Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Angola: Serikali na Unita zalumbana juu ya mazishi ya Savimbi
Mzozo umeibuka baina yaserikali ya Angola na upinzani juu ya mipango ya kuzika upya mwili wa aliyekuwa kiongozi wa vugugu la waasi wa Unita ambaye kifo chake kilitokea miaka 17 iliyopita na kumaliza vita vya wenyewe kwa wenyewe vilivyodumu kwa karibu miongo mitatu.
Serikali ilikuwa inataka kuukabidhi mwili wa Savimbi kwa wawakilishi wa Unita, ambacho sasa ni chama cha upinzani, ili waweze kuuzika mwili wake nyumbani kwao tarehe Mosi Juni.
Hata hivyo, makabidhiano ya mwili hayakufanyika na kila upande sasa unamlaumu mwingine.
Helena Savimbi, mmoja wa watoto wa kike wa kiongozi huyo wa waasi ameliambia shirika la habari la AFP kwamba serikali haikuheshimu mkataba. "Ni mkanganyiko mkubwaIt's ," alinukuliwa akisema.
Serikali nayo imeishutumu Unita kwa kushindwa kuuchukua mwili Jumanne, kama walivyokubaliana.
Savimbi aliuawa katika mapigano na serikali mwaka 2002, na kuzikwa katika jimbo la magharibi mwa Angola la Moxico. Kifo chake kiliwezesha kufikiwa kwa mkataba wa amani na hatimae kujumuishwa kwa waasi wa Unita katika mchakato wa kisiasa.
Kikiwa ndio chama kikuu cha upinzani , Unita kimekuwa kikifanya kampeni ya kutaka mwili wa Savimbi uzikwe kwa heshima.
Mwili wake uliofufuliwa ulitakiwa kukabidhiwa na serikali kwa Unita The exhumed body was katika Luena, ambao ni mji mkuu wa jimbo la Moxico Jumanne.
Lakini kwa mujibu wa msemaji wa Unita , Alcides Sakala Simoes, serikali ilibadili "akatika dakika za mwisho ", ikisema makabidhiano yatafanyika "Kuito na hatimaye Andulo" - yote ikiw ani miji iliyopo katikati mwa Angola.
" Hatujui ni wapi mwili ulipo ... Wanataka kuikatisha tamaa Unita," aliliambia shirika la habari la AFP. "hii haitasaidia mchakato wa ujenzi wa taifa."
Hata hivyo, waziri wa masuala ya kitaifa Pedro Sebastiao amepuuzilia mbali kauli hizo.
Kwa mujibu wa shirika la habari la taifa hiilo, alisema mwili umekwishapelekwa Luena kama ilivyopangwa lakini Unita haikuwepo kukabidhiwa mwili na umeachwa katika kambi ya jeshi ukisubiri kuchukuliwa na Unita.