Mgogoro wa Iran na Marekani: 'Vita haitatokea Iran'

Iranian Foreign Minister Mohammad Javad Zarif is seen in Tokyo, Japan

Chanzo cha picha, Reuters

Maelezo ya picha, Zarif amedai kuwa Trump hataki vita bali watu ambao wamemzunguka ndio wanamsukuma kupigana na Iran.

Waziri wa mambo ya nje wa Iran amesema kuwa haamini kama vita itatokea nchini mwake baada mvutano mkubwa na Marekani.

Mohammad Javad Zarif alizungumza hayo kupitia chombo cha habari cha serikali na kubainisha kuwa Iran haitaki vita na nchi hiyo haina wazo ya kupambana na taifa lolote lile.

Marekani tayari imeshatuma zana za kijeshi ambapo meli za kivita pamoja na ndege za kijeshi zimeonekana nchini humo siku za hivi karibuni, jambo ambalo raia wa Iran wanaona kama vitisho.

Ingawa rais wa Marekani amedai kuwa anataka kuzuia migogoro .

Zarif alisisitiza kuwa Trump hataki vita bali watu ambao wamemzunguka ndio wanamsukuma kutaka kupigana ili kuifanya Marekani kuonekana kuwa na nguvu dhidi ya Iran.

Kwa nini kuna mvutano?

Mgogoro ambao umekuwepo baina ya nchi hizo mbili tangu mwaka jana wakati rais Trump alipojitoa katika mkataba wa kimataifa wa mwaka 2015 uliolenga kumaliza mpango wa nyuklia nchini Iran.

Jambo la kuona makubaliano hayo kuwa na kasoro, Trump aliamua kuweka vikwazo.

Iran iliamua kuacha kutekeleza kile ambacho ilihaidi kufanya mwanzoni mwa mwezi huu na kutishia kuanza kutengeneza tena nyuklia.

Meli na ndege za jeshi zilizotumwa nchini Iran ambazo wafanyakazi wake sio wa dharura wametakiwa kuondoka.

iran

Chanzo cha picha, AFP

Tahadhari ya ndege na meli

Wakati viongozi kutoka pande zote mbili wamesisitiza kuwa hawataki vita itokee, lakini bado mvutano ni mkubwa.

Wanadiplomasia kutoka Marekani wametoa tahadhari kuhusu ndege za kibiashara ambazo zinaenda katika maeneo hayo kuwa ziko hatarini.

Je tishio la Iran linaweza kuzaa vita? Wachambuzi wengi ndani ya Marekani watakujibu hapana.

Wengi wao wanakubaliana na kuibana Iran, na pia kuwapa onyo kali dhidi ya kushambulia maslahi ya Marekani lakini si kufikia kiwango cha vita.

Kitu cha msingi zaidi ni kuwa, hakuna bahati mbaya katika kuanzisha vita, si kitu ambacho hutokea bila watu kujua nini cha kufanya.

Kama vita italipuka basi itakuwa ni maamuzi pambanifu ya viongozi wa mataifa hayo mawili hasimu.