Siku ya mama duniani : Uraibu wa pombe ulivyodhoofisha uhusiano wa mama na mtoto

Chanzo cha picha, Getty Images
Simulizi ya binti aliyekuzwa na mama mwenye uraibu wa pombe, Ella ambalo sio jina lake halisi.
Jina langu ni Ella, nna umri wa miaka 26, kile ambacho ninakikumbuka kuhusu mama yangu ni kuwa alikuwa anakunywa pombe kupita kiasi.
Uhusiano wangu na yeye haukuwa mzuri kutokana pombe.
Hiyo sio sababu pekee iliyonifanya kuwa na tatizo la pombe pia.
Kiuhalisia ninafahamu vizuri muda wa kunywa pombe na muda ambao sio mzuri kunywa lakini kutokana na sababu mbili kuu zinanifanya ninywe.
Mimi ni mtu mcheshi na pombe inaongezea uchangamfu.
Ingawa pombe hii hii imeondoa uhusiano wangu na mama yangu, mtu ambaye alinileta katika ulimwengu huu, akanipenda na kunijali na asingeweza kumchagua mtu mwingine zaidi yangu.
Na kwa sababu hiyo nnajikuta nnaipenda pombe na nnaichukia pombe.
Nnapenda jinsi pombe inavyoweza kujumuisha watu pamoja ingawa inaweza kuwagawa watu pia.

Chanzo cha picha, Getty Images
Nimekulia katika mji ulio karibu na bahari na familia yangu ilikuwa ina kila kitu ambacho tulikihitaji na hata zaidi.
Matatizo yalianza wakati nimekuwa kidogo kipindi ambacho mama yangu alianza kuitegemea pombe zaidi na hata akaanza kurukwa na akili.
Nina kumbukumbu nyingio zinaniumiza na hata ilifikia wakati sitaki kusheherekea siku yangu ya kuzaliwa kwa hofu ya kupata aibu kutoka kwa watoto wenzangu ikiwa wangemuona mama yangu amelewa.
Tabia yake ya kunywa kupita kiasi ilimfanya auze nyumba , mahusiano yake yasiwe mazuri na hivyo kupewa talaka, alinifanya nisumbuke wakati wa mitihani kwa sababu alikuwa anachukua komputa.
Vilevile nilikuwa nakosa kadi za pongezi za kusheherekea siku zangu za kuzaliwa, tulikuwa tunakwenda hospitali kila mara , nilikuwa najikataa, kujilaumu na kujiona mkosaji.
Nilikosa upendo kutoka kwa watu niliowapenda katika maisha yangu.
Mama yangu alichagua pombe kuliko mimi na dada zangu.

Chanzo cha picha, Getty Images
Alikuwa anaumwa sana. Alikuwa hakubali kuacha uraibu wake na hata mambo aliyokuwa anayafanya vilikuwa sio vitendo vyake yeye mwenyewe binafsi bali ni kutokana na uraibu wa pombe.
Maisha yalikuwa magumu kwangu na dada zangu , yani hayaelezeki kwa watu kwa nini hayupo katika maisha yetu.
Kwa miaka mingi , ilituwia vigumu kukabiliana na hali hiyo ya kumpoteza mtu ambaye alikuwa hai.
Ni vigumu kukumbuka wakati mzuri ambao tulikuwa pamoja kwa sababu akili huwa ainaamua kuchagua karibu kila kitu ambacho nilipitia nilipokuwa mdogo.
Lakini ni kama watu wengine tulkuwa na wakati mzuri na siku ambazo hazikuwa nzuri.
Siku ambayo ilikuwa mbaya zaidi ya nyingine ilikuwa tarehe 22 Agosti mwaka jana, tulipomkuta amepata mshtuko wa moyo.
Hivyo mwaka huu nnasheherekea siku ya mama duniani huku mama yangu akiwa hayupo tena.
Ingawa alikuwa hayupo karibu na maisha yangu kwa takribani miaka tisa.

Chanzo cha picha, Getty Images
Mara nyingi nimekuwa nnatamani kupata ushari kutoka kwa mama yangu lakini siwezi kupata tena.
Siku kama hii ya kukumbuka mama inakumbusha maumivu makali ambayo nimepitia katika maisha yangu lakini nimeamua kusheherekea siku hii na watu wote ambao walijitahidi kunilea kwa namna moja au nyingine.
Nilipata mbadala wa mama ambao ni baba yangu, dada zangu, shangazi, binamu na marafiki zangu ambao walinipenda , awalinifundisha na kunisaidia kukua vyema.
Pamoja na yote niliyopitia ,nnajiona mtu mwenye bahati.
Ninajiona ni mtu mwenye bahati kuwa na mama kama yeye kabla hajapata uraibu ambao ulichukua maisha yake lakini vilevile ninajiona mwenye bahati kuwa na baba anayejali, dada na bibi ambao wamenikuza vyema.
Nina faraja kwa kuwa nna marafiki wazuri, kazi nzuri na kumbukumbu nzuri katika maisha.













