Kondoo wapelekwa shule Ufaransa

A photograph of freshly-shorn sheep in southeastern France

Chanzo cha picha, AFP/Getty

Muda wa kusoma: Dakika 1

Mkulima mmoja nchini Ufaransa amewaandikisha shule kondoo wake 15 ili kuongeza namba ya wanafunzi baada ya mamlaka za kijiji kimoja kutangaza kutaka kusitisha masomo.

Shule ya Jules Ferry iliyopo kwenye kijiji cha Crêts-en-Belledonne, kwenye safu za milima ya Alps karibu na jiji la Grenoble, kimekuwa kikikumbwa na tatizo la kushuka kwa namba ya wanafunzi wanaoandikishwa kwa masomo.

Hali hiyo inatishia kufungwa kwa shule hiyo.

Lakini kama hatua ya kupinga kufungwa kwa shule, mfugaji na mkulima Michel Girerd ameamua kuwaandikisha baadhi ya kondoo wake kama wanafunzi.

Baadhi ya kwanafunzi hao ambao ni kondoo wanafamika kwa majina kama Baa-bete, Dolly na Shaun.

Ruka X ujumbe
Ruhusu maudhui? (Mitandao ya kijamii)

Mkala hii imebeba madhui yaliyotoka kwenye mitandao ya kijamii. Tunaomba ruhusa yako kabla kitu chochote hakija pakiwa, sababu wanaweza wakawa wanatumia Cookies na tekinolojia nyingine. Unaweza ukasoma sera sera ya kutumia cookies katika mitandao ya kijamii kabla ya kukubali. Kutazama maudhui haya chagua accept and continue

Onyo: Imetoka kwingine na inaweza kuwa na matangazo

Mwisho wa X ujumbe

Presentational white space

Bw Girerd alienda shuleni hapo akiwa na kondoo 50 kuhudhuria sherehe maalumu iliyohudhuriwa na watu 200 wakiwemo wanafunzi, walimu na maafisaa wengine.

Meya wa eneo hilo, Jean-Louis Maret alikabidhiwa vyeti vya kuzaliwa vya 'wanafunzi' hao wapya. Pia akaonesha kukerwa kwake na suala la kutishia kufunga shule hiyo kutokana na uhaba wa wanafunzi.

"Sasa hakutakuwa na tishio la kufungwa kwa kitu chochote," moja ya wazazi Gaelle Laval amesema, na kuongeza kuwa mfumo wa elimu "hauangalii hoja zilizopo katika eneo hilo, na badala yake unaangalia idadi (ya wanafunzi) tu."

Wanafunzi waliohudhuria sherehe hiyo walibeba mabango yalikuwa na ujumbe kuwa: "Sisi siyo kondoo".

Presentational grey line