Kwa nini baadhi ya vijana hawapendi kutumia kinga?

Condoms of various colours

Chanzo cha picha, iStock

Katika hafla moja ya usiku, Hayley alifurahia kukutana na mvulana aliyesoma naye sekondari.

Alikuwa hajamuona Aaron*, kwa muda mrefu kwa sababu kijana huyo alikuwa jeshini kwa miaka mingi lakini walipoanza kuzungumza walikuwa ni kama wameonana jana.

Kukutana na rafiki yake wa zamani kulisababisha kuvuruga mipango aliyokuwa anaitarajia jinsi muda ulivyokuwa unaenda, maongezi yalibadilika ghafla na mwisho wa siku walienda nyumbani pamoja.

"Ni kama nilifanya maamuzi kama mtu ambaye hajakuwa wakati nilikuwa elimu ya juu," alisema msichana wa miaka 24.

"Tulikuwa tumekunywa na nnadhani kwa sababu hakuwa mtu ambaye simjui ndio maana niliona sawa tu kutotumia kondomu, wakati si kweli kuwa tunajuana sana.

Na baada ya hapo nilianza kuona dalili za ugonjwa wa zinaa."

Baada ya kuambukizwa ugonjwa wa zinaa, Hayley aliwaambia wenzie kuhusu suala la kujikinga.

"Nilichanganyikiwa sana," Nilijiambia mwenyewe kuwa mimi ni mpumbavu , kwa nini niliamini watu ? napaswa kukua.''

Lakini msongo wa mawazo ulimfanya aache kuamini watu pale alipobaini kuwa hata marafiki zake walikuwa wanalalamikia juu ya magonjwa ya zinaa.

Ingawa bado walikuwa wanaendelea kulala na watu bila kutumia kinga" alisema.

A condom next to a pencil

Chanzo cha picha, BBC Three/iStock

Wakati ambao Hayley alivyokuwa anafanya ngono kabla hajakutana na mpenzi wake wa sasa, alikuwa anatumia dawa mara nyingi badala ya kondomu.

Hii ni kwa sababu alikuwa anajiona hayuko huru lakini pia alikuwa anaona kama ni jambo la ajabu kumwambia mwenza wake.

"Wakati huo nilifikiri kuwa ni ujinga au nitamkera,nilikuwa na ile fikra ya kutaka kumridhisha mwanaume" aliongeza.

Kwa Hayley kupata ugonjwa wa zinaa, na kama hatapata tiba, tatizo hilo linaweza kuathiri mfumo wake wa uzazi lilikuwa jambo lililomshtua:

"Sikuwa naliona tatizo kwa namna hiyo kwa kutokutumia kinga, kama unamuamini mtu kweli haupaswi kufanya hivyo kirahisi ."

Test tubes and a plastic container with the acronym STI

Chanzo cha picha, BBC THREE / ISTOCK

Licha ya kuwa somo la kuvalisha kondomu katika ndizi limekuwa likifundisha shuleni na kuacha kumbukumbu kwa wengi , Si Hayley peke yake ndio alishindwa kutekeleza kile alichofundishwa darasani katika maisha ya uhalisia.

Utafiti ambao ulifanywa England , umebaini kuwa vijana kati ya miaka 16-24 walikubali kuwa walikuwa wanafanya ngono na wapenzi wapya bila kutumia kinga. Na utafiti huohuo umebaini kuwa mmoja kati ya kumi, hawajawahi kutumia kondomu.

Wakati huohuo idadi ya watu wanaoripotiwa kupata magonjwa ya zinaa wanaongezeka.

Asilimia 20 ya ongezeko la magonjwa ya zinaa yaliripotiwa nchini Uingereza kati ya mwaka 2016 na 2017.

A condom on a banana

Chanzo cha picha, iStock

Katika jaribio la kupunguza ongezeko la magonjwa ya zinaa, kampeni ya kuhamasisha watu kutumia kondomu ilianzishwa mwaka 2017 kwa kuwaruhusu vijana kupewa kondomu bure.

Lakini kama kondomu zipo kwa wingi na ndio kinga pekee inayoweza kusaidia kuwalinda watu na magonjwa ya zinaa, je ni kwa nini hawatumii?

Sababu moja inayoweza kusababisha watu kutokutumia kondomu, ni umaarufu wa kinga hiyo kushuka na njia nyingine za mpango wa uzazi kufahamika zaidi.

A finger with a condom on it, with a graph showing decline

Chanzo cha picha, BBC Three / iStock

"Zamani nilikuwa nina hofu kubwa juu ya maambukizi ya Ukimwi, tulisikia kuwa Ukimwi unaua hivyo nilikuwa makini zaidi kutumia kondomu wakati ambao nilianza kufanya mapenzi miaka kama kumi iliyopita lakini siku hivi hatari ya kupata maambukizi ya Ukimwi hayatajwi sana hata kwenye vyombo vya habari," Samuel, kijana mwenye miaka 27 alieleza.

"Magonjwa mengine ya zinaa yanaonekana kuwa si magumu kupata tiba kama Ukimwi hivyo watu wanakuwa hawaogopi," Samuel alisema.

HIV medication

Chanzo cha picha, BBC Three / iStock

Utafiti umetoa tahadhari juu ya mimba zisizo tarajiwa na magonjwa ya zinaa yanaweza

Laura*24, amekuwa akitumia kondomu kila wakati mpaka sasa alipopataa mpenzi ingawa awali alikuwa hana mpenzi wa kudumu.

Kwa sasa , huwa anatumia kinga na mpenzi wake mpya pia.

"Kuna mambo mengi ambayo yanaweza yasiende sawa na kuharibu kila kitu ndio maana nnachukua tahadhari," alisema Laura.

"Suala la kutumia kondomu linanisaidia- huwa inanifanya nihisi salama. Nadhani watu wasiopenda kutumia kondomu mara nyingi huwa wana nia zao, ni kama uraibu tu "

Baadhi ya watu huwa wanaona aibu kutumia kondomu.

Josh* alipoteza ubikira wake akiwa na umri wa miaka 26 ndio siku pekee alitumia kondomu.

Hapendi kutumia kondomu katika mahusiano yake, mara nyingi anapenda kutumia vidonge.

A drooping banana with a condom on it

Chanzo cha picha, iStock

Kuna wengine ambao wanahofu ya kutumia kondomu kwa kupata wasiwasi wa kupata madhara.

Vidonge vya mpango wa uzazi huwa ngumu sana.

Kuna baadhi ya wanawake ambao waliwahi kupata madhara kwa kutumia vidonge hivyo, lakini hata kwa kondomu.

Mtaalamu aliongeza kusema kuwa mara nyingine ubora wa hiyo kondomu na ukubwa wake.

A condom next to a tape measure

Chanzo cha picha, iStock

Utafiti mmoja unaona kuwa ni vyema kama kondomu hizo zitabuniwa kwa muundo mzuri ambao utawahamasisha watu kufanya ngono salama.

Muundo huo utakaoweza kuwafanya waweze kutumia kiurahisi na kutoweza kuharibika kwa urahisi pia, labda hata isiweze kupasuka kwa bahati mbaya hata ukiing'ata na meno unapofungua karatasi lake.

Mike Hore's easy to apply condom

Chanzo cha picha, Mike Hore