Maandamano mjini Khartoum yasababisha watu sita kuuwawa

Sudan protesters

Chanzo cha picha, Getty Images

Waandamanaji wapatao watano na mtu mmoja wa kikosi cha usalama wameuwawa katika mapigano yaliyotokea katika mji mkuu wa Sudan , Khartoum.

Watu hao waliuwawa kwa risasi wakiwa nje ya makao makuu ya jeshi na wengine kadhaa kujeruhiwa wakati ambapo raia walikuwa wanaandamana kudai serikali kuongozwa na raia.

Waandamanaji wanasema askari walikuwa wanahusika na tukio hilo ingawa askari wenyewe wanakana kuhusika na tukio hilo na kuwalaumu watu wasiojulikana.

Sudan imekuwwa katika serikali ya mpito tangu mwezi uliopita mara baada ya rais Omar al- Bashir kuondolewa madarakani.

Waandamanaji wamekuwa wakiandamana kuzunguka makao makuu ya jeshi tangu tarehe 6 mwezi Aprili , siku tano mara baada ya jeshi kumpindua Omar al-Bashir ambaye alitawala Sudan kwa miaka 30.

Bashir aliondolewa madarakani tarehe 11 Aprili baada ya kuongoza kwa miaka 30.

Chanzo cha picha, AFP

Maelezo ya picha, Bashir aliondolewa madarakani tarehe 11 Aprili baada ya kuongoza kwa miaka 30.

"Nilipigwa na kubaki na majeraha mawili. Hawa watu hawajielewi kabisa kwa sababu bado niko hai. Mwanaume aliyenipiga nilimwambia kuwa kwa jina la mama yake mpendwa, kama ataniua , aniue sasa. na nitaenda kwa Mungu" mtu aliyejeruhiwa katika maandamano.

"Alinipiga risasi akiwa kama mita 20 mbali na mimi. Aliponiona tu akaamua kunipa risasi kwa maksudi.

Hakunipiga risasi kwenye mguu au angani , alinipiga kifuani kwa malengo ya kuniua kabisa na sio kunitisha ," mtu mwingine aliyepigwa risasi na kujeruhiwa.

Tayari mazungumzo kati ya utawala wa kijeshi na walioandaa maandamano umeanza kuonyesha kuwa na matumaini .

Hata hivyo kabla ya usiku wa jumatatu, pande zote mbili zilitangaza kukubaliana kuandaa muundo mpya wa uongozi.

Wanaume waliokuwa wakipiga risasi mtaani walionekana kugawanyika katika pande mbili.

Baadhi ya askari walionekana kutofurahishwa na namna watu walivyokuwa wanaendelea kukaa nje ya makao makuu ya jeshi ingawa waandamanaji walikuwa wanahisi kuwa hawawezi kuacha kukaa barabarani mpaka wapate wanachokitaka.

Arial view of protesters in Sudan

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Maandamano yalianza mwezi Desemba

Hali hii imefikaje hapo?

Mwezi Desemba , waandamanaji walianza kuandamana dhidi ya maamuzi ya serikali katika mgawanyiko wa uongozi mara baada ya rais aliyeongoza miaka 30 kuondolewa madarakani.

Katika wiki tano za maandamano , tarehe 17 Januari, watu walioshihudia kikosi cha usalama wakirusha bomu la machozi na kusababisha mauaji ya daktari.

Daktari huyo ambaye alikuwa anatibu watu waliojeruhiwa katika maandamano nyumbani kwake Khartoum , wakati ambao polisi walirusha bomu la machozi katika jengo lake. ,

Shuhuda aliiambia BBC kuwa daktari ni miongoni mwa watu wengi waliouwawa wakati ambapo waandamanaji walikuwa wanapinga serikali.

Baraza la uongozi wa jeshi lilichukua utawala tangu April 11 lakini waandamanaji walisisitiza uongozi ukabidhiwe kwa raia jambo ambalo lilikuwa linapingwa na utawala wa kijeshi.