wafanyakazi huku yakiwa na mamia ya matawi kote duniani.

TV na Muziki

Beyonce

Chanzo cha picha, Larry Busacca

Idadi ya wanawake katika fani ya Muziki na televisheni pia wameweza kuonekana katika orodha ya jarida la Forbes. Miongoni mwao ni muandaaji wa kipindi cha mazungumzo cha televisheni nchini Marekani Oprah Winfrey na Ellen DeGeneres wakiwa na utajiri wa dola bilioni 2.6 na dola milioni 330.

Judy Sheindlin, kutoka kipindi cha TV cha Judge Judy ana Hot Bench, pia wametajwa . "Tangu mwaka 2012, Judge Judy ameweza kupata dola milioni $47 kila mwaka kutoka na kip[indi chake.

"Judge Judy kwa sasa yuko katika msimu wa 23 na bado kipindi chake ni nammba moja miongoni mwa vipindi vinavyopeperushwa wakati wa mchana ."

Kutoka ulimwengu wa muziki Madonna, Taylor Swift, Barbra Streisand na Celine Dion wanapata pia pesa, sawa na Beyoncé, huku Forbes likilkokotoa hesabu zake na kusema muimbaji huyo anautajiri wa thamani ya dola milioni $400

Mumewe Beyoncé Jay Z Jumatatu alitajwa kuwa ndiye Bilionea kwa kwanza katika fani ya muziki wa hip hop.